Siiogopi Yanga SC, ila ninauogopa zaidi huu Muunganiko wao Hatari, Tukuka na Mtakatifu ufuatao

Siiogopi Yanga SC, ila ninauogopa zaidi huu Muunganiko wao Hatari, Tukuka na Mtakatifu ufuatao

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Winga ya Kulia Morrison, Winga ya Kushoto Kisinda, Mbele anasimama Mayele halafu nyuma yake kidogo yuko Aziz K huku wote hawa wakiwa Wanatibiwa vyema na Daktari bora kwa sasa ndani ya NBC Premier League Aucho.

Natangaza mapema hapa hapa JamiiForums kuwa nikiwa kama mwana Simba SC Tukuka kwa huu Muunganiko sasa yameshanianza Kugonga na Kurudi Tumboni huku nikiona kabisa kuwa pona pona yetu Simba SC hiyo tarehe 23 Oktoba, 2022 kwa Mkapa ni kuombea tu 85% hawa tajwa hapa wawe Injury au Warogwe vya kutosha na yule Bibi yetu wa Kizanzibari ( Pemba ) mwenye Titi Moja ili wasiwe na Madhara ila ikitokea Njemba zote hizi zikawa 100% Fit nisiwe Mnafiki zile 5 bila au 6 bila tulizowahi Kuwapiga ( Kuwafunga ) zitarudi na hata Kuzidiwa ( nikimaanisha Rekodi ) Kuvunjwa.

Yanga SC wamesajili Kiufundi sana!!!!

Cc: Rais2045
 
Mkuu Gentamycine, uliadimika sana, bora umerudi sasa! Karibu sana

Kuhusu uchambuzi wako wa wachezaji tajwa wa Yanga, ni kweli kwamba mwaka huu Klabu hii imejipanga vyema kwa kuwasajili wachezaji wazuri sana kiufundi. Simba watapata tabu sana kwenye 'Derby' ya wiki ijayo!
 
Kuwa na wachezaji wazuri hakuguarantee kumfunga mwenzako kirahisi hivyo maana kila timu hujipanga kudhibiti njia hizi vema kabisa.

Katika soka ujanja si tu kuwa bora mwenyewe bali kuwa bora kuyajua na kuyatumia madhaifu ya mpinzani wako kumwadhibu.

So punguza presha , mpira una njia zake ,Kumbuka wewe sio Simba ni Yanga so usizuge unaogopa while huogopi lolote.Simba damu tunajua game ijayo utachezwampira mkubwa wala Simba hawezi kufungwa 5 na Yanga in that match

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Wakati huo simba wamefungwa kamba miguuni na manula amefungwa kamba mikononi sio ? POPOMA
 
Nakumbuka pia mwaka juzi uliwahi sema kwa squard hili la
7 Morson
8 bwalya
9 kagere
10 chama
11 miquisonh uto atakula 7, matokeo yake ulijionea uto alisawazisha bao zote mbili ndan ya dakika 10 tu
 
Hakuna shabiki wa Simba anawaza kuendelea kufungana na Yanga siku hizi. Kiu ya shabiki wa Simba sasa ni Kimataifa. Hata ukiuliza msimu ulioisha mechi gani iliwauma na kuwavunja mioyo ni ile ya Orlando kuliko hata ile game ya Final ya FA na Yanga. Kama kufungana tushafungana sana tumepata nn zaidi ya kelele kwenye vijiwe vya kahawa, mitaani tu.
Same as Man Utd au City wanawaza kufanya vyema na kuchukua Ulaya zaidi kuliko kuendelea kufungana tu eti kisa ni derby.
 
Ukifungwa na Orlando hakuna kelele za fukuza matola ila ngoja ufungwe na Yanga hiyo tarehe 23 ndo utajua makolo wanawaza Caf au wanawaza nini!.
 
Back
Top Bottom