Mzibua Vyoo
Senior Member
- Nov 8, 2023
- 108
- 241
Wakuu, hii nimeikopi sehemu.
MAELEZO YANGU:
Wanaume tunahangaika kujipa ukamilifu ili tuweze kumdhibiti kiumbe anayeitwa mwanamke. Wasakatonge na wajanja kwa kuliona hili, wameamua kutumia mwanya huu kujipatia pesa.
COPY & PASTE
SIFA ZA MWANAUME LEGELEGE (FEMININE MAN)
KWANINI WANAUME LEGELEGE HUVUTIWA KIMAPENZI NA WANAWAKE WABABE NDANI YA FAMILIA
Hakuna familia imara inayoongozwa na baba dhaifu /baba legelege.
baba legelege sio huleta mateso kwa watoto bali huwa chanzo cha manyanyaso kwa mama watoto wake.
Baba legelege huwa hawezi kusimama kama kiongozi shupavu ndani ya familia badala yake anakuwa na gubu, kisirani,wivu,kususa, kununa,kutangaza madhaifu ya familia yake mtaani,huwa anaruhusu ndugu zake kumdhalilisha mke/mchumba wake,huwa anaruhusu mama yake mzazi kumdhalilisha mke/mchumba wake,huwa hana msimamo anaishi kwa kuendeshwa na maoni ya kila mtu.
Wengi huwa wanadhani mwanaume shupavu ni dikteta, mnyanyasaji, aenatesa mke/mchumba wake pamoja na watoto haipo hivyo.
Kwanini wanawake wenye tabia nzuri,wenye nia ya kujenga familia imara huparamia wanaume ambao hawaeleweki?
Kwanini wanaume wenye tabia nzuri kwenye jamii huparamia wanawake wenye tabia za ubabe, ukali kupitiliza, kiburi, jeuri, dharau na majivuno?
Kwanini ukiwa mtu mstaarabu sana unapata mwenza asiekuwa na shukurani,asiekuwa na huruma, mbinafsi na mchoyo kupitiliza?
Yote hayo utayaona ndani ya ujumbe huu wa leo.Kutoka ndani ya kitabu cha JINSI YA KUPONA MAUMIVU MAKALI SANA MOYONI ukurasa wa 98.
Tuanze na sifa za mwanaume legelege,kisha sifa za Mwanamke ambaye huvutiwa kimapenzi na mwanaume legelege kisha tuangalie namna mwanaume legelege anaweza kupata mwenza mwenye heshima, utulivu na mshikamano ndani ya familia.
SIFA ZA MWANAUME LEGELEGE
Mwanaume legelege (feminine man,weak man) huwa na sifa zifuatazo
1.Huwa anataka kupendwa na Mwanamke badala ya kuheshimiwa
(Mwanaume Rijali huwa hana shida ya kupendwa na Mwanamke) lakini mwanaume legelege kipaumbele chake ni kupendwa na Mwanamke tu
Kitendo cha kutaka kupendwa sana husababisha anakuwa mvumilivu sana wa tabia zenye udhalilishaji, dharau, kiburi, kugombezwa, kukaripiwa, kutolewa dosari za muonekano, kunyimwa unyumba.
Mwanaume legelege huwa yupo tayari kutumia fedha nyingi sana,kutoa ushauri, kukumbusha wema ambao amemfanyia Mwanamke,kusamehe kila kosa ambalo Mwanamke atafanya kwa lengo la kuhakikisha anapendwa sana kuliko mtu yeyote.
Hitaji la Mwanamke huwa ni kupendwa ndio maana Mwanamke anakuwa mvumilivu wa usaliti, vipigo, matusi, kugombezwa, kukaripiwa - vilevile kwa mwanaume legelege kipaumbele chake huwa kupendwa tu jambo ambalo ni kosa kubwa sana.
2.HAJUI ANATAKA NINI
Mwanaume legelege huwa hana kipaumbele maishani mwake zaidi ya kufurahisha Watu wengine.Kwa mfano mwanaume legelege (feminine man) anaamini anatakiwa kujitoa mhanga kwa ajili ya kumfurahisha, kumridhisha Mwanamke nyakati zote ili apate kupendwa sana kuliko wanaume wengine.
