Sijaupenda utaratibu wa NIDA wa kufungia namba

nusuhela

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2014
Posts
6,607
Reaction score
8,381
Leo nilienda kupata huduma inayohusisha namba ya NIDA. Cha ajabu huduma sijapata kwakua namba yangu ya NIDA imefungiwa. Nilipotaka kujua sababu, nimeambiwa kuna zoezi lilifanyika la kufunga namba zote ambazo wamiliki hawajafuata vitambulisho vyao.

Swali fikirishi. Ni wangapi wamehama mikoa walikojiandikishia kwa sababu mbalimbali na ikawawia vigumu kurudi kufuata vitambulisho?

Wao ndio waliosababisha watu kutochukua vitambulisho kwa wakati na wao ndio wanaowafungia watu wasipate huduma. Hii nchi inakera sana kuongozwa na watu wasiojiongeza.

Nimekosa huduma ya muhimu kwa huu mpango wao.... Inakera sana maana nilipopata taarifa ya kitambulisho changu kutoka, nilimuagiza mtu anichukulie wakagoma maana nipo mbali
 
Umefanya upumbavu, yamekupata na bado umeamua kuandika humu kujivunia UNDEZI wako
 
Back
Top Bottom