Sijui kwanini nimeumia hivi

Pole sana! Umeshamjua, achana naye, ikibidi waeleze Mama na dada yako kama njia ya kujipa ahueni kwa kutendwa, ila huyo mtu msahau!
 
Siku zote ishi kwa kusaidia bila kutegemea malipo yeyote. Iwe ya shukrani ama chochote.

Kwa sababu hata shukrani isingekuongezea chochote.
Unaweza kusema shukran haiongezi chochote, ila si kwa kutumiwa vibaya kiasi hiki. Shukran inampa mtu faraja!
 


Ndugu yangu Mimi ni Mkarimu sana, ila sasa nimekuwa mbaya zaidi ya Mnyama, kuna Mdada alikuwa mke wa rafiki yangu, aka paralyse, akiwa katika hali hiyo, nikampalaki 8, kumbe lishamtelekeza rafiki yangu, akaenda kwao kijijini na alishakufa.

Kuna sababu kwa nini watu huwa wana shida, nakueleza ukweli mimi naweza enda mahali nikasaidia mtu nisiyemjua kiasi kikubwa cha hela, ila ni ngumu SANA saidia mtu ataayekuja nililia shida.
 
Nimejifunza kitu aisee.. Nitaanza kua na roho mbaya na mimi
 
Pole sana! Umeshamjua, achana naye, ikibidi waeleze Mama na dada yako kama njia ya kujipa ahueni kwa kutendwa, ila huyo mtu msahau!
Nilishafaya hivyo mkuu.. Niko good now
 
Asante mkuu, siku nyingine ukipita Bombambili uje tupige stori huko naogopa wanajeshi😃😃😃
 
Duuh, kwakweli
 
Barikiwa sana mkuu, Umenena vyema
 
Iliwahi kunitokea nashukuru nilisahau hata alivonitafuta miezi saba badae sikuwa na kinyongo naye


NB single mom hawasaidiwagi
Nimejifunza mkuu, barikiwa sana
 
Duuh 🤔
 
Ubinadamu kazi my dear

And it's okay moyo kukuuma

Lakini usiruhusu kuumia sana

Take it easy, umefanya kwa nafasi yako kadri ulivoweza

Mengine mwachie yeye na Mungu wake watajuana wenyewe
Namshukuru Mungu niko good saizi
 
Kaa kimyaaa kama vile hakuna kitu kilitokea.
Nakurudia tena,kaa kimya mdogo wangu.
Kaa kimya kuna jibu linakujaa.
We kaa kimya tuu na usisimulie saana kwa watu.
 
Kinacho uma ni vile hâta kutambua msaada wako. Anawashukuru wengine na anakuacha wewe. Hama huo mtaa mkimbie na Blocks juu
 
Bora wewe mtu baking, mi niliwahi uguza bamkwe katokea kijijini singida nimempambania tezi dume tena hakua hata na Bima.
Nilitoboka kisawasawa na madeni juu niliingia.
Alivyoruhusiwa hosi akarudi kwao singida hata asiniage, yaani alimuaga bintiye tu akamwambia ataniagia. Kumbuka kafikia kwangu kila siku tunaonana.
Niko zangu job ndio natumiwa message wasap mzee anakuaga anaondoka.
Sikujibu wala nini, nilipotezea ila kwakweli niliumia.
 
Hilo ndo kubwa zaidi mkuu.. Pole sana aisee
 
Kaa kimyaaa kama vile hakuna kitu kilitokea.
Nakurudia tena,kaa kimya mdogo wangu.
Kaa kimya kuna jibu linakujaa.
We kaa kimya tuu na usisimulie saana kwa watu.
Nashukuru lilipita mkuu, niko vizuri saizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…