NGOJA NIKUANDIKIE VIZURI BROTHER.
Nilikua nae kwa muda wa miaka mitatu hadi sasa, na tumebahatika kupata mtoto mmoja wakiume.
Amewahi kuondoka na kurudi kwao mara mbili na hii mara ya tatu na kibaya zaidi hataki kupokea simu yangu na ananitusi kwenye meseji kila nikitaka kumujulia mtoto hali.
Mara ya kwanza alivyoondoka alikuta meseji kutoka kwa mwanamke kwenye simu yangu. Alichukua simu aina ya Samsung akaondoka nayo na nilivyo muuliza aliniambia kwamba kuna mmasai alimpa dawa ya uzazi lakini hakumlipa hela shilingi elfu 5 kwahiyo ameichukua kama malipo.
Kesho yake nimerudi nyumbani kula, nikakuta amefunga mlango na kufuli, na ufunguo upo kwa majirani. Nilipojaribu kumpigia simu yake ikawa haipatikani na nilipowapigia nyumbani kwao (ukweni) wakasema wao hawana taarifa na alipo.
Nilikaa mwezi mmoja, nikaamua kumfuata kwao, na tukaishi kwa amani kwa muda mfupi ila tena matusi yakaanza. Alikua analalamika akisema sipendi watoto, sipendi yeye azae.
Niliamua twende hospital kwa wataalam wa uzazi, wakamfanyia vipimo na kumkuta ana retlovated uterus ila Dokta akasema haina shida yoyote.
Mwaka mmoja kabla ya kuanza hivi vituko aliwahi kubeba mimba ikafikisha miezi mitatu ikatoka kwa bahati mbaya (miscarriage). Daktari alisema sio kawaida mimba ijitunge nje ya uterus, na ndivyo ilivotokea kwa mke wangu.
Baada ya hiki kisa ndio matatizo na ugomvi na mke wangu ulipoanza.
Mara ya pili alivyoondoka, ni baada ya mimi kuchelewa kurudi kutoka kazini kwangu (hospital). Safari hii aliondoka na pesa kidogo tuliokua tumeweka kama akiba, na aliondoka akidai nachelewa kurudi nyumbani nilikua kwa wanawake wengine. Mimi nafanya kazi ya uuguzi katoka hospital xxx ambapo najitolea ili nipate ujuzi, iwe rahisi kupata ajira hapo baadae.
Aliondoka akiwa na ujauzito wa miezi minne, na nilimfuata baada ya miezi mitatu, muda huo ujauzito ukiwa umetimiza miezi saba.
Muda wa kujifungua ulipofika, alijifungua salama kwa njia ya operation. Ila hii haikuepusha visa na ugomvi wetu, kwani viliendelea vile vile kama zamani.
Mara ya tatu kuondoka, ilikua siku ambayo nimetoka kazini, na nilirudi nyumbani saa tatu usiku nikiwa na sabuni ya unga ya kufulia lita 10. Ile kufika, nikapokelewa na matusi nikidaiwa nimetoka kwa wanawake na akaniomba nauli kesho asubuhi arudi kwao. Kipindi iko mtoto wetu ana umri wa miezi mitatu tu.
Niliona ni busara nikiongea na Mama Mkwe kwenye simu na kumueleza kila kitu, nae akaongea na mwanae akamsihi abaki, na kweli yakaisha.
Ila baada ya wiki, nilikua nimemuachia shilingi elfu therathini, huku mi nikiwa sijabakiwa na pesa yoyote. Nilipotaka kuchukua kiasi kidogo nikatumie nikakuta pale tunapotunza pesa sioni kitu, nikamuuliza akasema ile pesa ametumia kununua begi la nguo la mtoto. Nikapiga moyo konde.
Siku hiyo hiyo jioni nilivorudi kazini, akaniambia amechoka kukaa hapo anaomba nauli arudi kwao. Nikamuambia kwa sasa sina hela, nipe muda kidogo nitafute ila akakataa. Nikamwambia basi chukua kitu kimoja Kati PC, Subwoofer au TV uuze upate nauli.
Nikiwa kazini, nikapata taarifa kua anahamisha vituvyote vya ndani. Nikawahi kurudi, ila tukasuruhishwa na wazazi. Yakaisha.
Akaniomba nauli, nikampa elfu arobaini akakataa kwa kusema haitoshi ingawaje nauli kwenda kwao ni shilingi elfu kumi na tano tu. Nikamuuliza kuhusu ile pesa tuliokua tunatunza yeye akasema atanunulia begi la mtoto, akasema ilikua shilingi elfu kumi na tano tu, tena mbele ya wazazi.
MWISHO WA KUREKEBISHA
Ila mwamba unapitia magumu aisee. Hapo hamna mke hapo piga chini bora nyeto.