Hongera kwa kustaafu mkuu,na mungu akubariki kwa hilo,nami pia namuomba sana Mungu anijarie nistaafu salama.
Back to the topic, hainiingii akilini kwa mtumishi uliyefanya kazi serikalini kwa zaidi ya miaka 30 ukipokea mshahara na huku ukiwa na Uhuru wa kukopa pesa toka mabenki tofauti hadi unastaafu unarudi tena kuanza kukopa badala ya kuanza kula pesa zako bila stress wewe unajipa stress tena,naamini kuna sehemu ulikosea mkuu ndo maaana hadi umri huo bado unakopa badala ya kuanza kupumzika wewe unakuwa tena mtumwa( pole kama nitakuwa nimekukosea heshima)
Na ukute hapo tayari una miaka miwili tu tangu ustaafu lakini tayari umemaliza Millioni 70+ na hazikukutosha ,kama mamilioni ya pensheni hayakumaliza changamoto zako unadhani pesa ya mikopo ndo itamaliza shida za maisha ulizonazo(nisamehe kama nitakuwa nimekukwaza)
Umri wa utumishi ndo umri wa kujijenga,ukstaafu pesa unayopata ni yakula bata huku ukisubiri raia wakuimbie paranda litalia,parapanda x2,sasa wewe eti unasema kuna kitu ulikuwa hujakiweka sawa ndo maana ukamua kukopa ili ukiweke sawa,kukopa kwenyewe umekopa ndani ya miezi miwili unarudi tena kukopa hii inaonesha wewe ni mtu wa aina gani,unapenda starehe,pombe na pengine makahaba,maana hainiingii akili ukope m 10 ndani ya miezi miwili unarudi tena kurenew mkopo wewe utakuwa na changamoto kubwa sana kwenye hicho kichwa chako( nisamehe. Kama nitakukwaza maana kiumri wewe ni sawa na baba yangu ila kimatendo ni sawa na mtoto)
Pambana na hali yako,watu kama ninyi mnamatatizo sana ukiwa kijana unakuwa huna ujuzi wa kuanzisha miradi Leo hii umezeeka unaanza kukopa na kuwa mtaalamu wa miradi mbalimbali,ulishindwa kuanzisha hata genge la kuuza Karanga ukiwa katika umri wa miaka 20+ sasa hivi uko at 60+ utaweza kweli au ni kupoteza pesa tu ?.
Mwisho nakushauri uturie nyumbani ulee familia yako achana na mikopo na miradi yako hewa isiyo na tija,wewe pesa ya pensheni 70M + umemaliza ndani ya miaka miwili,ukakopa 10+M umemaliza ndani ya miezi miwili bado tena unarudi kukopa? Kitu ambacho hujui ni kuwa baada ya kustaafu ni muda muafaka kwa muhusika kusimamia miradi aliyoianzisha ungali katika utumushi na kula matunda yake na sio muda wa kuanzisha miradi hapo utachemka sana.
Nisamehe kama nitakuwa nimekukwaza