Fundisi Muhapa
JF-Expert Member
- Nov 25, 2013
- 4,422
- 2,112
kuna rafiki yangu mmoja alienda sumbawanga halafu akawa anawauliza vijana nasikia huku kuna wachawi sana mbona siwaoni ? giza lilipoingia alijuta na kulipokucha aliondoka na kurudi zake. Halafu hiyo kauli ndiyo iliyomponza kiongozi mmoja akasababishwa kulala nje bunda
Asante kiongoz kwa kuni beep. Ngoja niisome mada kwanza.Nawashukuru sana WAKUU. Kuanzia MziziMkavu na wengine wote(ingawaje ukinzani wa mawazo umekuwa mkubwa mno kias kwamba bado nimebaki angani kias flan).
Ila imenisaidia kwa kias kikubwa.
Wapi Ishmael?
Kama hauna kinga halisi ambayo ni damu ya Yesu, kulogeka inawezekana kwako.Wakuu heshima mbele,
Nakuombeni mnisaidie sana ktk jambo hili. Mimi ninaumri wa wastani tu japo unatosha(ni kijana). Mpaka sasa, sijawahi kwenda kwa mganga kutafuta uchawi wa kujiganga, sina chale hata moja(labda ya kujikwaruza mahali tu, sio ya uganga),wala sina destiny au interest kabisa na mambo ya uchawi mpaka sasa.
Ninaimani yakutosha ktk dini & Mungu wangu. Pia, nimewahi sikia kuwa, wachawi au uchawi/urozi humdhuru yule ambaye kwa namna moja au nyingine naye anajishughulisha na mambo ya kiganga au amewahi kuwatembelea kina Sangoma walau!
Sijawahi fanya hivyo na sina chochote cha kiganga/kishirikina nafsini au mwilini mwangu.
Sasa je! MCHAWI ANAWEZA KUNIDHURU AU KUNIROGA? (mfano kuniwangia au kuniua).
Msaada tafadhari wanaJamvi.
Taja jina lako la ukweli jina lako jina la mama yako jina la baba yako na jina la ukoo wako humu humu ndani wako watu wachawi siwezi kukutajia kwa jina Mkuu Fundisi Muhapa kama kitu hujuwi bora uulize msikilize alivyosema Mkuu Tiba kuwa uchawi mpaka kwenye vitabu vya Dini umeandikwa Biblia na Quran vinasema uchawi upo ila usipende kuamini na kuabudia. Wewe ukitaka kujaribu kurogwa nenda Mikoa ya Pwani,Tanga, bagamoyo, Pangani, kilwa,Sumbawanga,shinyanga,Mtwara, lindi,Mafia,Tabora na kigoma kisha katembee na mke wa mtu. Kisha uone jinsi Uchawi utakavyo kupata .Ikiwa unamjua mchawi yeyote, mwambie aniloge........
Mkuu Ishmael Tupe Chanzo cha Duwa yako pamoja ushahidi wa dua yako kama inafanya kazi kweli? au umeitunga wewe Mwenyewe?MAOMBI YA KUSAMBARATISHA UCHAWI NA NGUVU ZA GIZA
Baba katika Jina la Yesu.
Laana zote nilizo tupiwa na wabaya wangu zimeshindwa kwa jina la Yesu na nazivunja na kuzisambaratisha kwa Damu ya Yesu. Mshindwe wote mnao tuma laana kwangu katika Jina la La Yesu.
Nawavunja na kuwaharibu na kuwakatakata Wachawi wote kwa damu ya Yesu.
Nasambaratisha kila neno la uovu lililosemwa juu yangu na famila yangu katika jina la Yesu.
Naharibu na kuisambaratisha madhabahu yenu mliyo fanyia kafara kwa damu ya Yesu.
Navunjavunja na kubomoa kila uovu na uchawi mnaonifanyia katika jina la Yesu.
Nairudisha misukule yote na majini yote yawarudie nyie na kuwalipa dhambi zote mnazo fanya katika jina la Yesu.
Naharibu kila uchawi, kila urogi, kila ndumba kila aina ya uovu ambao mnaufanya ili uniumize mimi na familia yangu katika jina la Yesu.
Nawateketeza kupitia damu ya Yesu Wachawi wote walio tumiwa kunitumia uchawi katika jina la Yesu.
Nawateketeza na kuwaharibu majini yote yaliyo tumwa kuja kufanya kazi hiyo waliyo tumwa na Wachawi katika jina la Yesu.
Nawateketeza na kuwauwa Makuhani wote ambao walienda kunishitaki kwa Wachawi ili waniharibie maisha, nawateketeza kupitia damu ya Yesu. Nawachoma kwa Moto wa Roho Mtakatifu katika Jina la Yesu.
Nateketeza aina zote za vyombo vya kichawi vilivyo tumiwa kuja kunichunguza katika jina la Yesu.
Naharibu fikra zao zote ambazo wanazitumia kufanya kazi zao za kichawi katika jina la Yesu.
