Sijamwelewa wife jamani. ..

Sijamwelewa wife jamani. ..

mkuu wakati tunaoana ye alikuwa amemaliza Masters na alikuwa amekusanya senti na kujenga bonge la hausi Njiro Arusha.. . .
Mie nilikuwa na nyumba maeneo ya kijitonyama lakini haikuwa kubwa kama yake. Tukakubaliana kuiuza ili tununue usafiri pamoja na miradi flani ya maendeleo. Mie kwa sasa sina nyumba, ila nilinunua kiwanja Moshono Arusha pamoja na Kingine Kidogo maeneo ya Wazo. .

Tunaishi kwenye nyumba ya wife, japo hajawahi kuninyanyasa wala kuringa. Ananipenda, tunapendana, tunaaminiana, ila hili la juzi limebadilisha kabisa mtizamo wangu kwake!

Hapo mkuu basi huna budi kujishusha kwa kila jambo piga moyo kondo mzee usije ukaibua mambo mengine ikawa ishu home na chakula cha usiku ukawa una nyimwa.
 
Calnde kama unamfahamu vema mkeo basi unayo haki ya kumtilia mashaka kwa reaction yake; mimi wangu alikuwaga na tabia ya kumsema mtoto mara oh hii pua mbona kama si yangu; oh mbona sura kama Mahita yaani ilimradi tu lazima amseme. Mimi nilikuwa naona ni utani tu but kuna siku alifululiza tangu asubuhi akitoa accusations zake nikampa jibu moja tu aende akacheck DNA. Sasa sijui kama alicheck kisiri au la sikumsikiaga tena.

Sasa wewe kama ni mara yako ya kwanza kujoki hivyo na mama amereact hivyo pengine ni kwa vile hajawahi kukusikia ukisema hivyo ndo mana kachukia lakini pia pengine kuna jambo?

Ushauri: Anza kuchunguza sura, maungo na vinasaba onyeshi kuona kama anaresemble na wewe! Ukishaona japo kimoja (hata kama ni rangi ya nywele) unafanana naye ridhika funga file ila na kama hutakiona basi amini mnafanana utumbo au kisogo so songa mbele mambo ya DNA yatakuchanganya bure kaka yangu achana nayo!

Mie sijawahi kabisa kuwaza mambo yakupima. Na ni lazima nikiri nampenda na kumwamini sana! Hilo la kufanana tena unaniongezea shaka, maana toka amezaliwa kila mtu anasema amefanana na mama yake. Hata siku moja sijawahi kumsikia mtuu akisema amefanana na baba yake. . .
 
Hata siku moja sijawahi kumsikia mtuu akisema amefanana na baba yake. . .

Unaniumiza kichwa sasa Calnde mtoto amefanana na nani na Baba au mama? Au mjomba au bibi au babu au binamu hii sura ya mtoto imeenda ukweni au kwenu?
 
Hapo mkuu basi huna budi kujishusha kwa kila jambo piga moyo kondo mzee usije ukaibua mambo mengine ikawa ishu home na chakula cha usiku ukawa una nyimwa.

Dah, kweli mwanaume lazima awe na kwake! Imagine toka hiyo issue itokee hataki hata nimshike, nikipima akigundua si ndo ananisuspend.. .
 
Unaniumiza kichwa sasa Calnde mtoto amefanana na nani na Baba au mama? Au mjomba au bibi au babu au binamu hii sura ya mtoto imeenda ukweni au kwenu?

Baba yake kwa maana ya mimi. Hatufanani, yeye ni mweupe kabisa, mie kidogo maji ya kunde. Ila hilo si tatizo, kimsingi hatufanani, anafanana na mama yake, sura ya wakwe ati. Na haya nimeanza kuyanchunguza baada ya reaction ya wife, kweli ndoa ni kitu cha kutunza, in a minute, mambo yanaweza haribika
 
Mkuu Calnde;

Kua uyaone.

- Nina live examples kama 3 ambazo Wife kazaa haramu ndani ya ndoa na Ama Mume kagundua au Mume Hajagundua lakini maisha yanakwenda kama kawa.

- Kama ukigundua si wako ukamwacha then utakuwa umeachieve nini zaidi ya aibu na fedheha kwako, wife na mtoto na jamaa?

