GE2025 Sigrada: Serikali kuletewa maendeleo si fadhila, ni utaratibu wa kisheria kwa mujibu wa katiba

GE2025 Sigrada: Serikali kuletewa maendeleo si fadhila, ni utaratibu wa kisheria kwa mujibu wa katiba

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mtia nia wa Ubunge wa Jimbo la Njombe Mjini kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Sigrada Mligo, amewataka wananchi wa jimbo hilo kutokuwa waoga wa kudai huduma wanazostahili, akisisitiza kuwa serikali ina wajibu wa kuwafikishia maendeleo kwa mujibu wa sheria na si kama fadhila.

Sigrada ametoa kauli hiyo alipokutana na baadhi ya wanachama wa CHAUMMA na wakazi wa mji wa Njombe, katika mkutano wa mapokezi na utambulisho wake rasmi kama mgombea wa ubunge kupitia chama hicho cha upinzani.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025


“Ninyi mkiletewa ambulance mnashinda mnaimba. Sikilizeni, kuletewa maendeleo si fadhila, ni utaratibu wa kisheria kwa mujibu wa katiba,” amesema Sigrada.

Screenshot 2025-08-11 172930.png
 
Back
Top Bottom