Mwanaume legelege hajui nini ambacho Mwanamke anatakiwa kumfanyia ili yeye (mwanaume) avutiwe kimapenzi na Mwanamke ) hali hiyo husababisha Wife material kujitenga nao.Hampi nafasi Mwanamke aonyeshe sifa nzuri .Matokeo yake "Wife material" huonyesha sifa zao nzuri kwa wanaume ambao ni "bad boy, players" ambao hawana mpango wa kujenga familia.
3.HUWA ANAJIONA MKOSAJI NA ANAONA KILA MWANAMKE NI MKAMILIFU
Mwanaume legelege huwa anaamini yeye mwenyewe yupo na dosari nyingi sana, mapungufu mengi sana ambayo yatafanya akose mwanamke wa kujenga naye familia.Kisha anaamini kila Mwanamke ni mkamilifu tu tabia hiyo husababisha anajishusha sana kila anapomuona Mwanamke jambo ambalo husababisha "Wife material" kumkwepa kwa sababu "Wife material" huwa wanapenda kujishusha wao mbele ya mwanaume.
Hivyo "Wife material" anahisi yupo na Mwanamke mwenzake .
4.ANAKUWA KING'ANG'ANIZI WA MAPENZI
mwanaume legelege huwa na tabia ya kupiga simu mfululizo,kutuma sms mfululizo hata kama anapiga na kutuma sms lakini hakuna majibu yoyote huwa hakati tamaa.Anaamini akipenda Mwanamke yeyote anatakiwa kukubaliwa.
Huwa anajibu sms na kupokea simu haraka ,huwa anaacha kazi zake na malengo yake ili kupokea simu za Watu wengine anaamini alichelewa kupokea simu na kujibu sms ataonekana mbaya sana matokeo yake anakuwa na marafiki na mwenza asiekuwa mvumilivu hata kidogo.
5.HANA MSIMAMO
Huwa anakubaliana na mawazo ya Mwanamke nyakati zote,akiombwa kiasi chochote cha fedha yupo tayari kutoa hata kwa kukopa jambo ambalo husababisha anapata wanawake ambao wapo kimaslahi (gold digger),huwa anaogopa mahusiano kuvunjika hivyo anaweza kuvumilia makosa ya kila siku ilimradi apate kudumu na mwenza wake.
6.BAADHI HUWA WAPOLE SANA AU WANAKUWA NA GUBU
Baadhi ya wanaume legelege huwa na tabia ya upole kupitiliza, huruma, kunyenyekea, kusamehe makosa, uvumilivu uliopitiliza kisha ghafla anakuwa na hasira kupitiliza, anakuwa na kisirani, atasusa, haongei zaidi ya kulalamika,anaweza kulia , kuomba msamaha,kupiga magoti, kutishia kujiua mara kwa mara.,anakuwa anataka kuonewa huruma na Mwanamke muda wote,anakuwa kama mtoto mbele ya Mwanamke kisha Mwanamke anakuwa kama mama mzazi wa mwanaume.
7.HANA SAUTI YA MAMLAKA
Anaweza kuwa mpole kupitiliza ghafla anakuwa na hasira kupitiliza kiasi cha kulalamika, kunung'unika,kulia,kujiona anaonewa,kujiona ananyanyasika.Badala ya kusimama kama kiongozi ndani ya familia anakuwa kama mtoto mdogo anayetaka kuonewa huruma.Anakubali vitu kwa shingo upande.
8.HAJIAMINI MBELE YA MWANAMKE
Siku zote anajiona anadharauliwa tu.Anakuwa na wivu wa mapenzi uliopindukia kwa kujiona mkosaji tu,au anaweza kuanza malalamiko tu kila wakati vijembe, mafumbo,anakuwa na maneno makali sana yenye lengo la kumkasirisha Mwanamke wake pale ambapo wamekwazana.
Anakuwa na tabia ya kukaa na kinyongo moyoni kwa muda mrefu sana.Anakumbusha makosa ya zamani mara kwa mara au anakaa kimya tu ili kuepuka migogoro ya kimapenzi
Anakuwa na haraka na pupa ya kuanzisha mahusiano na Mwanamke ,anakuwa anataka ukaribu uliopitiliza na mwanamke wake..
SIFA ZA MWANAMKE AMBAYE HUVUTIWA KIMAPENZI NA MWANAUME LEGELEGE
Mwanaume legelege huwa anavutiwa kimapenzi na Mwanamke mwenye tabia zifuatazo
1.MWANAMKE NGANGARI ANAETAKA UHURU KUPITILIZA (Strong and independent woman)
Kwa sababu mwanaume legelege hajui sifa za Wife material huwa anaparamia Mwanamke mwenye hulka ya kiume (Masculine woman) - ambaye anakuwa na tabia za ubabe, ukatili, udikteta, udhalilishaji, dharau, majivuno, kiburi na jeuri.
