Sijaona Tatizo kwenye wimbo wa Diamond wa Hallelujah

Basata wanatakiwa watoe muziki mmoja pamoja na video, uwe mfano katika mashairi na mavazi.. Ili iwe mwongozo vinginevyo watauwa sanaa ya Muziki nchini
Nimecheka sana mkuu
 
Kwetu Mke tunaita Nke, Mtoto tunaita Ntoto so usishangae kwa matumizi ya R na L kwetu ni mtihani. Sorry kama kwa usumbufu.
Hataki sisi Z tunaitmka S [emoji13] [emoji12] go ahead sir [emoji120]
 
Mkuu, Serikali imeshaamua. Kama unampenda Domondi, mtafute mkanywe chai. Halafu, hili jambo linakuwaje la kisiasa hadi liwe hapa?


JUKWAA LA SIASA
Tanzania's Political Forum. Tafadhali hakikisha hoja unayoiweka hapa ni ya kisiasa kweli!
Kwa sababu maamuzi ni ya kisiasa zaidi.
 
Poleni sana Roma Mkatoliki na Nay wa Mitego, wengine subirini tu kdg mtafunguliwa hakuna shida kubwa kwenu.
 
Hiyo ni strategy tu ya kutuhamisha kutoka kwenye mjadala wa usalama wa raia na mabadiliko ya katiba inayoendana na nyakati za sasa. Na watanzania wengi tuna tatizo la ADHD (Mental issue) hua tunashindwa ku focus kwny suala moja. So its a political strategy, ila kufunika issue ya mauaji ya raia, ukiukwaji wa haki mengineyo mengi ambayo raia haturidhishwi nayo.
 
Suala hili sio la leo sema Basata kwa kipindi kirefu lilikuwa limelala. kipindi cha nyuma kabla ya kurekodi wimbo ulikwa unatakiwa kwanza upeleke mashairi ya wimbo, kukiwa na maneno ambayo lugha yake ni tata au katika jamii maneno hayo hayafai ulikuwa unaambiwa urekebishe. Pale RTD enzi hizo kulikuwepo na watu wa kuyapitia mashairi ya nyimbo zenu kabla ya kurekodi baada ya kufanya hivyo ndipo mnaweza rekodi nyimbo zenu. Hii ilikuwa mpaka kwenye sinema, ukileta sinema unaipeleka pale audio visual inaangaliwa sehemu zisizofaa zinaondolewa ndipo unaruhusiwa kuionyesha.

Tatizo lililopo kwa wasanii wa sasa, ni kwamba wanapenda maneno magumu kusikilizika, halafu na studio zipo nyingi wala hazina haja kutaka kujua umesema nini katika wimbo wako na unaonyesha nini katika video yako. Tunasikilizishwa maneno maguma ambayo mengine huwezi kusikiliza mbele ya familia na wala huwezi tazama video na watoto au baba yako na mama yako. Ifike mahali studio zote zisajiliwe na zipewe mwongozo wa mamna ya kufanikisha kazi za wasanii. Na vituo vyetu vya redio na televisheni navyo viangalie kazi za kurusha.

Niwashukuru Basata kwa kuliona hilo maana tulikokuwa tunaelekea kulikuwa kubaya na maadamu wamesema huo ni mwanzo na hizo zilizofungiwa ndizo walizoanza nazo na zingine zinafuata. tufike mahali tujue kulinda vinavyopaswa kulindwa. Muziki upo tangu zamani lakini hatukuwahi kuimba kuvuka mipaka kufikia kiasi ambacho wanamuziki wa kizazi kipya wamefukia. Nawapongeza sana Wizara husika, Basata TRA na wale wote wanaounga mkono jambo hili.
 
Alafu wameshapatikana, then kinachofiatia kwa Hallelujah ni nini????
Katika Abam anayokwenda kuizindua na huu wimbo upo, itakuaje sasa????
Na atakuwapo huyo seduce me akikata mauno kuicheza vilivyo Hallelujah!
 
BASATA ni mambumbu tu kama yule Bichwa Treni.
 
Mf kama chura ya Snura,aliimba ktk kampeni za CCM karibia Tanzania nzima ,ina maana BASATA hawakuiona au walitaka waheshimiwa waburudukike kwanza na MSAMBWANDA wa Snura,alafu ndio waifunge na kuhusu Haleluya daimond na Juu ya JUX mbona mimi naziona hazina tatizo.Ndio tatizo ya vitengo vya vijana kuwapa wazee,lkn hata huko nyuma kuna nyimbo zenye ukakasi na bado zinapigwa mfano mkunaji na mkunwa ,muhogo wa jang'ombe hizi zote ni matusi ,ila sijajua labda wana deal na matoleo mapya ya matusi na si yale matoleo ya zamani kwani yamepitwa na wakati.
 
wangeifungia waka waka aliyomshirikisha rick rossi
maana ile ndio misambwanda wazi wazi kaa kokoro ya rich mavoko.....
 
Nyimbo zote za Diamond shida ni kwenye video sema tuu Basata hawakuwa clear
 
Ungeweka sababu za kufunguwa hapa ili tujue kama unazifahamu then uje na critics zako genuine and logical ili yupime sasa kama una hoja au ni mkurupukaji tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…