Sigara ni kero kwa wasiotumia

Joined
Jun 16, 2024
Posts
45
Reaction score
56
Uvutaji wa sigara hadharani umekuwa kero kubwa sana mitaani na katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu kama vile vituo vya daladala na baadhi ya maduka ya rejareja.

Ikumbukwe kuwa sigara ni hatari zaidi kwa asiyetumia (second-hand smoker), yaani yule ambaye ametulia zake mara ghafla moshi wa sigara unampitia pale alipo.

Wauza maduka nao wamekuwa na utaratibu mbaya sana kwani wanatundika kibiriti au lighter kwenye maduka yao, hivyo mvuta sigara anawashia pale dukani na wakati mwingine kuna wamama na watoto wadogo.

Ushauri: Tustaarabike. Kama unavuta sana sigara, kajifungie chumbani ili upate moshi wote wewe mwenyewe au nenda sehemu ambazo hazina watu.

Na wauza maduka mnaotundika viwashio (kibiriti au lighter), tafuteni utaratibu mwingine.

Nchi za wenzetu kuna maeneo maalum ya kuvutia sigara.

Ni kwa sababu wanaelewa vitu hivi vina madhara, siyo kwa mvutaji tu. Sigara inaweza kusababisha kansa ya mapafu (lung cancer) baada ya kutumia kwa muda mrefu.

 
Yake matangazo ya miaka ya1980, ndio yamefanya watu waone ni kawaida kujivutia popote, tutafika tuu!
 
Kero Kubwa Kwa sasa ni Kuadimka Na Kupanda Bei kwa UBALOZI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…