Sijapata kuona wanafiki kama Watz, haya huyu muingine (aliyekua timu misifa) aibuka na kuponda mradi wa ufuaji umeme wa Stiegler

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Mojawapo wa vitu nilivyoshuhudia sana kwa Watanzania, huwa wana unafiki uliopitiliza, yaani jamaa huongea kistaarabu na wanaweza wakakakusifia mpaka ufurahi sana ila subiri uondoke, utasemwa mpaka basi. Watakuita mkuu, wataongea na wewe kwa furaha mpaka uone kama vile uko bingu nyingine, watakupa shikamoo kwa furaha nyingi tu, ila majungu na machungu waliyosheheni kwa ajili yako, dah!
Na ndio tofauti kubwa na Wakenya, maana hapa Kenya huwa unaambiwa kama ilivyo, ukizingua unaambiwa, umeze uteme utajijua mwenyewe ila kama uko uchi utaambiwa tu.

Marehemu rais Magufuli aliogelea kwenye sifa za Watz, waliimba mapambio yake tu, kila siku walimfanya ajione kama mtume fulani hivi, hakuna aliyediriki kusema vinginevyo, labda yule Lissu aliyeondolewa kwa marisasi.
Sasa leo hayupo tena hao hao waliomlamba miguu wameibuka na kuanza kuponda kila alichokifanya, kumbe walikua wanaumia kimya kimya wote. Kuna spika tena mwandani wa karibu sana wa marehemu juzi ameomba michakato ya ujenzi wa bandari ya Bagamoyo izinduliwe, kuna huyu mwingine naye ameponda mradi wa ufuaji umeme, ule wa Stiegler, na watatendelea kuongea wengi sana, kwanza sasa hivi wanajadili upigaji uliovumbuliwa na ukaguzi wa CAG, upigaji ambo haujaonekana tena kwao huko, yaani kipindi chote cha JPM jamaa wamepiga hela ufisadi wa kupitiliza.....kha hawa bana.

 
Watanzania ni watu wanafiki na waoga
sana. Mbona wanangoja mtu afariki ili waanze kumponda? Kama wao ni wanaume kamili nilitegemea wangemponda akiwa bado yupo hai. Mbona huku Wakenya wanamponda Uhuru kwa sababu ya madeni mengi anayochukua kila siku na wala hatufichi mapungufu yaliyo huku? Hawa watu wapunguze uoga na unafiki. Ponda mtu akiwa bado yupo hai ili ajuwe mapungufu yake.
 

Halafu kitu cha hovyoo zaidi ni yaani hao wanaomponda marehemu leo hii, muda akiwa hai usingewaambia kitu, walikua wanamsifia tena kwa mapovu, yaani ungedhani wapo radhi kufa kwa ajili yake, ndio unafiki uliokubuhu. Kha! Magufuli kama akiwa huko ana uwezo wa kuangalia duniani aone yanayotendeka.....hehehe
 
Tony kila Mara ninatumia neno kwamba wakenya hamna akili na uwezo wenu wa kufikiria ni mdogo, japo ninajua sio vizuri kutumia msemo huu, lakini ninalazimika kutumia kutokana na ujinga wenu

1)Huyo Prof. Muhongo hajapinga wala kuponda mradi wa uzalishaji umeme unaoendelea, huyo aliyefungua huu uzi unamjua vizuri kichwa chake, hupaswi kumsikiliza bila kujiridhisha, huyo ni mkikuyu "hard liner".

Alichosema ni kwamba, katika miradi yenye kurudisha pesa haraka, umeme wa kuzalisha kwa maji, haumo kawaida unachukua muda mrefu kurudisha pesa, Kama tunataka kufikia per capital ya $2500 by 2025 tunahitaji kuongeza bidhaa mpya zenye kutoa faida haraka.

Kwamba wakenya hawajikombi kwa viongozi, mumesahau Sonko alivyokua akimsifia Uhuru Kenyatta wakati alivyokua Governor wa Nairobi?, alivyoondolewa kazini umesikia aliyosema kuhusu ufisadi wa Uhuru Kenyatta na familia ya Kenyatta, kwanini asingelisema alipokua Governor.

Rutto sasa hivi anailaumu serikali kwa kukopa, wakati yeye ni Naibu rais, kabla ya ndoa yake na Uhuru kuvunjika alikua akitetea kila jambo lililifanywa na serikali.
 
Wakuu,,, hii imekaaje, kama si unafik ni nini???
mkorinto, passioner255, lwiva, Mwanzi1, babayao255, luangalila, Naby Keita tuusan, Darmian
»»»
KATIKATI YA MAJONZI:
Ndiyo Nagutuka kuwa Tuliyempoteza ni Shujaa Aliyepitwa na Wakati!
Anaandika Peter Simon Msigwa
 
Ila Prof Muhongo mnamuonea tu. Aliamua kukaa kimya tu ila hakuwahi kutoa pambio saana wala kusupport huo mradi.
 
13 May 2019
Tazama maelezo na mapendekezo ya Spika wa Bunge kuhusu uamuzi wa Serikali kusitisha mradi wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo


Spika Ndugai Aishangaa Serikali Kusitisha Mradi wa Bandari Bagamoyo

 
13 May 2019
Tazama maelezo na mapendekezo ya Spika wa Bunge kuhusu uamuzi wa Serikali kusitisha mradi wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo


Spika Ndugai Aishangaa Serikali Kusitisha Mradi wa Bandari Bagamoyo


Wow! Sasa ilitokeaje akaufyata, na ndio hicho yule CAG wa kitambo anasema wote hao ni wasaka tonge, wanasklizia upepo unakovuma......
 
 
Wengi wao walikuwa hawamkubali Jiwe sasa ile alikuwa katili libidi waigize Ili maisha twende ndio maana saizi wanafunguka

Jiwe mwenyew alikuwa jizi huku likijifanya kupigania wanyonge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…