Sijajutia kabisa safari yangu ya Morogoro kuangalia maeneo (ardhi) ya uwekezaji

Shida ya vijana wenzatu wakienda kwenye maeneo ya watu wanakuwa na element zilezile za mjini. Wakati ukifika huko Kwa watu kituo Cha kwanza ni kwenye uongozi katika huo uongozi hukoswi wazee kamwe jioni waombe uwatoe hata kama kilabuni au bar au kwenye kijiwe nunua pombe wanywe ama kahawa Hadi wakimbie. Halafu waachie na 5000 Kila mmoja Kazi kwisha. Jambo lolote ukiwafata hata Hela hawakuombi Tena!
 
Aiseeeeh sijui kwa kule maana hata wao kwa wao wanaogopana
 
Ni kweli kabisa heshima aikuondolei chochote katika maisha haya. Wazee wa muhimu kuwaona .
 
Katika Maisha yangu natamani niishi Morogoro Vijijini, kazi ninayotamani ni Kilimo na Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji tu.

Naamini nitatoboa, ni vile mambo bado hayajakaa sawa.

Kwa kifupi umenipa ramani halisi ya Kile natamani
Ukipata hela nenda nunua mapema zaidi maana siku hizi usafiri wa SGR umerahisisha mambo unaenda na kurudi fasta. Kuoshi huko imekuwa rahisi zaidi ukiweka mikakati yako vizuri mzee
 
Mwezi wa 4 nilikuwa pwaga, sikuina fursa nilikuwa na kama 40M nilirudi nazo town
 
umetisha sana mzee, umenikumbuka mwaka 2022 nilifanyanga hii tour nilianziaga mang'ula mpaka ifakara, nilibadili mawazo yangu kabisa kuishi dar nilikutana na utajiri mkubwa sana, nilinunuaga mashamba ya kutosha, eneo la kiegea, nikarudi dar najichangachanga mambo yakiwa safi narudi zangu , term hii tuliani nikajichimbie huko,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…