Sijawahi kuwa Monitor, ila nikiwa Rais nitafanya haya

Hatutaki udikteta wa ki Putin nchini kwetu.
 
Hakika
 
Hatutaki udikteta wa ki Putin nchini kwetu.
𝐏𝐮𝐭𝐢𝐧 𝐢𝐬 𝐭𝐡𝐞 𝐨𝐧𝐥𝐲 𝐏𝐞𝐫𝐬𝐨𝐧 𝐢𝐧 𝐭𝐡𝐞 𝐖𝐨𝐫𝐥𝐝, 𝐰𝐡𝐨 𝐝𝐢𝐝𝐧'𝐭 𝐬𝐞𝐥𝐥 𝐡𝐢𝐬 𝐂𝐨𝐮𝐧𝐭𝐫𝐲 & 𝐩𝐞𝐨𝐩𝐥𝐞 𝐭𝐨 𝐆𝐥𝐨𝐛𝐚𝐥𝐢𝐬𝐭𝐬
 
Who are Globalists?
 
Ndio maana huwezi kuwa Rais,maana bado hata hujui mifumo ya dunia Kiuchumi,kijamii na kiutawala inavyoendeshwa.
1.eti utafuta somo LA Historia-bila historian utajua umetoka wapi na unakwenda wapi?.tambua kuwa kila kitu na kila chochote tunachokifanya ulimwenguni kote tunajifunza wenzetu waliotutangulia walifanyaje-hii duniani kote.
2.Huongezi ajira kwa kupunguza umri wa kustafu,kama ingekuwa hivyo basi Nchi zote duniani ajira isingekuwa tatizo.gharama za kuwastafisha watu wakiwa na jmri mdogo ni kubwa kuliko mishahara wanayoipata kufikia umri wa kustaafu.

Ajira zinaongezwa kwa kuanzisha viqanda vingi na kuaanza kuzalisha,kwa kutumia rasilimali zilizopo..
3.Jeshini na uzalendo wapi na wapi,kama unadhani kwenda jeshini ndio uzalendo na kuwa Rais (mwanasiasa) sio uzalendo,mbona wanajeshi ni wengi kuliko hao wanasiasa- kwa nini wasitumie uzalendo wao kuirekebisha Nchi.

Hivi unajua kuwa Rais anaendesha Nchi kwa 98% kwa kumtegemea Mkuu wa Majeshi?,kwa hiyo Mkuu wa majeshi hana uzalendo anaona anayemkingia kifua anaharibu Nchi na yeye anaangalia?.

Nchi kukuosa uzalendo kunatokana na watu wake kutokuwa na maarifa ya kutosha,kama kila moja wetu angeona uchungu wa Kofi yetu basi hamna mwanasiasa angecheza na fedha ya umma.
 

Totally sikubaliani na wewe kabisa.
Kwanza hiyo mifumo ya kidunia unayosema siyo lazima kila nchi iifate.

Kuna mifumo mingine ni ya kipuuzi tu.

Na mifumo unayosema wewe kuwa ya kidunia ni ile ambayo imekuwa introduced na nchi za magharibi hasa Marekani na umoja wa ulaya (EU) ambayo hiyo mifumo wameileta kwa ku-favour maslahi yao wenyewe huku wakivuruga maslahi ya wengine kwa kutumia Ubeberu wao.

Unaweza kuchukua mkondo tofauti kabisa na mifumo yao na ukafsnikiwa na ndiyo maana ukiamua kuchukua mkondo tofauti na wao wanavyowaza basi wanakuharibia ili nchi yako isitawalike, vikwazo vya kiuchumi vingi ama kukuua kabisa.

Na mifumo hayo unayoyasema wewe ndiyo hayo yanatumika kwa ulimwengu wa tatu sasahivi lakini umesaidia nini zaidi mbona tunaendelea na matatizo yale yale tena ndiyo yanazidi zaidi.

Ni mifumo ya kipuuzi sana hiyo.

Na ni lazima nikukanye kwamba unaposema jeshi halifunzi ama halina uzalendo wowote ujue unalikosea heshima.

Kwanza lazima ujue nchi nyingi duniani jeshi na siasa/serikali huwa havitakiwi kufanya kazi kwa kuingiliana.

Yaani jeshi ni state within a state, ni kama serikali inayojitegemea kabisa ndani ya nchi.

Na wanajeshi wazalendo mara nyingi wamepindua nchi zao kwa ajili ya maslahi ya wananchi pale walipoona wanasiasa wanaleta uchuro.

Angalia wakuu wa majeshi miaka ya juzi hapa huko Misri,Sudan,Chad,Guinea,Burkina Faso,Mali.

Wananeshi wazalendo walupindua serikali za kisiasa na kuchukua nchi kwa sababu ya upuuzi wa wana siasa
 
Haha ha ha! Haujielewi hata Sudani hamna Bu.nge ni wanajeshi tu ila Khartoum ni mapigano na nchi wameiharibu tayari
 
Angalia tu North Korea ni jeshi na umaskini wa kutisha na hofu kwa kila mtu ndo unataka Tz tuwe hivyo?
 