Mwanamke mwenye hulka ya kiume (Masculine woman) anakuwa hashauriki, haambiliki,anakuwa mjuaji,anafanya makosa lakini anageuza kibao kwa mwanaume,siku zote anataka kushindana na wanaume,siku zote anataka kumtawala mwanaume kimabavu na kumpangia sheria.
2.ANAKUWA NA MISIMAMO MIKALI SANA
Mwanamke mwenye hulka ya kiume (Masculine woman) huvutiwa kimapenzi na mwanaume legelege kwa sababu mwanaume legelege huwa yupo tayari kuongozwa ndani ya familia hivyo hali hii husababisha kila mmoja anavutiwa kimapenzi na mwenzake.Mwanamke mwenye misimamo mikali sana anapenda wanaume legelege ambao anaweza kuwagombeza, kuwafokea, kuwatukana, kuwadhalilisha, kuwajibu vibaya
Kwa sababu mwanaume Rijali hawezi kuvutiwa kimapenzi na Mwanamke mwenye misimamo mikali sana kwake inakuwa tishio la mamlaka yake ya kiuongozi ndani ya familia.
3.HATAKI KUKOSOLEWA WALA KUAMBIWA CHA KUFANYA
Mwanaume legelege huvutiwa kimapenzi na Mwanamke ambaye hataki kuambiwa makosa wala mapungufu yake kwa sababu mwanaume legelege mwanzoni tu wa mahusiano huwa anakubali kufuata sheria za Mwanamke hivyo hujikuta anaamini kwamba kama atatoa fedha nyingi sana,kama anakubaliana na kila kitu ambacho Mwanamke atasema basi wataishi kwa amani, utulivu na furaha lakini inakuwa kinyume chake.
Kutokana na hali hiyo mwanaume huishi akiwa na hasira kupitiliza,wivu wa mapenzi uliopindukia, anakuwa na kisirani,anakuwa na gubu kwa muda mrefu sana.
Mwanaume legelege huwa anajieleza sana mbele ya Mwanamke hali hiyo husababisha mwanaume kutuma sms ndefu sana,kupiga simu mfululizo, kutuma sms mfululizo lakini Mwanamke anajibu kwa mkato kisha mwanaume anabaki kulalamika tu.
4.HANA HISIA ZA MAPENZI
Mwanamke mwenye hulka ya kiume (Masculine woman) huwa hana hisia kali za mapenzi hivyo husababisha wanaume Rijali kumkimbia kisha wanaume legelege huona fursa ya kumshawishi, kumbembeleza sana,kujitutumua ili kumfurahisha lakini matokeo yake mwanaume anakuwa kama mtoto na Mwanamke anakuwa kama mama mzazi wa mwanaume.
Mwanamke mwenye hulka ya kiume (Masculine woman) huwa yupo busy sana ,simu hapokei na sms hajibu kwa makusudi hali hiyo husababisha mwanaume legelege kupiga magoti, kutishia kujiua, kutoa ushauri, kukumbusha wema wa zamani,kupiga simu mfululizo, kutuma sms mfululizo lakini Mwanamke anajibu kwa mkato au anakaa kimya.
Kwa mwanaume Rijali akiona Mwanamke anajibu sms kwa mkato anakata mawasiliano papohapo lakini kwa mwanaume legelege inakuwa kinyume chake zaidi anakuwa king'ang'anizi.
5.ANATAKA KILA MTU NA KILA KITU KIWE CHINI YAKE
Mwanamke mwenye hulka ya kiume (Masculine woman) huwa anataka kuwa kichwa cha familia,huwa anataka kuwa na kauli ya mwisho kwa kila mtu na kila kitu,anataka kila kitu kifanyike vile ambavyo amepanga yeye na ikiwa haiwezekani basi kisifanyike chochote.
Mwanaume legelege huwa anaogopa mahusiano kuvunjika hivyo huwa anakubali kufuata sheria za Mwanamke kwa shingo upande ili kuepuka migogoro ya kimapenzi matokeo yake mwanaume anakuwa na hasira kupitiliza, anakuwa na wivu wa mapenzi uliopindukia, anakuwa na kisirani, atasusa,atanuna lakini Mwanamke hajali chochote.
