Sigrada: Nchi hii sasa hivi tumehama kwenye sheria, tunaishi kwa matamko

Sigrada: Nchi hii sasa hivi tumehama kwenye sheria, tunaishi kwa matamko

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mbunge wa Viti Maalum (Mkoa wa Njombe) kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Sigrada Mligo amesema Tanzania imeacha kuongozwa na misingi ya sheria katika baadhi ya masuala na badala yake inaendeshwa kwa matamko, hali ambayo amesema inaathiri utekelezaji wa haki na uhuru wa kisiasa.

Akizungumzia suala la mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, Sigrada alisema sheria za nchi pamoja na Katiba zimetambua na kueleza wazi haki ya vyama kufanya mikutano hiyo, lakini utekelezaji wake umeathiriwa na maamuzi yanayotokana na matamko badala ya sheria.

Soma: Sigrada Mligo: Wabunge tunalipwa hela ya mafuta kulingana na bei iliyoko sokoni siku hiyo ndio maana wabunge hawajadili kupanda kwa mafuta

"Licha ya changamoto zilizopo kwenye sheria zetu, Katiba na sheria za vyama vya siasa zimezungumzia vizuri mikutano ya hadhara. Lakini sasa tumehama kwenye sheria, tunaishi kwa matamko. Leo mtu anatamka jambo, na wote wanafuata alichotamka," alisema.

 
Back
Top Bottom