Sijaona sababu za msingi kwanini Serikali haitaki kutoa takwimu za idadi ya wafuasi wa dini

Sikutaka asome ripoti nzima, nilitaka aweke dondoo zaidi sio kutoa taarifa kwa dakika kumi tu kwenye tukio kubwa kama hili
 
Aliyekwambia hii nchi inaegemea Dini ni Nani wee jamaa nonsense ,mpuuz
 
Kazi ya kuhesabu waumini si ya Serikali. Kwanza kumbuka Serikali haina Dini. Kama unataka kufanya Sensa ya kidini waambie viongozi wako wa dini waandae budget na utaratibu wa kuwahesabu.
 
Mtoa mada bila kusahau
Simba sc
Young africans
Azam
Coastal union
Mtibwa sugar
Mbeya city
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Yale ni matokeo ya awali tu. Ripoti kamili bado.
 
Wenye dini zao ndo wafanye sensa ya waumini wao, serikali haina Dini wala ukabila,
 
Kwanza unaelewa dhumuni la serikali kufanya hiyo sensa ya watu na makazi?
Tuanzie hapo.
 
Kiongozi mjinga tu ndio atatumia hicho kama kisingizio. Hatuendeshwi na mambo yaliyofanywa au kutofanywa na wakoloni
Kwahiyo nyerere mjinga? Maana ndio alitoa kuhesabu kabila na dini za watu kwenye sensa
 
Hata wanawake na wanaume wangeainisha na umri. Maana ninaamini wanawake wanaosemwa wengi ni wale ambao siyo umri wa kuolewa au kuzaa(vizaa vya over 45yrs) na visichana under 18.

Hata wanaume pia wangeainisha umri in groups
Hayo maswali yote yaliulizwa kwenyr sensa
 
Issue za dini zinagusaga hisia za watu na watu huwa wanaongelea issue za dini Kwa mihemko sana so it's better ziachwe tu
 
Wakatoliki wanaijua idadi ya waumini wao kuanzia ngazi ya jumuiya, kigango, parokia, jimbo mpaka kitaifa. Na imeenda mpaka world wide. Very smart and intelligency.

Dini na madhehebu mengine mnakwama wapi? Hata nyerere alisema dini inayotaka kujua idadi ya waumini wake iwahesabu kwenye nyumba zao za ibada. Shida ikwapi?
 
Takwimu hizo zitaisaidia vipi serikali kwenye mipango yake?
 
Na faida yake Ni Nini?
 
Bila kusoma huo utopolo kwa kuzingatia heading yako! " Nchi yetu hazingatii huo ujinga na hautusaidii chochote pia sio nchi ya dini wala kabila hizo takwimu kila mtu akaziulizie kwenye dini yake au kabila lake " au nenda randwa na kenya naona bado wana element hizo za udini na ukabila

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kama hujui Waislamu ndio tulikuwa tunataka hiyo idadi, serikali ndio ikagoma

Makabila yote makubwa ni Christian majority.
1. Sukuma
2. Haya
3. Chagga
4. Nyakyusa
5. Maasai
 
Makabila yote makubwa ni Christian majority.
1. Sukuma
2. Haya
3. Chagga
4. Nyakyusa
5. Maasai
Masai kabila kubwa kijina na umaarufu sio kinamba

Halafu Tanzania hii hakuna kabila linalofikia zaidi ya asilimia 10 ya Tanzania, aka hakuna hata kabila moja ambalo hata ulikusanye unaweza pata idadi ya watu wa kuweza kufikia hata idadi ya watu waliopo Dar, aka hakuna kabila lenye watu zaidi ya milioni kumi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…