Sigrada Mligo: Mikopo ya asilimia 10 fedha hazitolewi kwa wakati na kiasi kinachotolewa ni kidogo sana

Sigrada Mligo: Mikopo ya asilimia 10 fedha hazitolewi kwa wakati na kiasi kinachotolewa ni kidogo sana

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Njombe Sigrada Mligo Amelalamika kuwa fedha za Halmashauri ya miji hazitolewi kwa wakati na kiasi kinachotolewa ni kidogo sana kulinganisha na maombi: "unaomba pesa leo umekamilisha documenti zote mheshimiwa mwenyekiti unakuja kupata hela mwakani uliomba kikundi kiliomba milioni 50 wanakuja kupata milioni tatu

Aidha Ili kukidhi vigezo vya mikopo ya halmashauri, mwananchi anahitaji andiko la mradi na katiba, mchakato unaoweza kugharimu hadi "laki sita (600,000)" kwa ajili ya mawakili na wataalamu wa IT

Pia soma ~ Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru inachelewesha sana kutoa mikopo ya 10% kwa vijan
 
Mbunge kama anaona ni rahisi atoe fedha zake kama mkopo ndio atajua usumbufu wa kukopesha wabongo. Zaidi ya 40% ya hao wanaocheleweshewa kukopa huwa hawalipi kwa wakati sembuse yeye anataka kila kundi wakiomba milioni 50 wapewe, atakayeomba 80M apewe. Tena eti wasiwe na katiba na wala andiko la mradi. Kwanza ni mbunge gani huyo analalamikia katiba ya kikundi na andiko la mradi kwenye mkopo?

Huyo labda ajadili utoaji wa sadaka na zaka. Ila kama mkopo basi sio hela ya kwenda tu ukachota unaondoka zako.
 
Vigezo na masharti Vizingatiwe.

Mtu hana Taarifa za mauzo + Profit za miezi mitatu nyuma unamwamini vipi mtu huyu?

Hana Leseni , Katiba Na hajajisajili popote.
 
Back
Top Bottom