Oburu alizungumza Alhamisi, Oktoba 15, siku aliyotimiza umri wa miaka 83 na ambayo pia iliadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha mdogo wake, Raila Odinga. Katika ujumbe wake, Oburu aliwashukuru madaktari, wauguzi na wafanyakazi wa The Nairobi Hospital kwa kumhudumia, pamoja na familia yake na wafanyakazi wake kwa kusimama naye katika kipindi hiki cha matibabu.
Kutokuwepo kwa Oburu katika hafla ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha Raila kulizua maswali miongoni mwa wafuasi wa ODM na Wakenya kwa jumla. Oburu alisema madaktari wake wamemshauri apumzike kabisa na kuepuka kuhudhuria mikusanyiko ya hadhara hadi atakapopata nafuu ya kutosha.
Katika ujumbe uliosomwa nakwa niaba yake kwenye hafla ya Bondo, alisema moyo na mawazo yake yalikuwa pamoja na familia na Wakenya waliokusanyika kumuenzi Raila Odinga.
Kisa hiki kinaonyesha jinsi uvumi kuhusu afya ya Viongozi unavyoweza kusambaa kwa kasi, hasa pale wanapokaa muda bila kuonekana hadharani. Ni muhimu kutofautisha taarifa zilizothibitishwa na madai yanayosambazwa bila ushahidi.
Lakini, unadhani ni kwa nini Wakenya hukimbilia kusambaza taarifa za kifo cha mtu kabla ya uthibitisho rasmi? Je, ni tamaa ya kuwa wa kwanza kutoa habari, au mitandao ya kijamii imefanya watu wasichunguze ukweli kabla ya kushiriki taarifa?