Angalia tu North Korea ni jeshi na umaskini wa kutisha na hofu kwa kila mtu ndo unataka Tz tuwe hivyo?

Kuna udikteta wenye akili na udikteta usiyo na akili.

Udukteta usiyo na akili na kama ule uliokuwa wa kina Idd Amin Nduli Dada na Kina Mobutu Seseko.

Hata North Korea ni kwa vile tu inaishi chini ya vikwazo vingi dhalimu vya US na UN, ila unadhani kama siyo hivyo vikwazo vilivyodumu kwa miaka unadhani hiyo North Korea ingekuwa maskini kama ilivyo leo.

Alafu North Korea inaendesha uchumi wake kijeshi siyo kama huu upuuzi wa huku kwetu.


Lile ni taifa ambalo muda mwingi limejihami kijeshi kwa sababu lina adui mkubwa US ambae anatishia usalama wake.
 
Wakati wenzake wanastrugle kuwa globalists yeye alikuwa wapi? Hii statement yako inaonesha kuna wengine wenye nguvu zaidi kuliko huyo kichaa wako.
 
Katika yote uliyoandika kwamba utafanya mabadiliko hakika sijaona hata moja litakalofanikiwa. Umeangalia uongozi wa nchi kwa nje tu jinsi mambo yanavyofanyika yakadhihiri lakin kwa mdani kuna msukumo mkubwa wa viongozi kufanya hata wasioyapenda na kuyataka.
Katika malengo yako hakuna "kujitegemea kiuchumi" AMIN AMIN NAKUAMBIWA hakuna maamuzi yako kama hauna uchumi imara.
 
Adui mkubwa ni yule ambae hataki mimi nijitegemee, ambae ni mataifa mapigaji ya kibepari especially US and Europe.

Kwa sababu wanavuna kwetu kwa hiyo natambua fika kabisa kuwa hawa ndiyo watakuwa maadui wangu wa kwanza maana hawatapenda nitalachokifanya kwa mustakabali wa maisha bora ya watanzania.

Najua jinsi walivyo haribu uchumi wa Zimbambwe kwa maslahi yao tu binafsi, Libya pia n.k.

Lakini mimi naamini tukiungana tunaweza kabisa, kwani wachina waliwezaje mbona miaka ya 1960's uchumi wa China na TZ ulikuwa almost sawa tu ?

Hii nchi inahitaji kiongozi Mzalendo na mwenye maamuzi magumu kuliko hata alivyokuwa magufuli.

Mimi naamini ukiwa na vision nzuri na wananchi wayaona matunda mbona watakuunga tu mkono.

Yaani nitaifungia hii nchi kama kisiwa kwa muda wa miaka kadhaa kwanza hata simu na magari hamtaagiza China na Japan kwanza alafu najenga vituo vingi vya sayansi na technolojia nione kama ndani miaka 15-20 kama hamjaanza kutengeneza magari yenu wenyewe na kuunda cm zenu wenyewe
 
Wakati wenzake wanastrugle kuwa globalists yeye alikuwa wapi? Hii statement yako inaonesha kuna wengine wenye nguvu zaidi kuliko huyo kichaa wako.
Ndo u-struggle kuwa shoga na lesbian.

Fala kweli we na hao watandawazi wenzako
 
Usisaha
Usisahau kufuta ujinga wa kurudia watu walewale kwenye uongozi wa juu wenye watu mil62 kwa sasa lakin kila siku ni
Marope, miguu, et all .

Tenganisha utendaji wa wananch na serikali.
Kuwe na mfumo mwingne wa kupata mawaziri ili mbunge aweze kumsema vizuri na kumchukulia maamuzi waziri.

Usisahau pia spika ni muwakilishi wa wananchi akiwa spika anasemea wapi yale anayotumwa na wananch wake ? Weka utaratibu tofauti wa kupata spika.

Rudisha somo la historia ya Tanzania alilotaka kutengeneza jiwe likaondoka zake bila maelezo wala usuli.

Na mengne mengi. BUT USIACHE KUNITEUA KUWA WAZIRI WA ELIMU BADO NNA LA KUFANYA KWENYE HII NCHI YA WATANGANYIKA.
 
Unaona kuna umuhimu wa spika na Bunge kwa sababu tayari una wazo negative kwa serikali kuwa haitokuwa adilifu kwenye uwajibikaji wake.

Trust me nakwambia kuwa kama serikali itakuwa adilifu na kuwajibika kwa haki kama hii ninayoiwaza mimi, basi hakuna umuhimu kabisa wa kuwa na Bunge wala mawaziri Lundo.

Kila kitu kitaenda murua kabisa na mabalioni ya pesa yanayotumikaga na wabunge yote nayaelekeza kwenye mahospitali na madawa huko ili watu wawe na afya bora.

Hayo mabilioni yanatosha kabisa kumkatia kila mtanzania bima ya afya.

Mimi huwa naamini Bunge halina maana yeyote zaidi ya kujadili mambo ambayo hata serikali huyapuuza na haifanyii kazi.

Kwa hiyo unaweza kuona wanakulaga pesa za bure tu pale alafu baada ya miaka mitano wanarudi na majumba ya kifahari na mahoteli mtaani utadhani Bungeni ndiyo walifata hayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…