Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Wakati wa mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Aprili 8, 2026, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Njombe kupitia chama cha CHAUMMA, Sigrada Mligo, amesema hotuba ya Waziri Mkuu "Ni hotuba ambayo kama huijui Serikali ya Chama cha Mapinduzi, unaweza ukasahau taabu zote. Ni hotuba nzuri sana... lakini njoo kwenye utekelezaji, tunapoteana. Matatizo ndiyo yanaanzia hapo."
Alieleza kuwa mara nyingi Chama Cha Mapinduzi (CCM) huja na sera na mipango ambayo inaonekana kuwa mizuri na yenye nia ya kuwasaidia wananchi, lakini akaonesha wasiwasi juu ya namna utekelezaji wake unavyokwenda chini kwa chini.
Katika hoja yake, aliibua swali la msingi akitaka kufahamu kama tatizo linatokana na watendaji wa chini au wanaoitwa “machawa” (wanaojipendekeza kwa viongozi) ambao wanaweza kuwa wanaharibu utekelezaji wa ahadi hizo. Kauli hiyo ililenga kuibua mjadala juu ya uwajibikaji na ufanisi wa watendaji serikalini, badala ya kupinga sera zenyewe moja kwa moja.