Sijawahi kuwa na Imani na Freeman Mbowe kama mwanasiasa mpigania haki na uhuru

Sijawahi kuwa na Imani na Freeman Mbowe kama mwanasiasa mpigania haki na uhuru

Tazizo lenu majukumu ya Wanaharakati mnayapeleka kwa Wanasiasa. Wanasiasa ni wafanya biashara wenye 'mamlaka' na interest tofauti tofauti kupitia ushawishi wa makundi ya watu wanaowaongoza. Wanaharakati walimalizwa na kitu kinachoitwa 'Demokrasia'.

Ila wewe pia kama unategemea 'upinzani' ukupambanie kwenye jambo unalohisi ni haki yako basi unahitaji kupimwa akili, upinzani ni tawi mchepuko la serikali, wenye uwezo wa kuwa na upinzani thabiti ni wananchi. Kama wewe na mimi tumeridhika na hali iliyopo unataka upinzani ufanye nini?? upigane kwaajili yetu??!!
 
Mbowe kapitiliza.uungwana ..nadhani mwenyekiti angekua Lema tungemfurahia .juzi kanikwaza sana Mbowe kutuliza ghasia...angeacha tu kama haoni..
Watu wamejifunza kitu kuhusu Mbowe kule Tanga
 
Ulitaka juzi kwenye msiba avue shati siyo!! awahamasishe vijana wamtimue na kumdhalilisha Masauni msibani then ww ungeridhika kwamba Mh. Mbowe ni Jembe.
 
Ndivyo ilivyo katika nafsi yangu kwa muda mrefu sana katika anga za siasa za Tanzania.

Freeman Mbowe kwangu mimi hajawahi kuwa na ushawahi wa aina yoyote ile, sio mpigania haki wala uhuru. Binafsi Imani yangu tangu enzi hizo najua Mbowe anafanya biashara ya siasa kupitia chama cha siasa yaani Chadema.

Nawapa pole watu wote wenye Imani na Freeman Mbowe na Chadema yake.

Siku hizi wanasiasq wanakemea uovu kisharobaro na kinyolonyolo.

Tuna upinzani ushuzi wanaoishi kwenye ghetto la popobawa.

Karibu ulingoni tubutue kwenye ulingo wa akili

Wadiz
Endelea kuwa na Imani na Makonda, Nape na January.
 
Haya sasa wewe ndio Mwenyekiti wa chama ungefanyaje?

Ungejitwisha mabomu ukalipue ikulu au?
 
Mbowe hana akili zenye uwakilishi mtambuka ana nadharia za ukipepeo. Na akiwa Tanga kwenye msiba wa kibao amedhihiri hilo, hawezi kuitisha press conference after every three days kupigania haki na uhai wa waliopotea.

Mbowe anapenda camera na amehodhi uzito wote, you can see Tundu Lisu amekosa airtime ya kutosha yenye platform ya kichama kuongelea mambo mazito.

Siku Lisu akiamua kuwa mpinzani mwenye Chama chake ama ahamie chama kingine Chadema itakuwa kama NLD
Mbowe ni very smart katika siasa za Tanzania na ukitaka kujua hilo angalia namna alivyo pika vijana ambao wengi aliwatoa vyuoni na kuwatengeneza hadi ccm wakawachukua na kuwapa madaraka, Ccm kama kawaida wamejaribu sana kumdhoofisha na hizi kelele zote ni kwasababu ccm wameshindwa wanataka Mbowe atoke ili waweke pandikizi lao ambalo watakuwa wanaliburuza watakavyo unaweza kuona kwenye vyama vingine namna wanavyo kunja mkia kwa ccm.

Kingine omba sana Lisu asije kuwa mwenyekiti wa Chadema au awe na chama chake hii nchi itakuwa ni vurugu kila siku Lisu hana cha kupoteza ccm wanatakiwa wamshukuru sana Mbowe jamaa anabusara sana uliona kwenye msiba waziri anazomewa yeye iliidi asimame kutuliza watu fikiri tu haya mambo ............ Sijui nyie maccm huwa mnataka nini.
 
