Sijui kama siku hizi zipo hizi

Kutupa barua ktk kijiji/mji husika wakati unapita na gari/treni na inafika kwa mlengwa.

mkuu pokea LIKE, umekumbusha enzi hizo, enzi za kupiga simu kupitia kwa operator wa ttcl akuunganishe kwa ndg/rafiki yako.
 
Kutahiriwa kwa babu kienyeji kwa wembe au kisu kidogo kikali hakuna cha ganzi wala nini!
 
Kuvaa chilimeni siku za siku kuu.(Hii sizani kama viajana wa sasa wanaijua)
 
mzee hizo red zilihusika sanakwa upande wangu.
  • kulilia nguo za sikukuu
  • kutoroka shule kwenda kwenye maembe
  • kudefine what is history kila morning speech,nk.
  • kusoma kitabu kimoja cha Mr Daudi watu zaid ya 10
  • kamali ya chelewa+wizi wa mifagio
 
Ukiwa unaenda shue miguu michafu unajiosha kwa umande (unapita kwenye nyasi zenye maji maji yale ya asubuhi).
 
Kuendesha magari yaliyotengenezwa kwa maboksi huku ukiunguruma kama injini pamoja na kupiga lesi wewe mwenyewe.
 
Na hii ya kulala na nguo mpya au viatu vipya mnaikumbuka wanajamii?
 
kunya bila kutawaza alafu mwisho wa siku kaptula zote zinakua na ukoko wa kinyeeeeeesi katkat
 
Kudandia magari, kukaa road msimu wa mvua ili kusubiri gari ikwame msukume mpate pesa, watu wazima kutembea road wamening'iniza rundo la funguo kwenye luksi, kuogelea kwenye vidimbwi, kukopa kacholi xul kwa ticha, kucheki tv dirishani kwa watu coz mtaa mzima tv adimu, vibiriti vyenye picha za mastelingi wa kihindi, kufuga samaki aka gapi,black,zebra. Kukata ndala matairi ya magari, kubeba vibegi vya spoti, kunywa uji wa mchele au maharage msibani, kupanda chaimaharage, dah siezi maliza yote.
 
Mmetisha wana jf ila bado kubeba madaftari mengi darasa la saba ili uonekane msomi!
 
Dah nimeheka sana jf noma
Kuweka shati la shule Jv ya vidonda kwa kuwa huna hela ya kununulia blue
Kutemea mate embe bichi ili mwenzio asikuombe
Kuvaa saa za discolight halafu ikipiga mziki mnacheza darasani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…