Siioni amshamsha ya Forex, vipi watu wameshapigwa?

Sasa humu unafanya nini?
 
Pole sana chief. Tena pole sana na utakufa masikini, n kama unafanya kazi utakufa ukiwa mtumwa wa muhindi. Forex ni real , forex imenifanya nione laki si pesa. Laki ya tz sawa na usd 50 ambayo jumapili usku baada ya soko kufunguliwa naipata ndani ya saa 1. Watu tupo busy na kumake hela. Ipo siku utaelewa na utataka kutrade forex na muda utakuw umeenda. Tumia vizuri simu yako kufanya mambo yenye tija na si umbea tena mtoto wa kiume.


N kama wataka kutrade forex bado hujachelewa. Nenda jangid pale kafanye usajili. Sio kuja hapa na kisimu chako cha tecno , bando la chuo uanze kutusumbua hapa.
 
Hahah,kuna watu wana roho mbaya,et.amsha amsha za matikiti maji,ufugaj wa kware,samaki,uyoga navyo vimepotea,hahahah
 

Attachments

watu wanakula hela zao na hawana mida tena wa kuja jamii forums. wapo busy sana. we endelea na majungu
 
Mkuu mwenyewe nimekuwa bize zaidi ya advance. Hata mpaka wife analalamika simkamui vizuri mana energy Zote zimeenda kwa forex
 
Anajua kuwa atakuwa masikini mwenzake
 
aliyefaidika sana na Forex trade ni Ontario tu na timu yake.. na faida kaipata kwenye training fees na commission ya broker wa forex.. hii ya commission ameipata indirect kwa akili nyingi sana hakuna mwanafunzi wake hata mmoja anaeweza kujua
Vipi kwa aliyefundishwa na akasimama mwenyewe yeye na broker wake,inamaana huyu hatapata faida ikiwa amepata uelewa wa biashara na akajisimamia?

Alichofanya Ontario kuwafahamisha watanzania fursa katika hii biashara ni jambo jema,mafanikio zaidi naamini yatatokana na juhudi binafsi za muhusika.

Watakaoshindwa hawatakosekana naamini,pia watakaofanikiwa watakuwepo na hii itatokana na sababu nyingi tu.
 
Hakuna sehemu nimemwombea na kufurahia MTU kushindwaa!!! Pitia kwenye post yangu upya nazani utaelewa nachokieleza!!!!
Siioni amshaamsha.....

Mkuu hii ina maana gani kama hula lako moyoni?

Hata kama unauliza kwa wema, umeshindwa kutafuta neno zuri badala ya kuweka hilo!

Halafu mkuu wewe umejiunga na hii ID yako September 16, 2017 ambapo ulikuta hii FOREX imeshakamilika kabisa kwa hatua zake na watu wameanza kujifunza, jambo ambalo linaonesha umeamua kuja na hii ID mpya ili uje ulete kejeli juu ya watu wenye nia na FOREX.

Ebu acha wivu mkuu sio jambo zuri!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…