Sijui kwanini nimeumia hivi

Pole sana mkuu,mi nakuelewa huwa inauma kweli sio kwamba ulitaka akulipe chochote lakini kibinadamu mtu aliekutendea mema inapaswa umshukuru. Hasa ukizingatia wewe sio baba wa mtoto wala ndugu yake. Hatumuombei shida lakini bado ana mengi yanayomkabili duniani hakupaswa kufanya huu ujinga. Kama aliweza kuscreenshot meseji za wengine na kupost,alishindwa nini kupiga simu ya kuaga kwamba anatoka hospitali. Mi nakushauri mpigie au mtumie meseji mwambie nimesikia umetoka hospitali,nafurahi kujua hilo, Msalimie mtoto
 
Pole sana mkuu ila kubali au ukatae huyo rafiki ako ana kitu rohoni mwake juu yako. Angeshindwa kukupost bas hata sim ya taarifa tu kuwa hospital wamesharuhusiwa ili usihangaike tena kuwafuata huko napo ameshindwa.

Huyo ni wale marafiki ambao unamsaidia alafu anakuona kama unajipendekeza au kama unajifanya una hela sana wanakuaga na roho za wivu mbaya sana. Usishangae hata anakukalia kitako huyu anakusema vibaya kwa watu, ni kawaida yao anaona wewe una kaz ye hana bas anajikuta kama we ndo mwanga wake hawez kukushukuru hata siku moja.

NB. Kaa nae mbali usipige tena sim wala sms ili siku akipata shida tena ashindwe jins ya kukuanza.
 
Kama unamsaidia mtu do it for good and for godsake, maana yeye ndiye analipa yote.

Pole sana.
 
Hapa duniani watu watenda mema huishia kuumia au kuumizwa tena huumizwa na watu wao wakaribu! Yani kwa tafsiri ya dunia watu watenda mema au wanao watendea mema wengine huonekana na kuchukuliwa watu dhaifu ila watenda mabaya na wanao tendea watu mabaya huonekana ni strong sana!

Ndugu Kanuni za dunia zinawakataa kabisa na zinakataa kabisa watu wanaotenda mema ndio maana wengi huishia kuumia na kuumizwa tena na walio watendea mema….

Dunia ni kama inahitaji watu makatili wasiojali na wenye roho ya kutu na ndio asilimia kubwa wana furahia maisha …kama unabisha kawatafute watu unaowajua ni wema halafu kawaulize idadi na walivyo na maumivu tena ya watu wao wa karibu

Dunia hii inawafanya watu na inafundisha watu kutotenda au kutotendea watu mema maana asilimia kubwa waliotenda au kuwatendea watu wema waliishia kuumizwa…pole sana hakika dunia sio sehemu salama kabisa kwa watu wanaowatendea mema wengine….

Pole sana usiache kuwatendea mema wengine na wala usitende mema ukitegemea jambo jema bali iwe ni part and parcel of your life….

Pole sana Mkuu dunia haina huruma uwezi amini kuna mtu nimetoka kumsaidia muda huu sasa najiuliza na mimi nitaumia au lah?

Ukipata muda soma hiki kitabu “who will cry when you die”
 

Attachments

Yaani nashindwa kueleza ninavyojiskia,, sihitaji anilipe chochote wala chochote ila tu nimeumia ndomana najishangaa kwanini inakua hivi hadi nashindwa kujizuia.. Hata sielewi naumia nini yani
Kwa mtindo wako huu wa kutendea watu wema na kuhakikishia utakufa mapema kwa maumivu ya moyo kabisa!
Dunia haitaki kabisa watu wema kama wewe utachofaidi hapa duniani ni maumivu tuu…
Pole sana
 
Wanaume wakilalamika masingo maza sio watu muwe mnaelewa. Fikiri hapo ungemsomeshea na kumlelea mwanae alafu mwisho wa siku anakuja kuchukuliwa na baba wa mtoto kirahisi tu na wewe kupewa maneno ya kuuudhi. Singo maza is a no go zone chapa sepa
 
Nadhani tabia yake mbaya Haina uhusiano na usingle mama wake.

Kuna watu kwa asili tu hawanaga shukrani.

Msamehe tu,kisha endelea na mambo yako.

Usimtafute tena.
Mbona wengine kuwashukuru ila main character katupa mbali
 
Wanaume wakilalamika masingo maza sio watu muwe mnaelewa. Fikiri hapo ungemsomeshea na kumlelea mwanae alafu mwisho wa siku anakuja kuchukuliwa na baba wa mtoto kirahisi tu na wewe kupewa maneno ya kuuudhi. Singo maza is a no go zone chapa sepa
Kwakweli nimeliona hilo
 
Kwa mtindo wako huu wa kutendea watu wema na kuhakikishia utakufa mapema kwa maumivu ya moyo kabisa!
Dunia haitaki kabisa watu wema kama wewe utachofaidi hapa duniani ni maumivu tuu…
Pole sana
Duuh🤔🤔😔
 
Asante kwa ushauri mzuri mkuu, barikiwa sana🙏🙏
 
Kwakweli nitafanya hivyo.. Mungu tu awasaidie waendelee kuwa salama ila sitowatafuta tena
 
Labda kweli
 
Amen, Nimejifunza kitu
 
Nimeumia sana mkuu, ameshindwa kunishukuru basi hata angenipigia Simu anijulishe kama wanaendelea vizuri.. Nimeumia haki ya Mungu tena[emoji3064]
Pole sana, tenda wema nenda zako usingoje shukrani.....kuna siku atakutafuta tena akiwa na shida.....for now mshukuru Mungu tu kwamba hela za wazazi wako hazikwenda bure mtoto alipona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…