Sijawahi kuona trafiki akimpiga faini bodaboda, Serikali ifute kabisa hii faini

Sijawahi kuona trafiki akimpiga faini bodaboda, Serikali ifute kabisa hii faini

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2016
Posts
17,506
Reaction score
16,003
Ndugu zangu,

Nimekuwa nikipita barabarani ukweli ni kwamba ni ngumu sana trafiki kukamata bodaboda. Mara nyingi nimeona wanaokamatwa na trafiki ni waendesha magari sio waendesha bodaboda.

Hata kwa hii faini ya elfu kumi sioni trafiki wakikusanya wala bodaboda wakilipa. Hesabu ya bodaboda kwa siku ni shilingi 7000.
 
Nyingi ni ajali na uhalifu,hakuna atakayeacha pikipiki yake Polisi kisa shilingi 30,000. Wengi wa vijana hawa hizo pikipiki sio zao
Nenda vituo vya polisi ukaone lundo la pikipiki na bajaj ndio urudi hapa.
 
Kwa mujibu wa sheria za traffic

Boda boda inatambulika kama jamii ya baiskeliii
 
Nyingi ni ajali na uhalifu,hakuna atakayeacha pikipiki yake Polisi kisa shilingi 30,000.Wengi wa vijana hawa hizo pikipiki sio zao
Kumbuka hiyo elfu 30 ni fine ya ndani ya siku 7. Ikizidi wiki bila kulipa deni linaongezeka, kwahiyo ukipigwa fine mara mbili jumlisha na fine ni lazima chombo chako kipelekwe polisi.

Tena kwa Bajaj na Pikipiki, polisi huwa wana siku maalum, wakizitaka wanaweka block kabisa wanakamata kila mwenye pikipiki anayepita.

Tena sehemu kama Kilwa road traffic huwa wanakodi kabisa SEMI TRAILER wakasomba pikipiki zote.
 
Hata huku Arusha sijaona Trafiki wakihangaika na Bodaboda, na nilishawahi kuhoji humu kuwa Mwenye Gari unakamatwa na Trafiki alafu hapohapo wanapita Bodaboda wapo mishikaki, hawana Helmeti, wapo spidi lakini wala huoni Trafiki akihangaika.

Labda Waziri anapata taarifa zisizo sahihi kutoka kwa Jeshi la Polisi, au la labda wanataka waanze kazi hiyo rasmi kama sehemu ya mpango wa kuongeza mapato.
 
Boda boda wao wanacheza na askari we wa voda faster,tena mpka wanakimbizana mpaka vichochoroni

Ova
 
Samia ni Magufuli.

Samia aliteuliwa na Magufuli kama alivyoteuliwa Sabaya, Hapi, Majaliwa,Mpango etc

Acha wanafunzi wa Magufuli waumane
 
Samia ni Magufuli.

Samia aliteuliwa na Magufuli kama alivyoteuliwa Sabaya, Hapi, Majaliwa,Mpango etc

Acha wanafunzi wa Magufuli waumane
Samia sio Magufuli wewe, Magufuli alimtaka Mwinyi mkwere akamlazimisha agombee na Samia kwa hoja ya Jinsia. Samia sio Magufuli.
 
Hiyo yote ni chanzo cha mapato serikali haina hela ati.

Alaaaa
 
Hizo nyingi ni ajali na zinajihusisha na uhalifu...kwa makosa ya kawaida barabarani ni ngumu kumpiga faini bodaboda.Ni ngumu pia kuitelekeza pikipiki polisi kwa kudaiwa 30,000
Kuna polisi wanaitwa sijui tigo nini ni wasumbufu haswa wanakamata sn wasiokuwa na leseni, kofia na makosa mengine mtaani
 
Mzee bodaboda wanatembezewa patrol na jamaa maarufu kama Tigo, wanakula sana hela za bodaboda na inawezekana bodaboda ndo watoaji faini wakubwa kwa hapa Dar Ila sizani kama pesa zinafika sehemu husika
 
Back
Top Bottom