Sijaelewa itifaki ilivyopangwa ziara ya Rais Samia huko Zanzibar

Sijaelewa itifaki ilivyopangwa ziara ya Rais Samia huko Zanzibar

mavumbi

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2013
Posts
596
Reaction score
328
Wanabodi,

Mhe. Samia alifanya ziara huko Zanzibar kwenye eneo la Kizimkazi mahali pa asili yake. Cha ajabu (sijui labda uelewa wa wengine sio ajabu) miongoni mwa viongozi wakuu watatu wa Zanzibar yaani Rais, Makamu 1 na Makamo 2 sikumuona hata mmoja hapo.

Au kwa vile ni kijijini kwake, kwa hiyo? Hapana vyombo vya habari vilitoa coverage ya kutosha kwa hiyo nadhani lilikuwa tukio la kitaifa.

Hii imekaaje?
 
Bro, Mhe Kassim alienda pia na palipendeza kweli kwa jinsi tulivyoona.. hakukuwa na haja ya uongozi wa juu wa Z'bar kuwepo, hata kwa Courtesy tu'..ama kuna jambo nyuma ya pazia?
 
Mambo ya kike yatakusaidia nn ww.umeambiwa alikuwepo first lady w zanzibar. Inatosha
 
Mkuu mavumbi, kwanza asante kwa kutuhabarisha kuhusu hii ziara ya Rais wa JMT kutembelea Kazimkazi mahali alipozaliwa. Sasa hiki ni kijiji muhimu kama Butiama kwa Mara, Chato kwa Geita na sasa Kizimkazi Zanzibar.

Kuna ziara za rais za aina 4.
  1. Ziara rasmi za kiserekali- hii ni ziara rasmi ya Rais kutembelea eneo fulani kama Rais wa JMT, ambapo katika ziara hiyo, viongozi wote wahusika wa eneo husika wanataarufiwa na lazima wawepo na ziara hiyo inatangazwa live.
  2. Mwaliko kwa Rais. Rais anaweza kualikwa kutembelea mahali popote ndani ya JMT kwa ajili ya tukio lolote, hapa wahusika ni viongozi tuu wa eneo husika na sio viongozi wa kitaifa.
  3. Ziara Binafsi ya Rais- Rais wa JMT anaweza kufanya ziara binafsi kutembeleo eneo lolote ndani ya JMT. Wahusika ni viongozi wa eneo husika pekee. Ziara hizo binafsi pia zinahusisha mapumziko, Rais anaweza kufanya ziara ya mapumziko mahali alipozaliwa, wahusika ni viongozi wa eneo husika tuu.
  4. Ziara za Kushtukiza-Rais wa JMT anaweza kufanya ziara ya kushtukiza katika eneo lolote ndani ya JMT, viongozi wa eneo husika tuu ndio watataarifiwa.
Hivyo sio kila Rais wa JMT akija Zanzibar lazima viongozi wa kitaifa wa Zanzibar wawepo.
P
 
Mambo ya kike yatakusaidia nn ww.umeambiwa alikuwepo first lady w zanzibar. Inatosha
Acha mitazamo hasi, hapa tunajifunza masuala wewe kama haikusaidii kaa na unyonge wako! Sio lazima uonyeshe wivu wako
 
Mkuu mavumbi, kwanza asante kwa kutuhabarisha kuhusu hii ziara ya Rais wa JMT kutembelea Kazimkazi mahali alipozaliwa. Sasa hiki ni kijiji muhimu kama Butiama kwa Mara, Chato kwa Geita na sasa Kizimkazi Zanzibar
Thanks kiongozi

Baadhi ya watu wamekuwa na hisia zinazoashiria kutoheshimika kwa President wa JMT kunalkostahili.
 
Back
Top Bottom