Sijawahi ona kura ya uchaguzi ikipigwa wazi


Wewe unaye taka kura ya wazi ndiye msaliti namba moja.acheni ubabe kura ni siri.
 

Kwani umeona kura ngapi za Katiba.usijishibishe upepo.kwanza ufahamu ccm inatuwakilisha wananchi tulio wengi.wananchi ni zaidi sana ya wana JF wanajiita majina ya siri
 
Kwani umeona kura ngapi za Katiba.usijishibishe upepo.kwanza ufahamu ccm inatuwakilisha wananchi tulio wengi.wananchi ni zaidi sana ya wana JF wanajiita majina ya siri
najua ccm inawakilisha wengi na ndio chama tawala kilichounda serikali,ila ninachoongea mimi,tangu chama kimoja mpaka sasa kura zote upigwa kwa siri sijaona ya wazi
 
Kwani hapa nani anafanya uchaguzi kama kweli unafikiri sawa sawa tumia akili kidogo uliyonayo basi.
 
Hii siyo aibu ya CCM tu ni aibu yetu sote kwasababu mtu mwenye akili timamu utaileza vipi! Hii imenikumbusha tukio jingine kama hilo wakati huo KANU chini ya Arap Moi wanatawala Kenya! Walianzisha kura ya mlolongo ambako wapiga kura wakijipanga nyuma ya mgombea!!

Inawezekana Mungu hakupanga Kikwete na CCM yake wasimamie kuandikwa kwa Katiba mpya ambayo itahakisi kwa kiwango kikubwa maoni ya wananchi. KANU na Moi walipoteza fursa hiyo kwa mawazo ya kijima kama tunavyo waona CCM.

Chama ambacho kinafanya chaguzi za siri kuwachagua viongozi wake ktk ngazi zote leo kinaogopa kura ya siri ktk jambo nyeti kabisa,KATIBA! Ni aibu kubwa sana. Ni kuishiwa na kufirisika kwa hoja kwa hali ya juu! Nchi nyingine Jeshi lisingesubiri waendele kuharibu pesa za wananchi!!!
 
Mbona unajipinga mwenyewe! Nani mwoga,
Anayepigania kura za kificho au za wazi.usiendeleze ulaghai eti unatetea wabunge wa ccm wanaotishwa.hayo ni machozi ya mamba
 

Hili wala si swala la CCM. Nakuomba utulie ujielimishe. Usome kuhusu mabunge yote ulimwenguni. Hakuna Bunge hata mija linalofanya maamuzi kwa kura ya siril kura ya siri ni kwa kumchagua mtu.
 
najua ccm inawakilisha wengi na ndio chama tawala kilichounda serikali,ila ninachoongea mimi,tangu chama kimoja mpaka sasa kura zote upigwa kwa siri sijaona ya wazi

Kama hujaona kura ya wazi nakuomba uangalie au usome kuhusu maamuzi ya MaBunge mengine yote. Kura ya maamuzi ya kikao au ya Bunge ni ya wazi.Kura ya kumchagua mtu ndiyo ya siri. Ni mambo mawili tofauti kabisa.
 
Naona unapotoka kwa kuingiza mambo ya jeshi. Pili, jielimishe. Kura ya maamuzi ya Bunge popote ni ya wazi. Kura ya kumchagua mtu ndiyo ya siri. Mambo mawili tofauti kabisa
 
Nakuomba utazame tena maandishi yako. Yametofautisha kura ya maamuzi ya Bunge na kura ya kumchagua mtu. Hilo ndilo jibu. Ni vitu viwili tofauti. Popote ulimwenguni, kura ya maamuzi ya Bunge ni ya wazi, na ya kumchagua mtu ni siri.
 
Naona unapotoka kwa kuingiza mambo ya jeshi. Pili, jielimishe. Kura ya maamuzi ya Bunge popote ni ya wazi. Kura ya kumchagua mtu ndiyo ya siri. Mambo mawili tofauti kabisa
Hivi mkuu bado mnafikiri ni kile kipindi cha zidumu fikra sahihi sijui za nani!!??? Bado mnafikiri watanzania ni wa kudanganywa katika karne hii???
 
Hivi mnaogopa nini kupiga kura za wazi? Bunge lazima lipige kura ya wazi acheni upuuzi wenu hapa.
Muogope mbunge asiyetaka kujulikana wazi anasimamia nini.
 
Nawaambia MaCCM safari hii mmekamatika, Kwanza kama kutakuwa na Serikali ya Tanganyika, hata kama kwenye muungano, CCM itakuwa chama ya wapi??
Labda ndio maana mnaogopa Serikali tatu, hamkujipanga!!
CCM ni muungano wa AfroShirazi Party na TANU, kwenye Tanganyika na Zanzibari CCM inabaki wapi???
There will be one party for the two states, hapo ni giza!!
Hicho ni kitenda wili MaCCM watangangania every straw, lakini ni kuzama tuu!!
Kura ya wazi delaying tactic, vile vile itakwama tuu!!
Kufa kwa Nyani mitiyote uteleza!!
Ehee Mungu tuokoe na mafisadi wachawi na wauwaji wanaoliangamiza taifa letu MaCCM!!
 
Wewe tathimini unajidanganya mwenyewe, huwezi danganya mtu mwenye akili!!
Mpaka bungeni kuna vitufe vya kupiga kura, Kwa nini mnganganie kura za ndiyooo za chama yenu CCM??
 
Nakuomba utazame tena maandishi yako. Yametofautisha kura ya maamuzi ya Bunge na kura ya kumchagua mtu. Hilo ndilo jibu. Ni vitu viwili tofauti. Popote ulimwenguni, kura ya maamuzi ya Bunge ni ya wazi, na ya kumchagua mtu ni siri.

Kwanza unazungumzia Mabunge ya kawaida. Ni imani yangu kwamba hujui Bunge Maalumu la Kutunga Katiba nini maana yake. Ingekuwa tumefuata utaratibu mzuri wengi wa wanasiasa waliojazana huko wasingekuepo. Bunge la JMT na BLZ wangekua na uwakilishi tu siyo wote kujazwa ktk Bunge Maalumu na leo kutuvurugia malengo yetu!

Hata ktk Mabunge ya kawaida huko nchi za Magharibi utakua umeisha ona wanavyopiga kura kwa sababu mara nyingi wanaonyesha ktk Tv zao wakifanya hilo zoezi. Ama kwa kupiga kura ya siri kwa kutumia karatasi ama kutumia mashine maalumu zilizoko mezani kwao.
 
Najua siruhusiwi kuweka pua langu humu maana hayanihusu kama Mkenya, lakini kwa pitia zangu JF naona hili itabidi nilitamke tu hata kama mtaniponda. Jameni Wabongo, swala la katiba sio ushabiki wa chama wala jamii, bali ni jambo la wote na vizazi vijavyo. Kura ya siri ni muhimu sana maana inamfanya mhusika kufanya maamuzi kwa kauli zake mwenyewe bila kuogopa wadhamini wake. Katiba muitekeleze bila migawanyiko ya vyama ama tofauti za kimaslahi. Hapa kwetu Kenya tulihangaika sana na mwishowe tukakamilisha, ila kazi kubwa iliopo ni kutekeleza tulioyaandika humo.
Naomba msiniponde, mimi nilikua napita tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…