Uchaguzi 2020 Sijui Gwajima atatumia Sabuni gani ya 'Kuwatakatisha' Waislamu wa Kawe 'aliowadhihaki' na 'Wakatoliki' waliokwazika naye 'alipomshambulia' Pengo

GENTAMYCINE,

Ni kama Halima Mdee alivuowakashifu Askari Magereza pale Gereza la Ukonga kwamba, namnukuu,' MASIKINI WAKUBWA NYIE NDO MAANA MNAKAA KWENYE NYUMBA ZA BATI,' Huo ulikuwa ni ujumbe kwa Watanzania wote wakiwemo wana Kawe wanaokaa nyumba zilizoezekwa kwa bati kwamba ni masikini
 
Ngwajima ana mambo matano anapaswa ayajibu kabla hajaenda jukwaani angalau tupate nafasi ya kumsikiliza.
1....Ukabila alioonyesha kwenye Video yake
2....Kuwa na chuki na Waislam na wakatoliki
3....Kufanya mapenzi kiholela No care
4....Alituaminisha hataki nafasi Za kisiasa
5....Ubadhirifu kwenye taasisi anayoingoza
Tunajua amejiandaa sisi wapiga kura mtulishe maneno tukafanye yetu , Wajumbe walishamaliza
 
Wakatoliki hatuko na hiyo tabia.
Mimi ni voter wa Kawe. Nakuambia Gwajima hatapata kura za maana kutoka kwa wakatoliki na waislamu.
Hapo Magufail kafeli kweli kweli.

Na ulichokiandika hapa ndiyo Ukweli mtupu Mkuu japo najua kuwa wale 'Team Vichwa Ngumu' watakupinga na kukubishia. Kazi ipo Jimbo la Kawe.
 

Sijawahi Kukutana na JF Member 'Popoma' kama Wewe katika Historia yangu hapa. Madai ya Gwajima unaweza Kulinganisha na hili moja la Mdee?
 
Baraza la Walei na jumuiya zote za Kawe tayari wameshaanza kazi ya kuliuwa hili joka lililoigiza sinema ya matusi.

Kwa 'Wakatoliki' ninaowajua Mimi kwakuwa 'Wamenilea' pia Kiimani na Kiroho kama 'Mkatoliki' huyu Gwajima na CCM yake Kawe wameshatokota!!
 
Sina tatizo nae kivile japo tu hapo katika 'Kumshambulia' Kadinali Pengo Mkatoliki Mwenzangu 'amenikera' ila 'Waislamu' wa Kawe wana Hasira nae.
Wewe siyo mkatoliki, na kama ni mkatoliki basi ukatoliki wako brain washed.

Mimi ni mkatoliki, na wakatoliki wote wenye kufahamu mazambi na usaliti wa Kadinari Pengo kwa wakristo wa madhehebu yote ni kukiuka makubaliano waliyokubaliana maaskofu wa madhehebu yote kuhusu msimamo wa kanisa kutokubaliana na mahakama ya kadhi.

Kama alivyo kibaraka sheikh mkuu wa Dar ndivyo alivyo kibaraka Pengo.

Nina mashaka na ukatoliki wako kama ufahamu ni kwa nini jimbo kuu la Dar Papa alimteuwa Ruwaichi kuwa Askofu mwandamizi kabla ya huyu Pengo kustaafu.

Wanaojuwa protocol ya kanisa katoliki wanajuwa hapa naandika nini, ingekuwa ni serikali za kawaida Pengo angestaafishwa kwa manufaa ya umma, ila kwa mfumo wa Vatican ili kukustiri unaletewa Askofu mwandamizi na madaraka yote muhimu unakabidhi kwake. Endover powers.

Kwa kifupi point yangu kwa hili Wakatoliki na wakristo wote tulikuwa nyuma ya Gwajima na mpaka kesho namuunga mkono kwa hili, huyu ndio Mtanzania pekee aliyethubutu kumvaa Pengo na kumpa makavu live bila kupepesa.

Baada ya kifo cha Mkapa mtu pekee ambaye anaweza kumwambia kitu Magufuli na akasikiliza na kutekeleza ni Pengo peke yake.

Lisu ni Mkatoliki na Magufuli ni Mkatoliki aliwahi kuwapatanisha kupitia ushawishi wake?

Ninachofurahi mimi ccm ndio waasisi wa siasa za kidini, imekuwa ikiwaumiza wapinzani kwa kuwatumia viongozi uchwara wa dini, this time nao waonje radha ya udini.
 
Gwaji hatoshinda hilo jimbo, hata misukule yake inalijua hilo na ieleweke kwamba wale wajumbe waliomkataa hadi nafasi ya3 ndio hao waislam na wakatoliki watakaomnyima ubunge.
 
Pengo alikuwa Askofu mkuu wa jimbo la Dsm, madaraka yake ni ndani ya jimbo lake la Dsm tu, maana hapa kuna kaharufu ka kupotosha watu.

Kila Askofu wa jimbo ni mkuu kwenye jimbo lake, hakuna kiongozi mkuu wa Wakatoliki wote Tanzania nzima, hakuna.
 
Hizi hasira nadhani ni za kufikirika zikizowekwa kwenye makundi ya kidini.

Ni wachache wanaokumbuka hayo hususan wana Kawe.

Ni dhahiri kuwa Chama Cha Mapinduzi kina watu wa kika aina mpaka wasiokuwa dhehebu kama kina kingunge RIP.

Chama Cha Mapinduzi ni dhahiri kuwa wamejiridhisha na kuona Mchungaji anafit vizuri kwenye nafasi hiyo.

Sina shaka na mikakati ya ushindi ya Chama Cha Mapinduzi hapo KAWE. Ifahamike kamwe CCM haiwezi vumilia sehemu wanapokaa viongozi waheshimiwa na Rais mstaafu iende upinzani. By hook, or by croock ushindi ni lazima.
 
Mimi si Mkatoliki ila wakatoliki wengi wana misimamo thabiti linapokuja suala la kashfa na dharau kwa viongozi wao
Mimi ni Mkatoliki, wakatoliki tulio wengi tuliokuwa hatupendezwi na uhuni wa Pengo kuligeuza kanisa kama sehemu ya jumuiya za ccm tulikuwa na tunaendelea kusisitiza Gwajima alikuwa sahihi kwa 100%

Issue ya Mahakama ya kadhi ni hatari kwa nchi yetu na ccm ilikuwa inawatumia mawakala wake kama huyu Pengo kubaliki vitu vya hovyo ambavyo vilikataliwa kwenye mkutano wa pamoja wa maaskofu.

Kwa hili tuache propaganda uchwara, wanaotaka kumuhukumu Gwajima kwa hili la Pengo wamuhukumu kwa haki na watafute sababu, mkumbuke Magufuli ni mkatoliki na anamuheshimu sana Pengo, anajuwa vyema Pengo ndio mkosefu katika hili na atuombe radhi wakristo wote kabla hajafa, huyu mzee ni msaliti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…