Sijaona umuhimu wa sekretarieti ya ajira kurudia majina ya waliopata kazi katika matangazo mapya ya kazi

Rais mwema kwakooooo😬😬😬kuna vitu vingine siyo mpk ukomenti, ufagio kafagilie hukooooo chattle🤔🤔 dadadeq
 
Rais mwema kwakooooo😬😬😬kuna vitu vingine siyo mpk ukomenti, ufagio kafagilie hukooooo chattle🤔🤔 dadadeq
Kama wewe ulikua ni mpiga dili lazima utaumia sana maana mianya ya wapiga dili imeziba kabisa
 
Kusubiri ajira utawala huu wa magufuli ni sawa na kusubiri bikra wodi ya wazazi,ni kujiongeza tu utawala wa magufuli ajira sio kipaumbele ila road na uongo uongo ndo vipaumbele
 
Kusubiri ajira utawala huu wa magufuli ni sawa na kusubiri bikra wodi ya wazazi,ni kujiongeza tu utawala wa magufuli ajira sio kipaumbele ila road na uongo uongo ndo vipaumbele
Tunaongozwa na waziri wa ujenzi, rais kastaafu😆😆😆
 
Inasikitisha sana, hizo kanzidata zinaficha mengi sana na nimekuja gundua kanzi data ndio " loop hole " ya kuchomeka watu katika taasisi mbalimbali

Kusema ukweli hata me niliwah kuhis hivyo , japokuwa nlipata kazi kupitia secretariet hiyo hiyo ila nadhani ilikuwa bahati tu na hakukua na namna sababu kuna nafasi kwene organization zingine kuu za serikali mitihani yote niliiiipasua hata kwa zile tulizobaki watu watatu na wanataka watu wawili tuliwah kukosa wote sababu tulibadilishana namba na tukapeana ukweli...mfano kulikuwa na interview za e-Government, mpaka leo sijaona watu wakiitwa au majina yakiwekwa kwa website ya serikali, mtu wangu wa ndani kaniambia wanapigia watu simu kimya kimya, nimechoka ila nawaombea wakuu mpate kazi tusaidiane kujenga hii nchi daaah sio poa mambo wanayofanya kama kweli yanafanyika
 
Huwa nawashangaa sana mnapotetea ujinga katika maswala ambayo yako wazi kabisa! Ni kichaa cha hali ya juu mno
 
Mkuu taasisi nyingi kubwa huwa kuna ndugu wengi wa wakubwa wanazugishwa katika saili ila mwisho wa siku huwa wana maswali yote ya written na oral na mwisho wa siku ndio hupata nafasi.

Ajira nyingi za halimashauri hupewa watoto wa maskini.

Kama field kupata tu Tanroads ni shida sembuse ajira
 
Na kwanini baadhi ya ajira zinachelewa sana kutoka kwenye oral mpaka kuitwa kazini. Yaani mpaka mtu unasahau kama umefanya interview
 
Mkuu nakuomba pm kuna issue nataka kukuuliza
 
Hatimae wameomba msamaha kuna makosa yametendeka, hakika jamii forum ni sehemu sahihi ya kupaza sauti wamedai Tangazo jipya litatolewa tarehe 28 likiwa na majina mengine 90.

Kwa maana hiyo inaonesha wazi kuwa hawa jamaa kuna nafasi nyingine walikuwa wameziweka " pending"

Taarifa yao kamili kutoka katika tovouti yao ni kama ifuatavyo;

UFAFANUZI WA TANGAZO LA KUITWA KAZINI LA TAREHE 25 JANUARI, 2021​



Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuomba radhi kwa makosa yaliyofanyika katika tangazo la kuitwa kazini lililotoka tarehe 25 Januari, 2021 lenye Kumb. Na. EA.7/96/01/L/22 la MDA’s na LGA’s kuwa baadhi ya majina ya wasailiwa na sehemu waliko pangiwa kituo cha kazi zilitolewa kimakosa.

Hivyo, Watumishi walioonekana kuitwa kazini kwa mara ya pili katika ofisi hizo hizo ilihali wamekwisha ripoti katika taasisi zifuatazo:- Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Hospitali ya Rufaa ya Bugando (BMC), Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC), Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (IAE), Hospitali ya Kikristo Kilimanjaro (KCMC), na Halmashauri ya Wilaya ya Katavi, tunaomba waendelee na majukumu yao kama kawaida katika ofisi husika.

Aidha, ofisi ambazo Wasailiwa wake wameitwa kazini hivi sasa ni hizi zifuatazo:-

  1. Wizara ya Mifugo na Uvuvi,
  2. Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea,
  3. Halmashauri ya Wilaya ya Igunga,
  4. Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga,
  5. Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua,
  6. Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo,
  7. Halmashauri ya Wilaya ya Manspaa ya Musoma,
  8. Halmashauri ya Wilaya ya Njombe,
  9. Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba,
  10. Shirika la Madini la Taifa (STAMICO),
  11. Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI),
  12. Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE),
  13. Chuo Kikuu Mzumbe – MU,
  14. Chuo Kikuu cha Dodoma – UDOM,
  15. Chuo Kikuu Ardhi – ARU,
  16. Chuo cha Taifa cha Usafirishaji – NIT,
  17. Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama Shinyanga – KASHWASA,
  18. Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Musoma – MUWASA,
  19. Mamlaka ya Elimu na Mafunzo – VETA,
  20. Mahakama ya Rufaa Tanzania,
  21. Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya – NHIF,
  22. Baraza la Taifa la Ujenzi - NCC
  23. Shirika la Umeme Tanzania, Kanda ya Mtwara,
Hivyo, tunapenda kuwaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaokuwa umejitokeza kutokana na makosa yaliyofanyika katika tangazo hilo. Kwahiyo, tangazo sahihi la kuitwa kazini mwezi Januari ni lililotoka upya tarehe 26 Januari, 2021 lenye jumla ya majina tisini (90), lenye Kumb. Na. EA.7/96/01/L/24.

Imetolewa na;

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Sekretarieti ya Ajira.

26 Januari,2021.
 

na maana yake nyingine ni kuwa inawezakuwa kuna uhuni huwa wanafanya aisee sio wakamilifu 100%
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…