Sijawah kufanya biashara na nina mil 1.2 nifanye biashara gani ..??

Sijawah kufanya biashara na nina mil 1.2 nifanye biashara gani ..??

Nunua chupa kubwa za chai, uza uji wa ulezi sehemu zenye mikusanyiko yawatu wengi kama vituo vya daladala n.k. Uza asubuhi na jioni soon utakuwa kama Bakhresa.

Kuwa serioz mkuu milioni 1na laki 2 nikafanye biashra ya uji haa..!!ndo ushaur gni huo!
 
kiuhalisia kusema ufanye aina gani ya biashara ni ngumu ila naweza kukupa mawazo halafu uangalie mwenyewe,pata

wazo la biashara kwa kuangalia eneo ulilopo mfano labda nyumbani unapoishi angalia ni kitu gani kinakosekana

hapo mtaani kwenu na hicho kitu kinahitajiwa sana na wengi na wakati mwingine hulazimika kukifata mbali,ukipata

hicho kitu hiyo ndo biashara yako na hakika utapiga hela sana mpaka wengine waje wakuige wewe utakuwa mbali

sana. Pia unaweza angalia mazingira mengine mfano mahali unapotumia muda mwingi kukaa angalia hilo eneo lina

uhitaji gani,eneo lolote tu lichunguze lina uhitaji gani ukitumia hiyo fursa vizuri umetoka.Usijali hata kama

hiyo biashara unaona si hadhi yako wewe fanya usione aibu hapo ndo mafanikio yako.


Pia unaweza angalia ujuzi gani ulionao,huo ujuzi ugeuze uwe biashara wekeza hapo utaona matunda yake.

Shukrani kwa Chasha vijana wame elewa somo lako.
 
Last edited by a moderator:
Kuwa serioz mkuu milioni 1na laki 2 nikafanye biashra ya uji haa..!!ndo ushaur gni huo!
why not,si unaboresha,unauzia kwenye disposable papercup,unaupa quality nzuri,blueband,milk etc,each cup tsh 500.
8118paper_coffee_cup.jpg
 
why not,si unaboresha,unauzia kwenye disposable papercup,unaupa quality nzuri,blueband,milk etc,each cup tsh 500.
8118paper_coffee_cup.jpg

Nieleze vizur mkuu nimevutiwa na maelezo yako..!
 
Ni wazo tu lilikuja ghafla,hizo cup majuu ndo wanauzia kahawa na inakua na mfuniko kama unavyoona.
Porridge linatakiwa liwe na guality kwani hapa target yako ni wale wa maofisini mida ya kifungua kinywa ama kuanzia asubuhi .porridge linawekwa kwenye hizo vikombe na kupakiwa kwenye box mbili tatu.
Utafute binti salesgirl mwenye mvuto na ushawishi wa kibiashara kwa maana ya anaejua kuongea,yeye ndo atapita maofisini kuchukua order na kudeliver kama per day atauza vikombe 100 minimum hapo una 50,000.
Mtaji wa kuanzia haufiki hata 200,000.
Hakikisha kwanza unaanza na promo kwa kutoa free kwenye sehemu ambazo unajua ukiwashika utakua na soko la uhakika daily.
Huyo salesgirl wako umlipe vizuri na awe presentable.
 
kiongozi Elungata
kwanza nashukuru kwa aidea nzuri ,inaonesha ktk wazo unalopewa we jamaa huwa unatarget mara 2 mbele
hiyo huduma nimeikubali sana
nami nikipata mtaji lazima nijaribu
ishu ni hozo package hapa bongo sijui kama zinapatikana
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom