Mkuu, kwa mawazo yako upo sawa kabisa.. Ila muziki ni zaidi ya hiari kuusikiliza ama kuangalia mtu halazimishwi, ndo maana kuna channels za vitu tofauti tofauti mfano:- movies, makala, Dini pamoja na burudani (muziki) na vingine vingi.. Ukiuangalia muziki, kwa upeo finyu kabisa unaweza mfungia yoyote unayetaka kwa sababu zako ila ukiangalia muziki kwa jicho pevu utaona ni jinsi gani hii ni Idara nyeti sawa na viwanda, dhamira kubwa ya viwanda mbali ya uzalishaji ni upatikanaji wa ajira za kutosha.. Muziki umeajili vijana wengi sana katika nyanja tofauti tofauti, kama waimbaji, watengenezaji wa huo muziki, wasambazaji, wachezaji, makampuni ya entertainment kwa uchache wao. Ivo badala ya kumuua msanii basi serikali inatakiwa kutengeneza mazingira mazuri inufaike nao, kwenye kodi na kusaidia kutoa ajira. Kumfungia msanii haisaidii kabisa, kuwa na mpango mzuri, sawa wimbo hauna maadili kwenye video yake, ruhusu ipigwe kwenye radio lakin si kwenye TV, weka kwenye internet sababu tunaamini wanapofika YouTube na kwingineko ni watu wazima.. Tuwe na mipango ya kujenga na si kubomoa.