Ukiona umuelewi jua mbowe anafanya siasa smart kuliko unavyotaka.Mnataka siasa za fujo na kufoka foka na chuki na ugomvi nia yenu ni ili Chadema kionekane ni chama cha ugomvi kifutwe mfurai.mbowe sio mjinga kiasi hicho.Anaamini katika siasa za hoja na masuala ndo maana Cdm inazidi kukua nakua imara pamoja na misukosuko inayopitia wanachama wake.Kama unadhani ni rahis anzisha chama chako uone.
 
Ndivyo ilivyo katika nafsi yangu kwa muda mrefu sana katika anga za siasa za Tanzania.

Freeman Mbowe kwangu mimi hajawahi kuwa na ushawahi wa aina yoyote ile, sio mpigania haki wala uhuru. Binafsi Imani yangu tangu enzi hizo najua Mbowe anafanya biashara ya siasa kupitia chama cha siasa yaani Chadema.

Nawapa pole watu wote wenye Imani na Freeman Mbowe na Chadema yake.

Siku hizi wanasiasq wanakemea uovu kisharobaro na kinyolonyolo.

Tuna upinzani ushuzi wanaoishi kwenye ghetto la popobawa.

Karibu ulingoni tubutue kwenye ulingo wa akili

Wadiz
zingatia msingi na malengo ya kuanzishwa kwa chama chenyewe anacho kiongoza kiongozi huyo, ndipo sasa unaweza kugundua anaongoza taasisi ya kijamii, chama cha siasa au ni chember of commerce?🐒

kisha ndipo utaelewa huyo kiongozi ni wa nini pale chamani na ana pambania nini zaid 🐒
 
Ndivyo ilivyo katika nafsi yangu kwa muda mrefu sana katika anga za siasa za Tanzania.

Freeman Mbowe kwangu mimi hajawahi kuwa na ushawahi wa aina yoyote ile, sio mpigania haki wala uhuru. Binafsi Imani yangu tangu enzi hizo najua Mbowe anafanya biashara ya siasa kupitia chama cha siasa yaani Chadema.

Nawapa pole watu wote wenye Imani na Freeman Mbowe na Chadema yake.

Siku hizi wanasiasq wanakemea uovu kisharobaro na kinyolonyolo.

Tuna upinzani ushuzi wanaoishi kwenye ghetto la popobawa.

Karibu ulingoni tubutue kwenye ulingo wa akili

Wadiz
Kiu yako ulitaka yatokee machafuko Tanga zaidi eti, vijana wa watu maskini wamekuja kumsindikiza mzee wao aliyeuawa kinyama na majingili wa serikali. Vijana wana uchungu na hasira wanataka kumtafuna Masauni mbele ya mbwa wake waliokua wamebeba kila aina ya silaha wawatawanye vijana wale kama kuku wa mdondo wakimtetea bosi wao. Vijana waliokua hawajabeba hata sindano ya kuwasaidia katika vurumai hilo. Kesho nyie nyie muwe wa kwanza kumvictimize Mbowe kuwa ndio chanzo cha mauwaji na kwamba alikua na nafasi kubwa ya kuzuia kadhia hiyo huku akisubiri utaratibu mwingine?
Umesahau baada ya chafua chafua ya uchaguzi iliyo kua inafanyika kipindi cha mwendazake, Mbowe alifikia enough is enough akawahamsisha watu Kwenda Kinondoni kwa Mkurigenzi kwa kuandamana? Kwmaba umesahau mbwa wa mambo sasa waliyavamia maandamano yale, wakaua mwanafunzi aliyekua tegemeo la familia yake, na Baadaye wakamfungulia Mbowe na Wenzazake kesi ya kusababisha mauaji ya Akwilina? Umesahau wauwaji hao hao wakajitolea kugharimia maziko na kumsomesha mdogo wa Marehemu? Utu uzima sio mvi tu bali ni Busara pia.
 
Ulitaka juzi kwenye msiba avue shati siyo!! awahamasishe vijana wamtimue na kumdhalilisha Masauni msibani then ww ungeridhika kwamba Mh. Mbowe ni Jembe.

Mbona yeye hakwenda kufanya? Amekaa na taulo lake anatuma msg tu
 
Back
Top Bottom