Sijaona sababu za msingi kwanini Serikali haitaki kutoa takwimu za idadi ya wafuasi wa dini

Kuna dini zinazaa kama free fall Kuu. Kwa hiyo hizo projections zinaweza kutokuwa sahihi ukizingatia mambo kadhaa kama birth rates katika dini tofauti ambazo zimebadilika toka enzi za mkoloni kutokana na shule nk.

Mazee nilichokuambia tafuta data
Sasa unajibu Kama hizo data ushaziona na hujazikubali...
Tafuta data kwanza
 
Serikali iligoma kwasababu tangu nchi ipate uhuru haikuwahi kuhesabu makabila wala dini waliona ingekuwa jambo jipya, mara ya mwisho watu walihesabiwa dini na makabila ilikuwa kipindi cha ukoloni kabla ya uhuru
Kiongozi mjinga tu ndio atatumia hicho kama kisingizio. Hatuendeshwi na mambo yaliyofanywa au kutofanywa na wakoloni
 
Shida yako ni kujua tu dini ipi ina wafuasi wengi????
Eleza faida za kufanya hivyo..
 
Point nzuri sana. Kutoa matokeo ya sensa na kusema tuko milioni 61, wanaume milioni 30, wanawake milioni 31, mie nimeona ni ujinga na kukosa busara...
exactly ingesaidia mambo mengi si ajira tu...hata projection za masomo na kibajeti kwa shule za msingi, secondary, vyuo na mikopo kama ya HESLB, huduma kama za bima. Kuishia kusema tu idadi ya watu kwa ujumla wake haileti maana kabisa maana hata NBS walisha kadiria kuwa tuko 61.3. Sense inapaswa iainisha umri wa watu kimakundi
 
Shida yako ni kujua tu dini ipi ina wafuasi wengi????
Eleza faida za kufanya hivyo..
Kwani ukiambiwa Tanzania kuwa wanawake milioni 31 wanaume milioni 30 inakufaidishaje?
 
Nimekuuliza ulitakiwa unijibu..
Serikali inahesabu watu kwa ujumla kwa maendeleo ya taifa bila kutumia vipengele ulivyotaja wewe.
 
Nimekuuliza ulitakiwa unijibu..
Serikali inahesabu watu kwa ujumla kwa maendeleo ya taifa bila kutumia vipengele ulivyotaja wewe.
Basi kujua idadi ya Wakrsto n Waislamu watajua ni maeneo gani yatengewe maeneo mengi kwa ajili ya msikiti na makanisa nk, wapi kuna wapagani wengi hawahitaji land planning kwa ajili ya makanisa na misikiti nk
 

Kwani ukiambiwa Tanzania kuwa wanawake milioni 31 wanaume milioni 30 inakufaidishaje?
Kasome ripoti ya sensa sio kuongea tu, ulitaka asome ripoti nzima. Lazima sensa ioneshe hayo unayosema. Soma ripoti nzima halafu ulete hoja zako najua hujaisoma. Watanzania ndo tulivyo hata huna uhakika unapiga. Lazima utofauti wa umri unaleta majibu ya watoto, vijana, watu wazima, nguvu kazi, utengemezi na uzalianaji na mengine.
 
Ukitaka hizo idadi za waumini nendeni kwenye makanisa na misikiti yenu muhesabiane nadhani mtapata idadi yenu vivyo hivyo idadi za watu kikabila itaneni kupitia kooz zenu mihesabiane wala hakuna shida.

#MaendeleoHayanaChama
 
unataka kutambika?
wewe elewa tu kwamba mwamosa ana NYOMI KWA SASA
 
Ila nahisi Waislamu wakiambiwa ni wachache kuliko Wakristo hawatakubali hizo takwimu, wanaamini mno kwamba wao ni wengi, kwa kuwa wao ni wengi Dar.
unaonaje kama hii observation ungeiweka kwenye main post?
 
Wakatoliki tulifanya sensa yetu kwa Jimbo nilipo mimi mwaka huu mwezi wa sita.

Na hili nadhani ni jambo la kundi husika,by the way hilo swali wewe uliulizwa kwenye maswali ya sensa?
 
Kipengere cha dini hakikuwa sehemu ya sensa... Na serikali haipangi mipango kwa kuangalia imani za watu.. Hata Mungu mwenyezi mwenyewe, hanyeshi mvua kwa waumini peke yake.. Sasa kwanini uitake serikali kufanya jambo ambalo hata Mungu mwenyewe hawezi kubagua watu wake ?? Mwl alijibu vizuri sana, kama wanataka wafanye wenyewe sensa zao.. Hata hivyo imani za dini zinaweza kutumia takwimu hizi kuona wapi waeneze imani zao..
 
Wakatoliki tulifanya sensa yetu kwa Jimbo nilipo mimi mwaka huu mwezi wa sita.

Na hili nadhani ni jambo la kundi husika,by the way hilo swali wewe uliulizwa kwenye maswali ya sensa?
Hawakuuliza maswali hayo Mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…