Sijui kwanini huwa simuelewi Vanessa Mdee?

[emoji38][emoji38]ukipenda usipopendwa,, tafuta KISELA ya Vanessa ndio utamwelewa anachofanya.
 
Hata "No body but me" huujui?
 
Mwenyewe huwa simuelewi nyimbo zake na huwa hazi hit ka za kina nandy na Maua Sama
 
sio kila nyimbo ni kwa ajili ya kutoa ujumbe nyingine ni za kuburudisha
 
Kwa hii Africa bado sijaona Msanii wa kike wa kumshinda Vanessa mbele ya Camera...sio Tiwa Savage, Yemi Alade au yeyote yule...Vanessa is the great japo watu wanam-underrate huyu Dada ila huko kwa Wenzetu wanamheshimu na kumuogopa kama ule ugonjwa wa "ukoma".
 
Suala la kazi za sanaa na tafsiri zake pamoja na kupata hisia ni tata sana.Ili kazi ya mtu kukubalika kuna vigezo vingi vinavyotofautiana vionjo toka mtu mmoja hadi mwingine.Hivyo, si kweli kuwa maudhui pekde ndiyo hufanya watu kupenda mziki.

Tazama watanzania, wengi hatujui Kilingala, lakin unaona jinsi mziki wa Kongo ulivyotukamata? Kuanzia wakongwe Franco, Lutumba, Papa Wemba mpaka kizazi kipya Ipupa na Feregora.Watanzania wangapi tunaelewa kisemwacho na hawa watu?Leo hii mimi Mhenga, nikisikia Yekeyeke ya Mori Kante naruka hadi boxer inaporomoka, sijui lolote lisemwalo humo.

Hivyo, wew sema hujapenda kazi ya huyo binti, na hilo unaweza usiwe na sababu maana kupenda na kuchukia havina sayansi sana.Inatokea tu.

Love doesn't ask why (Celine Dion)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…