Sijawahi kuona mwanamke ananuka miguu au soksi

Sijawahi kuona mwanamke ananuka miguu au soksi

Superbug

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
13,864
Reaction score
35,079
Huu ndio ukweli wangu toka nizaliwe sijawahi kuonamwanamke ananuka miguu au soksi je nikwasababu wanawake ni wasafi? Au ni kwasababu hawavai Soksi mostly ni open shoes?
 
Kuna wale ambao hawapasuki visigino miguu yao haitoi jasho,wasiopasuka hutoa jasho,jasho linapochanganyikana na vumbi likafungiwa ndani ya soksi huvunda na kutoa harufu mbaya. Ila wanawake wengi huvaa viatu vya wazi.
 
Hata vikwapa na midomo pia hawanuki. Wanawake tupeni Siri ya kutonuka midomo.
Siri kubwa ya kutonuka mdomo ni kusafisha ulimi ukiwa unasafisha meno. Ulimi una hifadhi mabaki ya chakula kutokana na maumbile yake. Safisha ulimi asubuhi na kabla hujalala ikiwezekana kila unapomaliza kula.

Kikwapa, ukiwa unaoga safisha kwapa vizuri na maji na sabuni. Usitunze nywele kwapani. Ukisha jikausha unaweza kuweka deodorant.
 
kuna wale ambao hawapasuki visigino miguu yao haitoi jasho,wasiopasuka hutoa jasho,jasho linapochanganyikana na vumbi likafungiwa ndani ya soksi huvunda na kutoa harufu mbaya.Ila wanawake wengi huvaa viatu vya wazi
Kupasuka miguu ni dalili ya uchafu, miguu inapasuka kwakua ngozi iliyotakiwa kutoka imeachwa na kuwa ngumu.

Ukiwa umepasuka miguu isafishe na jiwe au brush ngumu. Ikitakata paka vaseline vaa socks kutunza unyevu nyevu ulale.
 
Wanawake mara nyingi viatu vyetu ni vya wazi si wavaaji wa socks.
 
Sitamsahau yule mgeni alikuja kwetu kipindi kile, dakiza 30 zilikuwa za mateso sana na ile harufu naikumbuka hadi leo, zaidi ya miaka 20 imepita
 
Wengi wanavaa sana open shoes, pia kama ana viatu vya kufunika wanajitahidi kuwa na pair zaidi ya moja.
 
wanawake kwa asili ni wasafi,kunukanuka jasho kwao ni aibu.Ndiyo maana wakiwa ndani ya nyumba inapendeza hata kama ni pango.Mageto yao ni masafi mno kuliko ya wanaume,wana mavazi mengi ya kubadilisha kila mara.Kuogaoga kila mara ni kawaida yao,saa ngapi watanukanuka uvundo? By the way hawana kazi za suluba zinazowafanya watokwe jasho
 
Siri kubwa ya kutonuka mdomo ni kusafisha ulimi ukiwa unasafisha meno. Ulimi una hifadhi mabaki ya chakula kutokana na maumbile yake. Safisha ulimi asubuhi na kabla hujalala ikiwezekana kila unapomaliza kula.

Kikwapa, ukiwa unaoga safisha kwapa vizuri na maji na sabuni. Usitunze nywele kwapani. Ukisha jikausha unaweza kuweka deodorant.
Kuuumbeh. Nilishaambiwa Siri ya mwanamke mzuri Ni ULIMI. kumbe walikua na maana hiyo. Wahaya wenzangu mmesoma hayo ☝️maelekezo ya ulimi?
 
Hata vikwapa na midomo pia hawanuki. Wanawake tupeni Siri ya kutonuka midomo.
Weeeeh..!!!!
Hapo kwenye vikwapa na midomo sio kweli!
Baadhi yao wapo wanaonuka vikwapa na midomo pia
 
Back
Top Bottom