Sijamuelewa Bwana mkubwa Kassim

Sijamuelewa Bwana mkubwa Kassim

Kwamba ktk degree yake hakupata ujuzi?,mpaka akaupate VETA?
Vyuoni napo wanatoa ujuzi pamoja na utaalamu ndio maana kuna walimu wanatoa huduma ya tuition na kuna wanasheria wengi wamekuwa mawakili wa kujitegemea kwa hiyo sio wote wahitimu wanatumia ujuzi na elimu yao kuibadirisha kuwa pesa kutokana na kutoona fursa na gharama pia.
So sio vibaya kwa muhitimu kutafuta ujuzi kwa sababu ameona fursa na anataka kuichukuwa kwa ajili ya maendeleo yake binafsi.
 
Anasema wahitimu wenye degree waende VETA ?

Tatizo kubwa la vijana ni ajira hili lipo wazi.

Kwamba kwenda VETA ni muarobaini wa kukabiliana na tatizo la ajira?,halaah sijaelewa

Vijana wote waliopita VETA wana ajira ndicho anachotaka kutuambia?,simuelewi.

Kwamba mimi nina degree ya ETE sona ajira,haya niende VETA nikasome Electronics au CCTV camera installation ndio nitapata ajira au vipi?.

Soma Pia: Waziri Mkuu Majaliwa: Wenye degree kasomeni ufundi VETA mjiajiri

Vipi yeye vijana wake wenye degree amewapeleka VETA na ameona mafanikio hivyo anataka nasi tufuate nyayo? Aaaaw.

Vipi huko VETA watasoma bure ama namna gani vipi?

Yale yalikuwa ni mapendekezo yake binafsi kama Kassim ama kama PM?.
Huyu PM ukimchunguza vizuri utabaini aliwekwa pale na Magu kwasbaba alikuwa dhaifu kichwani tena sio yeye hata Yule mama mkuu wa machawa.
 
Back
Top Bottom