Nyumba niliyonayo ni ya urithi, nilipewa ikiwa imemalizika vitu vingi, nilihamia tu ?
Nami nataka nijenge nyumba ambayo pengine naweza pia kuirithisha huko mbele.
Sina ujuzi wala uzoefu wowote wa kujenga.
Kwenye usimamizi kitu pekee nachoweza labda ni ulinzi wa vifaa na kuhakikisha mafundi hawapigi story muda wa kazi ila kuhusu kukagua mambo ya ujenzi sina elimu yake
Je nisimamie kienyeji bila kuwa na elimu yake kama wengi wanavyofanya au nitafute mtaalam ?
Kwanza nimesoma baadhi ya comment umesema upo mkoa wa mbeya huko kidogo ujenzi ni rahisi…
Kwanza inabid ufahamu kuwa ujenzi sio garama kubwa gharama zinaletwa na ww kwa kuruhusu wizi na usimamiz hafifi
Ukisema utafte mtaalam ( alisoma ana vidigirii na vi dploma kaofisi kidogo na ka mkataba). Sio mbaya na utajengewa nyumba kali san nzur na ila tatizo gharama zao huwa kubwa maana ye anakuwa mtu kati kati yako ww na local fungi yaani yule anaeenda kujenga sasa au kupauwa wew utamwajil na yy ataajili
Na hapa inabidi agharau uwe umeshajenga hata nyumba mbili tatu unajua uwe unajua idadi kamili ya material la sivyo utapigwa sana yaani nyumba ya kujengea seruji (cement) 100 utaandikia 150 mpaka 300… hapo uwe makin sana
Na hao walosoma tunao mtaan huku ss ndo tunawaelekeza ..mfano inatakiwa esabu ya kuezeka atamuita fundi ampe esabu alafu ndo nae aje akupe ww kiufupi hawana uzoefu
Wapo waliiva na n wanauzoefu mkubwa ila gharama zao kubwa sana tuchanane nao
Wapili N fundi wa kaiwaida labda elim yake ni pa nne tu hapo utakuwa na aina mbili umpe yy kazi akusimamie au
Ummpe mfano ajenge,baadae utafte wa kupauwa, baadae wa plaster na hii ndo wengi wanajengaa
Hapa mm nikushauri fundi wa kwanza wa nyumba yako n wewe mwenyew na usimamiz wako ww sio kwenye ujenzi ni material yako usipigwe, mtu akijenga utaona ty hapa fundi yupo au hamna..
Huyu fundi yupo kwa rafiki zako na waty wako wa karibu hata tu ukipita ukiona nyumba imejengwa kali omba namba ushampata
Mm nakwambia haya n fundi galagala 4m 2 B huko tunapedwa kuitwa local fundi,tunaona mengi sana kweny ujenz watu wanaibiwa sana na ukijaa kwemy mfumo (yaan mtu akusimamie labda awe hajui kama ww ) ila utajikuta unajenga nyumba mbili kwa wakt mmoja..
Mwisho kabisa nikupe hii hamna fundi anweza kazi zote kuna zingina anakufanyi udalali ila sio mbaya ukimpa kazi kiwango chake ni kizuri atakutolea kazi kali sana.
Mwisho kila anaejenga hajui huwa wanaenda kujulia huko huko anza kujenga simamia mwenyew dukan uende mapema ili uzijue itakusaidia kupunguza gharama
Mwisho kabisa tafta mafundi watatu mpka wanne ukaangali maelezo na bei zao ukachagua mmoja
Fundi galagaja hapa ukiwa na swali au kuhus kujenga,kuezeka, blandering n gpsum uliz utajibiwa hizo zilizobaki kama litakuwa zito sana nitakuulizia wa wataalam zaid wa yangu wa upand huo mfano tailz na rangi au umeme na maji