- Afterall who is Mtoto na and why Mtoto? Bill Clinton ni mtoto wa Kambo lakini kachukua jina la baba wa Kambo na mambo yao wote ni Super tu.

- Mtoto ni Mtoto wala si nguo. Mpe mapenzi kama unayo nafasi ya kumpa.

QED!
 
Dah, kweli mwanaume lazima awe na kwake! Imagine toka hiyo issue itokee hataki hata nimshike, nikipima akigundua si ndo ananisuspend.. .

Hapo sasa amevuka mpaka mkalishe chini kiume mlizungumzie na umpe mashaka yako yote kama ulivyoyaleta hapa na akizidi kuja juu mwambie unakwenda kucheck DNA ili kujua ukweli kwa sababu huelewi kinachomkasirisha wakati ushaomba msamaha na isitoshe ulimwambia mtoto katika hali ya kumkataza kufanya utundu si kwamba umemwambia mtu baki! So asilete mashauzi yake
 
pls don tel me that,
miaka nane yote hiyo unataka kuniambia nini
God forbid jamani

Pole sana Mkuu, hukusema kwa nia mbaya lakini kuna maeneo mengine ambayo huyagusi kabisa katika kauli zako ama yanaweza kuleta kasheshe ndani ya nyumba. Sasa umeshakuwa na wasiwasi endelea tu kumuomba msamaha mwenzao maana kauli yako imemuumiza.
 
Naona Calnde hofu yako kubwa ni kwamba unaonyesha hofu flani hivi kwa vile upo kwake lakini sometimes lazima utumie kibase ukiwa kama mwanaume
 
Hapo sasa amevuka mpaka mkalishe chini kiume mlizungumzie na umpe mashaka yako yote kama ulivyoyaleta hapa na akizidi kuja juu mwambie unakwenda kucheck DNA ili kujua ukweli kwa sababu huelewi kinachomkasirisha wakati ushaomba msamaha na isitoshe ulimwambia mtoto katika hali ya kumkataza kufanya utundu si kwamba umemwambia mtu baki! So asilete mashauzi yake

Hapo hata mie nakubali, leo jioni ntakaa nae mpaka kieleweke, kesho asubuhi ntakupa updates, nadhani nisikurupuke kupima DNA kwanza. Ila Ndoa ni kitu kingine kabisa, kwa mapenzi yetu sikuwa kutegemea kama ndoa inaweza kuwa na hard moments kiasi hiki. . .
 
Pole sana Mkuu, hukusema kwa nia mbaya lakini kuna maeneo mengine ambayo huyagusi kabisa katika kauli zako ama yanaweza kuleta kasheshe ndani ya nyumba. Sasa umeshakuwa na wasiwasi endelea tu kumuomba msamaha mwenzao maana kauli yako imemuumiza.

Msamaha nshaomba sana mkuu, ila leo tena ntakaa nae, kwa busara na upendo, ntaona reaction yake, nadhani tutayamaliza tuu....
 
kuna vitu mtu unaropoka lakini vinaku cost,sasa wewe utamwambiaje mtoto hivyo? .....haipendezi! nadhani huyu mama atakuwa amechukia ulivyomsemelea mwanae hivyo, na kutofanana na mtoto ndio kusababishe ufikirie yote hayo kwasasa, kama mtoto kafanana na mamake shida ipo wapi, mhhh na ukienda huko kwenye DNA akijua bi mkubwa ndio hamtaelewana kabisa na likizo atakupa, bora umshirikishe tu na cjui utamuanzaje.
 
aliumia tu ulivyosema "katoto katundu utadhani si kako " hata mie ningejisikia vibaya
 
Naona Calnde hofu yako kubwa ni kwamba unaonyesha hofu flani hivi kwa vile upo kwake lakini sometimes lazima utumie kibase ukiwa kama mwanaume

Ni kweli mkuu, ila mie mkristo, yanipasa nitunze ndoa. Nikimpoteza huyu ndo siwezi oa tena mpaka afe . . ..
Ndoa tamu bwana, ,
 
Calnde kama unamfahamu vema mkeo basi unayo haki ya kumtilia mashaka kwa reaction yake; mimi wangu alikuwaga na tabia ya kumsema mtoto mara oh hii pua mbona kama si yangu; oh mbona sura kama Mahita yaani ilimradi tu lazima amseme. Mimi nilikuwa naona ni utani tu but kuna siku alifululiza tangu asubuhi akitoa accusations zake nikampa jibu moja tu aende akacheck DNA. Sasa sijui kama alicheck kisiri au la sikumsikiaga tena.

