lyinga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2013
- 2,496
- 1,057
Ndugu zangu tunapozungumzia utaifa hembu tuweke ushabiki wa vyama pembeni na kuuvaa uzalendo jamani siku zoote mbinguni na duniani inajulikana chaguzi salama na zahaki huwa zinafanyika kwa siri kuondoa migongano ambayo inaweza kujitokeza mbeleni na ndio maana hata mwenyezi Mungu akaweka kifo kuwa siri hembu fikiria ungekuwa unaambiwa utakufa kesho saa fulani na dakika kadhaa dunia ingekuwaje?
Kwa nini suala upigaji kura wa siri inawatia hofu baadhi ya vigogo wa ccm kwamba ndio itakuwa mwisho wa ufalme wao wa uongozi waliojiwekea?
Nini kibaya walichokifanya wanahofia wakiondoka madarakani historia itawahukumu? Jamani tunawaomba nyie wabunge wa ccm msituharibie katiba yetu sisi wananchi ndio tuliyoitaka kwa mustakabali mzuri wa nchi yetu tunaomba msiingize ushabiki wa chama kwenye mustakabali wa wananchi kama hamna nia mbaya na sisi wananchi tuachieni kura ya siri ambayo pasina shaka haina mawaa mbona kwenye kuchagua marais , wabunge, na madiwani huwa hampigi kelele kura za wazi kuna nini hapa kimejificha?