Uchaguzi 2020 Sijui Gwajima atatumia Sabuni gani ya 'Kuwatakatisha' Waislamu wa Kawe 'aliowadhihaki' na 'Wakatoliki' waliokwazika naye 'alipomshambulia' Pengo

Waislam hatuwezi kumsamehe aliepanga kubadili misikiti yetu mitakatifu kuwa sunday school, wallah, tallahi sisi waislam hatuna unafiki wa kumsamehe mtu wa kaliba hii.
Huenda Pengo na waislamu walishamsamehe Gwajima hivyo hayo yameshapita, sasa tunaganga yajayo.

Kila laheri Askofu Gwajima na wagombea wengine wote.
 
Anajiita kiongozi wa kiroho tena lakini kinywa chake kimejaa matusi na kashfa. Ni huyu huyu Gwajima aliye mshambulia Makonda Tena kwa kutumia madhabahu. Ni huyu huyu Gwajima aliyetoa Matusi makubwa akimshutumu Kadinali Pengo Tena ambayo hayakustahili kutolewa na kiongozi yeyote wa dini.

Gwajima hafai tena ni mzushi, nilimuona baada ya kutoka polisi alipokuwa akihojiwa kwa kumtukana Kadinali Pengo, alijifanya kuwa na maumivu yaliyo mpelekea kutumia baiskeli ya miguu miwili, lakini siku moja akiwa mbele ya wafuasi wake alinyanyuka ghafla kwa madai kuwa Mungu wake amemuona akiwa katika mateso hivyo amempatia nguvu na kusimama kutoka kwenye kiti huku akitembea hata bila ya kuchechemea.

Huyu jamaa ana kinywa kichafu hafaii kuwa kiongozi.
 
Hahahahahahaha eti anatembelea wheelchair na kuinuka ghafla kwamba 'Mungu' wake kamfanyia miujiza.

Sent from my SM-N910W8 using JamiiForums mobile app
 
Hata msipo mpa kura zenu ngwajima atashinda malaika watabadilisha kura zenu bwana asifiwe kiongozi kwa imani analindwa na Mungu
 
Gwajima ni tapeli, haiwezekani kamwe kuichanganya dini na siasa hapa duniani, yani atoke kuongea propaganda kwenye mikutano ya kampeni halafu kesho yake aende kanisani kumtaja Mungu? hapana, huyu atakuwa anamtumikia mungu wa ulimwenguni sio aliyetuumba.
 
Kuhusu Gwajima na Makonda wala hata wakikunjana au wangekunjana mashati poa tu, wote wanatabia zinazofanana!
 
Nilivyoona heading nikajua ametukana tena.

Pengo alistahili kukabiliwa kwa kuwa alikuwa mnafiki. Alitumika sana kinafiki na serikali ya kina mkwere na Pinda

Khs Bashite ni wale wale tu.



JESUS IS LORD
 
Atakuwa anatumikia ubunge kwa kupitia kura za wizi, hivyo nayeye kama Askofu atakuwa ameshiriki wizi.
Askofu ataiba vipi? Ngwajima kashukiwa na roho mtakatifu akapewa kibali cha kuweza kuingia kwenye siasa aweze kuwapigania watu wa kawe
 
Tumnyime kura kabisa watu wa dini zote hatufai

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…