Sijui kwanini nimeumia hivi

Nilivyokua nasoma nilikua nahisi kuna kibaya kimewakuta hospitalini kumbe alipona mtoto na kuruhusiwa, nimeshukuru kwa hilo.

My dear binadamu hatuma wema, binadamu ni wasahaulifu, binadamu tuna wivu na tuna visasi.
Huwezi jua kuna kitu hakikuwa sawa kati yenu mlivyokuwa mnasoma akaweka chuki nawe na alipopata nafasi ya wewe nawe kuumia akaitumia, ni dhana tu lakini.

Yote ya yote jana imepita achana nayo tungojee kesho.
 
Misaada ya kujitoa kwa kujiteketeza mara nyingi huambatana na maumivi.
Ni mara chache mno mtoa msaada wa kujiteketeza akapewa shukran aliyoitegemea toka kwa msaidiwa.

Saidia kile una uwezo nacho, sipendi kujitoa kumsaidia mtu end of the day nikaja kuumia kama hivyo.

Unamsaidia kumbe anakudanganya, msaada wako anautumia kinamna nyingine tofauti na alivyokuomba.
 
Wanaitwa ENTITLED KIDS walifundishwa kuwa ni haki yao kupewa kika kitu walichoomba badala ya ni hisani.

Hivyo kushukuru inakuwa nadra
 
umefanya ukarimu kwa tendo la huruma la kipekee sana mkuu,

usiumie sana, ndivyo walimwengu tulivyo.
angekukumbuka zaidi, kama ungemtumia muamala kwenye simu au ungempa cash mkononi.

wema wako umekuponza,

kujitolea muda, fedha na hasara ambayo ungeipata kazini kwako kabisa hajaithamini πŸ’

Tenda wema uende Zako..
Kwa Neema na Baraka za Mungu, wema na ukarimu wako Mungu ameuona πŸ’
 
Ni jambo jema sana.. Nimejifunza in a hard way
Kila binadamu anapenda appreciation pale anapofanya jambo jema. Ila sasa sisi sisi binadamu pia ni very complex creatures, tuna tabia na malezi/makuzi tofauti tofauti pia.

Ndio ukubwa huo mama, tunajifunza kila siku.
 
Kwakweli nashukuru Mungu kwa hilo pia
 
kwakweli nimeliona hilo, nimejifunza kitu kikubwa sana
 
Ukieza kuhandle hizo reaction automatically na huruma inapungua tukio la huyo mate wake limempa introduction tu ya jinsi binadamu walivyo
Huruma isipungue bhana , unajua msaidie mtu kama umeguswa na anayo yapitia kwa kujipa amani yako ww mwenyewe kwa kuona angalau ule ugumu kwa huyo mtu umepungua , bila kuweka matarajio ya malipo ya aina yoyote kutoka kwa yule mtu , matarajio ndio yana waumiza watu pale yanapokwenda kinyume .
 
AmenπŸ™
 

Binafsi nimefurahi.

Sikujua kumbe na nyie wanawake mnaumiaga mkifanywa chuma ulete.

Mwanaume akija kulalamika humu kafanywa chuma ulete na mdada, mnamponda mwanaume kuwa hana hela, wanaume wa jf tunanalalamika sana, tunakimbia majukumu, tule kwa jasho etc , mnamtetea mdada aliemchuna uyo mwanaume.

Itabidi mjue how it feels like, mtu ukijua kwamba ulikuwa used.

Ndo mpate taste ya sisi wanaume tunavojisikia Leejay49 Mrs Van
 
Kila binadamu anapenda appreciation pale anapofanya jambo jema. Ila sasa sisi sisi binadamu pia ni very complex creatures, tuna tabia na malezi/makuzi tofauti tofauti pia.

Ndio ukubwa huo mama, tunajifunza kila siku.
Ni kweli, ila walau nimepata ahueni baada ya kusoma comments zenu.. Mbarikiwe sana
 
AmenπŸ™πŸ™.. Nitafanya hivyo nikipata nafasi, Barikiwa sana mkuu
Pia nataka nikuambie Leejay49 unajisikia vibaya ni kibinadamu tu,lakini wewe mbele za MUNGU umeshinda kwa tukio hili. Ni jaribu kwako,kipimo chako. Hiyo ni sadaka kubwa. Kuanzia muda wako,gharama zako. Hujapoteza bure.
Mbele za MUNGU umetoa sadaka kubwa. MUNGU ana maajabu yake.
Kitu kizuri utalipwa siku ambayo wewe hukuitarajia,niamini. Utatendewa kitu ambacho wewe hujui kimekujaje.

Hujui tu MUNGU alikuhifadhi maalumu kwa ajili ya kumuokoa huyo mtoto. Achana na mamaake,wewe muwazie yule mtoto jinsi ulivyomuokoa. Tena nataka nikuambie usingefanya Jambo baada ya kuambiwa,na kuona hali ya yule mtoto,angekufa. Hapo ndio ungejisikia vibaya mara mbili ya pain unayoipitia sasa.

Ndio maana MUNGU anazidi kuangalia uvumilivu wako kupitia kukuruka wewe. Kwa mawazo ya kibinadamu unaweza kuliona la kawaida,lakini ukiliwazia hata kidogo linaonekana wazi kabisa ni la ajabu. Umeshinda
 
Ila nimeumia mkuu.. Hajanipigia hadi saizi bado
Na hata kupigia nakuambia,Akipiga atakuja na excuse ya kitoto kweli.Ndivyo walivyo.

Atakuweka karibu akiwa na tatizo tena trust me.

Wewe ni daraja,Kuwa daraja ni kazi sana
Binafsi Nime deal na watu wa hivyo wengi mno.Nilipopata somo kwama mimi ni daraja nikaona.Ila nimepumguza huruma.Sababu mtu wa hivyo hata siku ukiwa na shida ya mia mbili hutaipata kwake.
 
Amen πŸ™πŸ™.. Hakika nimejiskia vizuri baada ya kusoma maneno yako mkuu.. ubarikiwe sana kwa hekima hizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…