Sijawahi kujihusisha na uchawi, Je! naweza kulogeka?

Sijawahi kujihusisha na uchawi, Je! naweza kulogeka?

TuntemekeSanga

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2015
Posts
1,346
Reaction score
862
Wakuu heshima mbele,

Nakuombeni mnisaidie sana ktk jambo hili. Mimi ninaumri wa wastani tu japo unatosha(ni kijana). Mpaka sasa, sijawahi kwenda kwa mganga kutafuta uchawi wa kujiganga, sina chale hata moja(labda ya kujikwaruza mahali tu, sio ya uganga),wala sina destiny au interest kabisa na mambo ya uchawi mpaka sasa.

Ninaimani yakutosha ktk dini & Mungu wangu. Pia, nimewahi sikia kuwa, wachawi au uchawi/urozi humdhuru yule ambaye kwa namna moja au nyingine naye anajishughulisha na mambo ya kiganga au amewahi kuwatembelea kina Sangoma walau!

Sijawahi fanya hivyo na sina chochote cha kiganga/kishirikina nafsini au mwilini mwangu.

Sasa je! MCHAWI ANAWEZA KUNIDHURU AU KUNIROGA? (mfano kuniwangia au kuniua).

Msaada tafadhari wanaJamvi.
 
Mchawi anaweza kukuroga kwa kukujaribu tu kama ni moja ya mchezo wake wa kiuchawi sio wewe lazima uende kwa Sangoma. Ngojea nikupe Historia ya Maisha yangu Mimi kwa miaka 1980 nilikuwa ninaishi Mjini Dar maeneo ya Magomeni kulikuwa na bibi mmoja Mtu mzima wa kizaramo Mtaani mwetu

anasifika kwa uchawi na alikuwa ana mume wake wakati mimi bado kijana wa miaka 18 basi huyo bibi alikuwa ananitaka nifanye nae mapenzi kila anapo niona huyo bibi alikuwa ananiita

mchumba na kutaka kunikaribisha nyumbani kwake ni karibu na mimi ninapoishi. Nikawa ninamkatalia kwenda nyumbani kwake kwa sababu nilijuwa ana nia na mimi kimapenzi kwa

sababu mume wake ninamuhishimu hapo mtaani mwetu kama vile baba yangu ninavyomuhishimu. Nikamwambia Mama yangu Mzazi kuwa Bibi fulani yaani mfano mama asha

ananitaka mimi kimapenzi mama akaniambia Mwanangu huyo bibi (Mama Asha) anakutania nikamwambia mama ananiita nyumbani kwake anapokuwa yupo peke yake niende kufanya nini?

wakati Mume wake Baba Asha yupo kazini? Mama yangu akanijibu anakutania wewe Mama Asha anakuona kama mjukuu wake nikamuambia Mama sio ukweli mama kuna kitu unanificha ,

Mama yangu mzazi akasema ni kweli mwanangu ndio tabia yake huyo Mama asha kutania vijana wa kiume.Nikaacha tena kumdadisi mama yangu hapo. Matokeo yake yule bibi nimepita

uchochoroni mwa nyumba yake nilivyopita siku nyingine alipoona mimi sitaki kwenda kwake amesha nisumbuwa sana kwenda kwake nilipopita uchochoro alikuwa anafagia huko uchochoroni mwa nyumba yake nilipopita tu akainama kama anaokota kitu kumbe alikuwa anauchukuwa

mchanga wangu wa unyayo ili aende kuufanyia mambo ya uchawi kuniroga mimi. Mimi nikapita wala sikuangalia nyuma ilikuwa wakati wa jioni kunakaribia kuwa giza basi ilivyofika wakati wa kulala saa 6 usiku nikalala nikaota ndoto kuwa yule bibi amenichukulia mchanga wa unyayo

wangu ili aende kuniroga mambo yangu kimaisha yapate kuharibika. Niliota hivi aliuchukuwa huo mchanga wa unyayo wangu kisha akaufunga kwenye kitambaa cheusi mafundo 7 kisha akamfunga mtoto wa kuku mchanga kisha akaenda kumtupa kwenye nyumba iliyoanguka

wenyewe. Ili kama ninafanya kazi nifukuzwe na mambo yangu ya kimaisha yawe mgumu kama anavyoteseka huyo mtoto wa kuku na mambo yangu kimaisha niteseke. Hiyo ndoto niliota usiku na asubuhi nikamwambia Mama kuwa nimeota ndoto hiyo Mama yangu Mzazi

akashangaa sana nikamwambia mama Mimi Mungu ameniotesha kuwa huyu bibi rafiki yako jirani yetu sio mtu mzuri ni mchawi. Na nitakwenda kumwambia mambo anayonifanyia hayatokuwa na Mungu atamlipa kwa yote aliyoyatenda. Mama alinikataza na kunipeleka kwa

mganga nae alisema ni kweli amefanyiwa kitu kibaya mwanao na huyo jirani yako. Yule Mganga akanitibu kwa kunipa dawa na makombe ya kujipaka na kunifanyia dua ya kinga na

kuondowa huo uchawi aliofanya yule bibi jirani yetu mchawi.Matokeo yake mimi mwenyewe nikaenda kwa yule bibi na kumuapiza kuwa kitendo alichonifanyia cha kuniroga mimi wakati sina ubaya nae Mungu atamlipa kwa ubaya wake aliruka na kukataa bibi wa wa watu huyo

mama Asha kuwa hakunifanyia kitu kibaya ananipenda kijukuu tu sio kwa nia mbaya. Baada ya muda maombi yangu ya dua ju yake Mungu akayapokea haikuchukuwamuda mrefu mume wake

