Sijivunii wazazi wangu

Maneno ya busara sana🤜🏽
 
Hakuna anayetaka kuwa masikini,

Pilika za kuyatafuta maisha Huwa zinachangamoto sana, uhai ndiyo fanikio la kwanza katika mapambano na mengine ni nyongeza.
 
( وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا ۚ إِمَّا يَبْلُغَنَّ عِندَكَ الْكِبَرَ أَحَدُهُمَا أَوْ كِلَاهُمَا فَلَا تَقُل لَّهُمَا أُفٍّ وَلَا تَنْهَرْهُمَا وَقُل لَّهُمَا قَوْلًا كَرِيمًا )

الإسراء (23) Al-Israa

Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima.

( وَاخْفِضْ لَهُمَا جَنَاحَ الذُّلِّ مِنَ الرَّحْمَةِ وَقُل رَّبِّ ارْحَمْهُمَا كَمَا رَبَّيَانِي صَغِيرًا )

الإسراء (24) Al-Israa

Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma. Na useme: Mola wangu Mlezi! Warehemu kama walivyo nilea utotoni.



Kma huelewi kiarabu ata icho kiswahili kinakutosha kuelewa
 
mkuu heshima ipo kwa wazazi wangu na nawapenda nilichokizungumzia juu ni hisia zangu za kutokujivunia wao.
 
Tunawapenda wazazi lkn katika eneo la utakosa baraka so kweli muhimu ni kutowadhalilisha nk
Watu wanashinda kuelewa, me sijasema siwaheshimu.... nawaheshimu sana na kuwapenda thats why unakuta najaribu kwenda nao hivihivi nina uhakika kwamba hata mimi ni mvumilivu sana pengine mwingine angeshawaropokea mbovu.
 
Hakuna anayetaka kuwa masikini,

Pilika za kuyatafuta maisha Huwa zinachangamoto sana, uhai ndiyo fanikio la kwanza katika mapambano na mengine ni nyongeza.
thank you man
 
Kuna watu wana mazito humu wakiyatoa ww utajiona cha mtoto. Basi tu humu tunatukanana, tunataniana, tunafurahi maisha yanakwenda.

Uzuri tukikaa humu JF tunakuwa kama wote tuko sawa kiuchumi, kijamii, kilevel na kiumri.

kuna wakati hatuna budi kukubali hali tuliyoikuta hususani kosa si lako. labda lingekuwa lako ungekuwa na nafasi ya kulirekebisha.
 
Kuna watu wana mazito humu wakiyatoa ww utajiona cha mtoto. Basi tu humu tunatukanana, tunataniana, tunafurahi maisha yanakwenda.

Uzuri tukikaa humu JF tunakuwa kama wote tuko sawa kiuchumi, kijamii, kilevel na kiumri.
kila mtu ana kiwango chake cha kumudu mambo mkuu, that's why kuna mtu anaweza kuua ili apate kitu fulani na mwingine hawezi, so mtu akieleza hisia zake don't compare with others.
 
kila mtu ana kiwango chake cha kumudu mambo mkuu, that's why kuna mtu anaweza kuua ili apate kitu fulani na mwingine hawezi, so mtu akieleza hisia zake don't compare with others.
Ni kweli, kuna wakati hatuna budi kukubali hali tuliyoikuta hususani kosa si lako. labda lingekuwa lako ungekuwa na nafasi ya kulirekebisha.
 
Pole sana mkuu, bora ya wewe wazazi wako wapo, ungekua kama yule kaka Samwel Mv Bukoba ambaye aliwapoteza wazazi wake wote wawili na yeye alikua mdogo hivyo hakua na taarifa muhimu juu ya wazazi wake zaidi ya kabila la wajita. Mpaka leo ni kijana mkubwa hajui ndugu yake yeyote humu duniani na hili linamuuma sana, mshukuru sana Mungu hata uwepo wa wazazi wako.
Point kubwa ni umeshajua madhaifu ya wazazi wako wewe wasamehe na kuwachukulia kua ni udhaifu wao. Endelea kuwasaidia pale unapopata nafasi.
 
Najivunia wazazi wangu, namshukuru Mungu kwa kunipa wazazi hao. Kama nilivyo na mapungufu mimi, na wao wana ya kwao, naheshimu maamuzi yao na jitihada zao, na kamwe siwezi kukosoa matakwa yao na mnana yao waliyonilea.

Asante Mungu kwa zawadi ya wazazi. Kwani wapo ambao walizaliwa hawakupata kuwaona wazazi wao kwa sababu moja au nyingine, walitamani ata kuwa na mtu wa kumiita baba au mama na hawakupata. Eeh Mwenye enzi Mungu uwape uzee usio na maradhi, na uwafanyie wepesi katika mwisho waa na mwisho uwape mwisho mwema. Amina.
 
🤜🤛
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…