Sasa wewe kama ni mara yako ya kwanza kujoki hivyo na mama amereact hivyo pengine ni kwa vile hajawahi kukusikia ukisema hivyo ndo mana kachukia lakini pia pengine kuna jambo?

Ushauri: Anza kuchunguza sura, maungo na vinasaba onyeshi kuona kama anaresemble na wewe! Ukishaona japo kimoja (hata kama ni rangi ya nywele) unafanana naye ridhika funga file ila na kama hutakiona basi amini mnafanana utumbo au kisogo so songa mbele mambo ya DNA yatakuchanganya bure kaka yangu achana nayo!

huyu shem wangu nae alikuwa anataka afanane na mtoto mpaka ulimi? kama alienda kumpima kimya kimya bila kukushirikisha cku ukijua/hakikisha utalichukuliaje?...
 
watu wengine hasa mnapenda kujikosesha raha! mtu useme kuwa "kakaa kaa si wko" kisha unaanza kujifanya hujui kakasirikia nini.

mkeo anasafura kw kuendelea kununa kwa siku nyingi, lakini kuhamaki kwa hapo kwa hapo ipo hasa kama ulitamka neno hilo zaidi ya mara moja mbele ya mtoto ambae mkubwa tena anafahamu
 
huyu shem wangu nae alikuwa anataka afanane na mtoto mpaka ulimi? kama alienda kumpima kimya kimya bila kukushirikisha cku ukijua/hakikisha utalichukuliaje?...

nyamayao hata sijui nitakachofanya but sidhani kama ningeichukulia a big deal juu ya hilo. Ndio nitaelewa kuwa hakuwa ananiamini but kwa upande mwingine nitashukuru kwa vile atakuwa amejiona ujinga wake na pengine trust itarudi. Hakuna kitu kibaya kama kuishi na mwenza asiyekuamini kwani utakuwa unafanya yote na bado hakuamini. Ndio maana mimi nilimwambiaga kama haniamini atafute private investigator ampe hiyo kazi. Wanakera hawa dada yangu we acha tu
 
Hapo sasa amevuka mpaka mkalishe chini kiume mlizungumzie na umpe mashaka yako yote kama ulivyoyaleta hapa na akizidi kuja juu mwambie unakwenda kucheck DNA ili kujua ukweli kwa sababu huelewi kinachomkasirisha wakati ushaomba msamaha na isitoshe ulimwambia mtoto katika hali ya kumkataza kufanya utundu si kwamba umemwambia mtu baki! So asilete mashauzi yake

Eh...Umekuwa mkaaaali heheheee

mimi hata sijui nisemeje hapa lakini jambo moja tu kuwa na IMANI ni kitu kizuri sana. The moment unapoteza imani dhidi ya mtoto/mke wako kila kitu utakishuku na hapo mambo yataanza kuharibika. Kuaminiana ni msingi mkubwa sana wa kudumisha ndoa.

Si kuna kale kautafiti kalikofanyika kakaonyesha kuwa katika watu waliokwenda kucheki DNA bongo, 6/10 walikuta wana watoto SIO wao!
 
Ni jioni, tumepumzika, na mpenzi wangu, mke wangu,katoto ketu ka miaka nane katundu kweli. Basi kanaleta utundu wake, nakafokea, kanazidi, nikakasirika na kukaambia 'we mbona mtudu hivyo, utadhani sio mwanangu?'

duuh, nikawa nimeharibu, wacha mama yake awake, unadhani wa nani. huniamini ee? akaendeleza maneno kibao ya malalamiko, toka juzi amekasirika. Nimemwomba samahani, kakubali, lakini bado kakasirika kwa msemo wangu.

wadau napata mashaka,simwelewi, mbona kakasirika?
Lakini na kina baba muwe mnachagua maneno ya kuwambia watoto. hivi unavyomwambia mtoto utadhani we si mwanangu una maana gani, that is a kid for god's sake, why would you use such language in front of the kid?
 
Umenena Carmel mtu unapaswa kuwa mwangalifu sana katika kauli unazotoa,hata ingekua ni mimi ningekasirika maneno gani hayo ya kumwambia mtoto.
 
Back
Top Bottom