Sijawahi kuona trafiki akimpiga faini bodaboda, Serikali ifute kabisa hii faini

Sijawahi kuona trafiki akimpiga faini bodaboda, Serikali ifute kabisa hii faini

bodaboda ni kama watoto mbwa. kwa trafiki sio kazi rahisi kuwadhibitiki, hii ni kutokana na mazingira yao ya ufanyaji kazi.

kitu pekee jeshi la polisi linaweza kufanya ni kuunda taskforce maalum ya kupambana na bodaboda tu.

nakumbuka wakati fulani enzi za jk kulikuwa na askari wanatembea kwa pikipiki kwa jina maarufu "tigo". hawa jamaa walijikita kupambana na bodaboda. hata hivyo makabiliano yao na bodaboda yalikuwa kama vita huku uswahilini.

niliwahi kushuhudia "tigo" wakila mzinga kwa kumbikiza bodaboda. bodaboda aliwazidi maarifa.
 
Back
Top Bottom