...Kwani hujui siku zote mtoto ni wa mama!!!?Ni jioni, tumepumzika, na mpenzi wangu, mke wangu,katoto ketu ka miaka nane katundu kweli. Basi kanaleta utundu wake, nakafokea, kanazidi, nikakasirika na kukaambia 'we mbona mtudu hivyo, utadhani sio mwanangu?'
duuh, nikawa nimeharibu, wacha mama yake awake, unadhani wa nani. huniamini ee? akaendeleza maneno kibao ya malalamiko, toka juzi amekasirika. Nimemwomba samahani, kakubali, lakini bado kakasirika kwa msemo wangu.
wadau napata mashaka,simwelewi, mbona kakasirika?
Hahahahaha duh ukiona n'tu anajihami basi ujue kuna kitu around basi wewe chunguza n'jomba utabaini ukweli kachukue kapime DNA utabaini pengine kweli sio wako.
Ushawahi kuingia delivery room/leba ukajionea watoto wanavyokuja duniani? Kama umewahi basi nitakushangaa lakini kama hujawahi hebu jaribu kuingia mtakapo-plan kuleta mtoto mwingine,then utapata majibu ya maswali yako yoooote.
Kitanda hakizai haramu ndugu...mkiambiwa wanawake nao wamo, mara ooh ni watu wa staha ona sasa. Kaza moyo kwenda kapime DNA...ndipo utakapopata jibu na roho yako kutulia. Ila uifanye kisirisiri sana. Na ukigundua wewe endelea naye tuu na usimwambie kitu.
...Sui kila siku majibu ya DNA yatakufanya utulie, ukiwa na kimavi yaweza kuwa ni mwanzo wa mwisho wako wewe na my wife wako!! Watch outKitanda hakizai haramu ndugu...mkiambiwa wanawake nao wamo, mara ooh ni watu wa staha ona sasa. Kaza moyo kwenda kapime DNA...ndipo utakapopata jibu na roho yako kutulia. Ila uifanye kisirisiri sana. Na ukigundua wewe endelea naye tuu na usimwambie kitu.
mkuu kweli nukigundua nieendelee, hapo sitaweza, atakufa mtu ati! Fikiria mtoto yupo darasa la pili, namlipia pesa nyingi mpaka nachanganyikiwa, alafu nieendelee nae! itakuwa kazi nzito. . .
Mungu saidia tuu awe wangu
Pole sana calnde nadhani wifi ameghafilika kidogo tu but inategemea na mtu inawezekana kabisa hakuna kitu bali ni reaction yake tu over vitu vinavyomuudhi.
mkuu, DNA itabidi nipime kwa siri au maana kama nimesema vile akawaka DNA si itakuwa balaa? Lazima atanitimua home mkuu
Pole mkulu, ni vijimambo tuu vya maisha hivyo. Utakuwa hujatenda haki kabisa. Maana ingekuwa ni wewe umezaa nje ya ndoa ungemleta mtoto ndani na mama angemlea. Je, kunatofauti gani hapo kama sio ubinafsi. Acheni hizo wanaume nyinyi.
Yeah kweli mkuu nenda kwa siri siri yeye asijue lakini unaweza beba mate tu ya mtoto na kuyapeleka kwa wataalamu wakachunguza na kubaini.
Hebu niambieni wanapimia wapi na vitu gani vinahitajika ili nipate najibu mazuri, ila akijua atantimua home aisee! Mungu wangu . . . .
mwanajamii we ni mwanamama inaelekea,
Nisaidie, anawezekana kweli wife akamind kivile kama hakuna lolote? Halafu always ni mkimya asiyependa makuu wala mabishani au majibizano, hajawahi kukasirika kiasi hicho toka tumeoana miaka zaidi ya nane sasa, ndo maana nikashtuka kwa nini amereact that much. . . .
Hehehe mkuu mahospital makubwa haya duhh mzee kwa hiyo unakaa kwake kama unakaa kwake basi inabidi utii amri mkuu............