alikuwa anafanya kazi akaumwa gafla na miguu yake yote 2 imevimba kaenda hospitali kujitibia hakupona Ma-Dakatari wanasema hawaoni maradhi Huyo bibi mchawi jirani yetu mke wa huyo Mzee aliyevimba miguu akaenda kwa mganga akapewa Dawa na mganga akampa Masharti ya dawa

aliyopewa ampate mama aliye za watoto mapacha aje kumchuwa mume wake ndipo atakapo pona . Huyo bibi mchawi akaulizia mtaani mwetu ni nani Mama Mwenye watoto Mapacha akaambiwa

kuwa huyo unaye mtania mchumba wako yaani mimi (Mzizimkavu) ni pacha nenda kwa mama yake akusaidie kumtibu mume wako kwa hiyo dawa uliye pewa na mganga. Bibi mchawi akaja

nyumbani kwetu na kumuangukia mama yangu ili aweze kwenda kumsaidia kumchuwa mume wake miguu ili aweze kupona. Mama akaniuliza mimi je niende kumtibu Mgonjwa wa mchumba wako? kwanza nilikataa kwa kusema mama utakwendaje kumuopowa Mume wa mchawi wa yule bibi?

baadae mama kanibembeleza sana nikakubali na kumwambia nenda kamponyeshe lakini sharti moja mimi nitamuomba Mungu amuhamishe huu mtaa wetu huyo bibi mchawi. Nikamruhus Mama yangu akaenda kumtibia yule mume wa yule bibi mchawi kwa muda wa siku 3 alikuwa

mama anamchuwa kwa mafuta ya dawa alizopewa yule bibi mchawi na mganga wake akapona. Mimi nikafunga siku 3 na kumuomba Mungu amuhamishe hapo mtaani mwetu yule bibi mchawi akahama na kuuza nyumba yake na kurudi kijijini kwake Gezaulole. Hiyo nimekupa History ya

wachawi wakitaka kukuroga hawana Sababu wanaweza kukuroga na ukarogeka hata kama wewe hushiriki mambo ya kwenda kwa waganga . Inatakikana umuombe Mwenyeezi Mungu akuepushe na Mambo ya uchawi sio sababu eti wewe hushiri au kwenda kwa kwa waganga na hufanyi mambo

yoyote yanayohusu mambo ya kiimani ya uchawi kuwa wewe hutoweza kurogeka? Mchawi akikutaka hana sababu na uchawi upo ila hauwezi kukupata mpaka akuandikie Mungu ndipo waweza kudhurika.

Mkuu.@TuntemekeSanga Hicho ndio kisa kilichonitokea mimi kwa bibi wa kiuchawi jirani yetu hapo nilipo kuwa ninaishi ,Bii wa kiuchawi aliyenitaka nifanye nae mambo ya mapenzi na mimi nilimkatalia ndipo alipo jaribu Kuniroga mimi na ingawa hakuweza kufanikiwa.
 
Usimsikilize Mzizimkavu, yaelekea na yeye ndo walewale. HUROGEKI unless kuwe na conflict baina yako na mchawi na wakati huohuo wewe ndo uwe mkorofi e.g. umemdhulumu, umemchukulia mke, umemtapeli etc.....
 
Kitu hukijuia lakini unalazimisha kuonekana unajua!
 
Posti #2 ni uongo mkubwa....!! Uchawi ni ujinga na uoga na kukosa elimu/ufahamu wa kanuni za asili.

Kwa kuwa umeamua kuamini uchawi unafanya kazi, utalogeka hata ukiwa sayari ya Mars.

Kumbatia elimu na hekima ya kujua zuri na baya. Uchawi ni kwa wajinga.
 
Kumbe tuliozaliwa mapacha ni dili ngoja niichangamkie fursa
 
Uchawi upo na hilo halipingiki kabisa. Uchawi umeandikwa mpaka kwenye Biblia. Kwa wale wasomaji wa Biblia katika kitabu kile cha Kutoka, tunasoma jinsi Mungu alivyomtuma Musa kwenda kuwakomboa Waisrael kutoka Misri. Katika kitabu hicho, Farao alishindana na nguvu za Mungu kwa kutumia wachawi. Musa alipoangusha fimbo yake chini ikawa nyoka ili kumdhihirishia Farao kwamba ametumwa na Mungu, Farao aliwaita wachawi wake nao wakafanya hivyo hivyo.

Kwa hiyo uchawi upo siku nyingi tu. Ninachofahamu mimi kama haujihusishi na mambo ya uchawi, sio rahisi mtu akuloge. Ukiwa ni mcha Mungu uchawi hauwezi kukudhuru hata siku moja. Ninayo mifano ya mtu aliyejaribu kuniloga lakini aligonga mwamba na baadae alikuja kuniambia kwa nia ya kutaka kujua ninatumia kinga gani. Uchawi upo.

Tiba
 
Madam Tiba, ni kwakua umeelimika. Uchawi ni uongo. Hata huo ulioandikwa kwenye biblia ni uongo. Lila na fila.......
 
Ikiwa unamjua mchawi yeyote, mwambie aniloge........

kuna rafiki yangu mmoja alienda sumbawanga halafu akawa anawauliza vijana nasikia huku kuna wachawi sana mbona siwaoni ? giza lilipoingia alijuta na kulipokucha aliondoka na kurudi zake. Halafu hiyo kauli ndiyo iliyomponza kiongozi mmoja akasababishwa kulala nje bunda
 
Back
Top Bottom