Nafuta kumbukumbu zoote zangu ambazo wamewapa Mashetani, Majini, Roho chafu, nafuta hizo kumbukumbu kwa kutumia damu ya Yesu, katika jina la Yesu aliye hai.
Nawateketeza waweka kumbukumbu wa kimashetani kupitia damu ya Yesu aliye hai. Naharaibu na kuchoma kupitia moto wa Roho Mtakatifu makabrasha yote yenye kumbukumbu zangu katika jina la Yesu.
Kila uchawi ulio fanywa ili uje kuharibu maisha yangu na ubomoa kupitia damu ya Yesu.
Kila uchawi ulio fanywa ili uje kuniua nauvunja na kuuteketeza kupitia damu ya Yesu.
Kila uchawi ulio fanywa ili kuja kuiba mali zangu, nauvunja na kuubomoa na kuuharibu kupitia damu ya Yesu.
Kila uchawi ulio fanya kuja kuniharibia familia yangu, nausambaratisha na kuuvunja na kuubomoa katika jina la Yesu.
Kila neno la kichawi lililo tumwa ili kuja kuniharibia, kunidhihaki, kunitendea mabaya nalirudisha kwa aliye lituma katika jina la Yesu.
Kila uovu, uchawi, wanga, ndumba, ramli, yaliyo tumwa kuja kwangu navunja yote hayo kupitia damu ya Yesu na katika Jina la Yesu.
Nyota yangu ambayo wanaita nairudisha kupitia damu ya Yesu. Nyota yangu ya baraka nailinda na kuzungushia na kuizingira na damu ya Mwana Kondoo katika jina la Yesu.
Namteketeza yule mtu aliye kuja kuiba nyota yangu katika jina la Yesu.
Nateketeza mbinu zote wanazo tumia ili kuja kuiba nyota yangu katika jina la Yesu.
Nateketeza wivu wao, chuki yao, laana zao, maovu yao na kila aina ya uchafu ambao wanao kwa ajili yangu katika jina la Yesu.
Naizungushia na kuizingira nyumba yangu na damu ya Yesu.
Naishungushia na kuizingira familia yangu na damu ya Yesu.
Nashungushia na kuzingira maisha yangu yote na damu ya Yesu.
Navunja laana zote zilizo semwa na mabau zangu katika jina la Yesu.
Navunja laana zato ambazo zilisemwa bila ya mimi kufahamu, nazivunja na kuziharibu kupitia damu ya Yesu na katika jina la Yesu.
Narudisha kila mali walizo ziiba kutoka kwangu katika jina la Yesu.
Narudisha kila baraka walizo ziiba kwangu katika jina la Yesu.
Narudisha amani na upendo katika familia yangu.
Damu ya Yesu ipo juu ya Maisha yangu na inasafisha kila uovu, kila uchawi unaaribiwa na damu ya Yesu katika jina la Yesu.
Leo hii mtaiona Nguvu iliyopo katika damu ya Yesu.
Katika Jina la Yesu aliye hai ninaomba.
Amen
Ikiwa unamjua mchawi yeyote, mwambie aniloge........
Tupe Aya kwenye Biblia umepata wapi hayo maneno ?Mkuu IshmaelYote hayo ni maneno ya Mungu. Just read between the line utasoma aya kibao za kwenye Biblia.
Karibu kwa Yesu
Unafahamu nani aliambiwa hayo maneno?Mkuu.@Ishmael BWANA YESU Alikuwa akisali na kuomba hivi Soma hapa:
Mathayo:6-9-13
9 Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje,
10 Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.
11 Utupe leo riziki yetu.
12 Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.
13 Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]
Sasa hivyo ndivyo alivyokuwa anasali kuomba Bwana YESU wewe nani aliyekufundisha KuSali namna hiyo?
Mkuu Ishmael inaonyesha wewe Biblia unasomaUnafahamu nani aliambiwa hayo maneno?
ZAIDI YA HAPO.
Nionyeshe, wapi tunasoma tena Yesu akisali hayo maneno?
Taja jina lako la ukweli jina lako jina la mama yako jina la baba yako na jina la ukoo wako humu humu ndani wako watu wachawi siwezi kukutajia kwa jina Mkuu Fundisi Muhapa kama kitu hujuwi bora uulize msikilize alivyosema Mkuu Tiba kuwa uchawi mpaka kwenye vitabu vya Dini umeandikwa Biblia na Quran vinasema uchawi upo ila usipende kuamini na kuabudia. Wewe ukitaka kujaribu kurogwa nenda Mikoa ya Pwani,Tanga, bagamoyo, Pangani, kilwa,Sumbawanga,shinyanga,Mtwara, lindi,Mafia,Tabora na kigoma kisha katembee na mke wa mtu. Kisha uone jinsi Uchawi utakavyo kupata .
Nashukuru umehabarisha vyema.
Hakuna uchawi, kuna ujinga wa kuamini uchawi tu.