Mahojiano kwa maneno kati ya Sigrada Mligo na Mwandishi wa habari
Mwandishi: Uliwaza nini kuondoka CHADEMA, kwa sababu tunajua kila kitu kina sababu.
Sigrada Mligo: Niliwasha simu nikakuta mtandaoni, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Mheshimiwa John Heche, anasema kwamba yule binti anatumika na dola kuiua CHADEMA. Hiyo sentensi ya kutumika na dola kuiua CHADEMA pekee yake, ndiyo iliyoniondoa CHADEMA.
Mwandishi: Pamoja na yote hayo, sasa hivi unaimiss CHADEMA? Unatamani urudi CHADEMA?
Sigrada Mligo: Kutamani kurudi, nitakuwa muongo. Au umesahau kwamba nilipigwa ngumi?
Mwandishi: Mhm, tunafahamu kwamba Bunge linaadhimisha miaka mia moja. Wewe kama mbunge unaipimaje, mchango wa Bunge kwa wananchi wa Tanzania?
Sigrada Mligo: Kwa kifupi naweza nikasema Bunge sio msaada kwa wananchi. Lakini pia Bunge ni... ni nini tuseme? Yaani ni taasisi ambayo inatumia gharama kubwa sana kuliendesha. Yaani fedha za Watanzania, asilimia kubwa zinatumika kuliendesha Bunge, halafu matokeo yanayotokana na hilo Bunge ni madogo sana.
Mwandishi: Lakini tunafahamu kwamba hao wabunge wamekaa miaka 20, 30, ndio wabunge ambao wana background kubwa ya Bunge, na mara kadhaa huwa wanasema kwamba ninyi ambao ni wageni bungeni inabidi mnyamaze, wao ni wazoefu. Hilo wewe una... unaliona vipi?
Sigrada Mligo: Ni mentality za kizamani. Yaani mtu anayeamini kwamba kwa sababu yeye amekaa bungeni miaka mingi ndio yaani yeye ndio huenda ndio anaelewa kuliko mbunge aliyefika miezi sita iliyopita. Na kuna wabunge sasa hivi ambao wana vitu kichwani, na wana uwezo wa kuvizungumza. Ila kwa sababu wako monitored na dola... Sijui kama unanielewa? Yaani wao ni wabunge, wanatamani wawe wanazungumza vitu fulani ila hawawezi kuzungumza kwa sababu wako monitored na serikali yao.