Sifikirii kama kuna ulazima wa kuendesha zoezi la sensa ya watu na makazi katika kipindi hiki cha mdororo wa uchumi

Naunga mkono hoja, kwa hali ilivyo hatuhitaji Sensa kwa sasa, labda hadi 2030, serikali ingeshughulikia uchumi wa watu wake na maendeleo mbali mbali, idadi ya watu haina maana kwa sasa. Tuna mambo makubwa ya kitaifa kushughulikia haraka, idadi ya watu haina umuhimu hivyo kwa sasa.
 
Mleta mada huelewi Nini kuhusu sensa,huwezi kuendesha nchi bila ya kuwa na takwimu,labda tutumi njia mbadara ya kuendesha sensa,tunawezi kutumia watendeji wa kata wakatupa takwimu za mahitaji ya msingi.ila sensa lazima ifanyike.
Kujenga barabara kunahitaji kujua idadi ya watu?
Kuajiri waalimu na madaktari inahitaji kujua idadi ya watu?
Kusambaza maji vijijini kunahitaji kujua idadi ya watu?
Miaka yote wanajua idadi ya watu mbona huduma za afya ni mbovu?
Mzungu ndio anajua kutumia sensa kuandaa mipango ya maendeleo ya baadae,
Tanzania hatuna plani zozote za baadae,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…