Sigara na swaga zake zinatulizaje mawazo?

mbere

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2015
Posts
6,967
Reaction score
6,465
Hii kitu unaongea na mtu jambo la msingi linalochosha mawazo, unashanga eti katoa sigara na kuiwasha, pafu 1, 2, eti mawazo yamepungua.

Niliwahi kuvuta mara moja nikaishia kaumwa na Kufua na kupigiwa Kelele na wife kwasababu ya harufu Mbaya.

Wajuzi hebu nambieni, hii swaga inatulizaje mawazo?!
 
Mkuu huo ulevi wa moshi naupinga sana..

Kuna lile dubwana linaitwa sonyo(tumbaku la kusokota na gazeti)
Ni balaaaaaaa
 
Subiri tuone japokuwa na mimi ni mtumiaji pale napokunywa bear
 
Sigara ndani yake iko na Nicotine sasa Nicotine ni aina fulani ya kilevi ambayo ikimwingia mtu kichwani inamfanya awe na mood fulani nzuri so hata kama mtu yuko kwenye msongo wa mawazo anapata relief kwa mda...
 
Sigara ndani yake iko na Nicotine sasa Nicotine ni aina fulani ya kilevi ambayo ikimwingia mtu kichwani inamfanya awe na mood fulani nzuri so hata kama mtu yuko kwenye msongo wa mawazo anapata relief kwa mda...
Nicotine ya sigara inapenda wachache basi
 
Kuna muda nilifikiria kuacha sigara, lakini nilivyo fikiria wapi nimetoka nayo, hakika niliona sigara ni rafiki yangu wa kweli. Nikiwa pekee yangu, alikuwa pembeni yangu, nikiwa na hasira ananituliza, nikiwa na furaha anazidisha kutengeneza tabasamu la xxx, maana moshi unanipiga machoni nakuwa kama jicho moja nafumba, basi naenjoy mpaka rahaa. Na mwisho imenipa msaada sana hasa pale napo kuwa mgeni sehemu, nakutana na wavuta sigara hawanibanii kunipa ramani ya sehemu husika jinsi ya kupata pesa. Nimekubali na nitapenda sigara ndio ije iniue kwa sababu ndio kitu nacho kipenda zaidi na kifo chake ni cha kukaa kitandani. Sitoacha sigara mpaka kifo changu, nipo ladhi nimwache mama chanja lakini sio sigara.
 
Aisee wewe unashawishi wenzio
 
swaga iko, na matatizo yapo...matatizo ni mengi kuliko swaga...

hivi swaga maana yeke nini?
Utathibitisha vipi kuwa matatizo ni mengi kuliko swaga wakati hata maana ya neno swaga hujui?
 
Ukivuta, moshi unatolea puani au mdomoni?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…