SABABU ZA KUPATA MWANAUME LEGELEGE
Mwanaume legelege hupatikana kwa sababu zifuatazo
1.KULELEWA NA BABA LEGELEGE
Familia ambayo baba ni legelege mama hushika usukani na kila kitu hufanywa kwa kufuata sheria na maagizo ya mama na kila mtu anakuwa chini ya mamlaka ya mama.
Mwanaume legelege huwa anajifunza kwamba wanawake wanatakiwa kusimama ngangari ndani ya familia na mwanaume anatakiwa kutii maagizo ili kuepuka migogoro ya kimapenzi.
Familia hiyo mara nyingi mwenye nguvu ya kiuchumi anakuwa mama sio baba,
Hivyo mwanaume legelege huvutiwa kimapenzi na Mwanamke mwenye tabia za ubabe, ukatili, udikteta, udhalilishaji, dharau, majivuno, kiburi na jeuri kwa sababu mwanaume anajishusha sana kwa kila Mwanamke.
2.KULELEWA BILA BABA
Mwanaume legelege anaweza kupatikana kwa sababu amekulia familia ambayo hakuna baba nyumbani labda kwa sababu ya kifo, talaka, kutengana kwa wazazi,baba kuitekeleza familia, baba kusafiri safiri mara kwa mara,mama kupata ujauzito kwa kubakwa au akiwa shuleni,
Hivyo mwanaume legelege anakuwa bila mfano bora wa mwanaume Rijali hivyo sifa za kiume anajifunza kwa mama yake mzazi.
3.KULELEWA NA BABA DIKTETA
Baadhi ya wanaume legelege huwa zao la kupata baba mkali kupitiliza, mwenye hasira kupitiliza, mwenye misimamo mikali sana (rigid),baba hashauriki, haambiliki, anakuwa mjuaji, anafanya makosa lakini anageuza kibao kwa mama au watoto.
Hivyo mtoto wa kiume anajifunza kuwa mpole kupitiliza, mvumilivu sana, mnyenyekevu kupitiliza, king'ang'anizi wa mapenzi,anakuwa anajali sana akiamini hataki kuwa kama baba yake.
Anaamini akiwa tofauti na baba yake atapendwa sana.
UFUMBUZI WAKE
Mwanaume legelege anaweza kubadilika kuwa mwanaume Rijali kwa njia zifuatazo
1.Epuka kupiga simu mfululizo, kutuma sms mfululizo,epuka kulia,epuka kutishia muachane,epuka kutishia kujiua kama Mwanamke akiwa akionyesha jeuri, dharau, kiburi na majivuno mwambie unataka heshima tu sio upendo wa Mwanamke.
2.JITEGEMEE KIHISIA
Ukiwa mpweke acha kusumbua watu,jali afya yako,jali malengo yako na kazi zako.Kazi yako iwe kipaumbele namba moja kisha mapenzi yawe kitu cha ziada.
Hauwezi kupata Mwanamke (Wife material) kama mapenzi ndiyo kipaumbele chako kwa sababu Wife material kipaumbele chao ni mapenzi siyo kazi hivyo mtakuwa balanced (mwanaume kazi-mwanamke mapenzi)
3.AMUA KUWA ROLE MODEL
Kila kitu fanya kama role model kwa watu wengine,hauwezi kujihisi ni mwanaume Rijali kama hauna wafuasi wenye kukuangalia kama kiongozi wao .
Sifa za kiume Masculine man anakuwa kiongozi, mpambanaji, jasiri, shupavu, asiekuwa ogopa,hataki kupendwa bali anataka kuheshimiwa tu.
4.WEKA MIPAKA
Tambua makosa gani hauwezi kusamehe na makosa gani unaweza kusamehe,nini kitafanya mahusiano yako yavunjike kisha kuwa na msimamo eneo hilo.
Sifa ya mwanamke ni uvumilivu lakini mwanaume hana sifa ya uvumilivu.
Ukiwa mwanaume mvumilivu hauwezi kupata Mwanamke Wife material kwa sababu Wife material huwa mvumilivu hawezi kuvutiwa kimapenzi na mtu mwenye sifa za Wife material.
#Spirit_Warrior
#Wounded_Healer
🤺🤺
Imeandikwa na Psychologist
Said Kasege
Temeke,Dar es salaam