Sijui kwanini nimeumia hivi

Sijui kwanini nimeumia hivi

Binadamu muda mwingine ni shida tu mshukuru Mungu umekuwa sehemu ya kukojoa maisha ya mtoto wake shida haziishi. Mie niliwahi kumtafutia kazi rafikinyangu kwenye kampuni nayofanyia kazi na alikuwa kwenye wakati mgumu yeye na familia yake lakini baada kupata akaanza kunipiga majungu kwa maboss nikaishia kupoteza
Pole sana huruma muda mwingine inaponza mumgu akutie nguvu
 
Huyo anatakiwa ajifunze kwa maumivu, next time akikosa msaada atajifunza kitu.

Mimi wiki iliyopita nadhani j4 ilinikumba ishu kama hii, nikamsaidia ili aende hospital nikakaa j5 nikampigia 2 times na sms juu kujua hali yake inaendeleaje lakini mpaka navyotype hapa hakuna response yeyote. Hiyo j5 alipost status ya bday party, simwambii kitu na wala simuombei shida ili anitafute tena ila nimenawa mikono tutabaki kuheshimiana tu.
Duuh🤔🤔
 
Habari za asubuhi wana JF,

Iko hivi, nina rafiki yangu ana mtoto (naweza nikasema ni single mom) ila isieleweke vibaya, nilisomaga nae O level huko ila nikama bahati tu tumejikuta tunaishi tena mtaa mmoja.

Ijumaa jioni wakati natoka tu ofisini alinipigia Simu akaniambia anashida kama naweza nipitie nyumbani kwao nikamuone, kwakua nilikua sina ratiba nyingine nikasema isiwe tabu kabla sijafika nyumbani nikapitia.

Nilimkuta yuko good ila mwanaye alikua anaumwa sana ile mtoto kazidiwa na akaniambia ameshindwa kwenda hospitali hana hela na almost kila aliyempigia simu wamemuahidi tu tangu asubuhi na hakuna aliyemtumia mpaka muda huo sa 1 jioni inaelekea saa 2.

Kiukweli sikua na hela and i was totally broke, yaani wiki ile iliyoisha mwenyewe nimeishi tu kwasababu nina wazazi maana nilikua nina mambo mengi yananihitaji hela kiasi kwamba sikua nimebakiwa na hata Mia mbovu. Lakini nikasema kwenye suala la kuokoa maisha ya mtoto isiwe kesi nikamwambia ngoja nirudi kwanza nyumbani, nikamsimulia mama tukaongea na dada yangu wakasema tu hapa kwa harakaharaka hatuna namna tumdanganye tu mzee kitu chochote jioni hii atupe hela, kweli mzee bila hiyana tukamshawishi akanipa 150k nikamfata kwao tukaenda hospitali usiku uleule.

Mtoto akapewa huduma ya kwanza na baadhi ya vipimo wakamlaza ili asubuhi aendelee na matibabu mengine (muda wote huo anawapigia ndugu zake wakiwemo na baba wa mtoto hata simu hawampokelei wengine), asubuhi yake niliomba tu ruhusa kazini nikawaambia nitachelewa ili nione mtoto atakua anaendeleaje.

Case ya mtoto ikawa kubwa wakasema tuende nae hospitali nyingine kubwa (Peramiho nadhani watu wa songea wanaijua), kuna vipimo alivyoambiwa wampime vilikua vinahitaji hela almost kama laki 2 tena nikamwambia mama akanitumia tukafanikisha. Kwasababu kazini nilikua wanapigapiga sana simu na nikaona wanaendelea vizuri na mama yake alikua ashafika nikamwambia naenda ofisini incase kimetokea chochote utatuambia nikampa na namba ya mama kama mimi nisipopokea ampigie, nikaondoka. The bad thing is nilikua busy busy sana hadi siku ikaisha sikuwatafuta tena.

Kinachoniumiza ni kwamba, jana mchana nilimpigia simu hakupokea nikaenda kwao sikukuta mtu, nikaenda hadi Peramiho tena kulivyo mbali nikaambiwa wameruhusiwa na hakunipa taarifa. Kuanzia jioni nimeingia WhatsApp naona ameweka status nyingi nyingi kufungua nikawa naona amescreenshot miamala yote ya watu waliokua wanamtuma hela na kuwapa credits Mungu awabariki sana kwa kuokoa maisha ya mwanae maana alikua kwenye hali mbaya sana na nini nini. Screenshot kama kumi hivi na kitu na amewataja na majina kabisa...

Cha ajabu hiyo miamala hakuna hata wa mtu mmoja uliofikia hata 30k, wote ni hizo hizo tu efu10 ef5 ef7, kawaandikia macaption mazito mazito. Nimebaki najiuliza mbona alikua ananiambia hawapokei simu, na hela inaonekana walimtumia siku ileile ambayo aliniambja na mimi niende kwake kumuona.

Mimi ambayo nilikua nae kuanzia siku ile hadi usiku nikaacha na kwenda kazini na tumeclear bills zote hata asante hajaniambia na wala taarifa kama wameruhusiwa hajanipa. Nimesubiri jana yote hadi leo saizi hajanipigia hata simu, Kina mama wananiuliza wanaendeaje nawaambia tu wanaendelea vizuri huku roho inauma.

Nimetenda wema nimeenda zangu wakuu, lakini bado roho inaniuma aisee😥😥
Kaka one day atakuja2
 
Nimeumia sana mkuu, ameshindwa kunishukuru basi hata angenipigia Simu anijulishe kama wanaendelea vizuri.. Nimeumia haki ya Mungu tena🥺
Pole Lee, kiukweli kuumizwa na hilo ni haki yako maana linaumiza.

Umia halafu jipe muda utapona. Lakini wakati unaumia chukua huo muda kumpigia simu na kumuuliza imekuwajee. Maana inawezekana alitenga muda wa kuwashukuru akakumbuka tu miamala akasahau keshi

Au alikuweka wa mwishoo kiitifaki ili aje aweke status kuubwa ya ma rangirangi.

Au anasubiria ukawatembelee apige picha mkiwa wote afu ndo aseme. Huyu ndiye amekuwa zaidi ya ndugu maana yupo hapa pamoja nami.

Mpigie/mtembelee halafu mueleze hisia(mwanamke to mwanamke) zako naye ataeleza majibu yake
 
Mkuu kwa jinsi alivyo atarudi tu,, maana hij ni mara ya pili namsaidia halafu inatokea vilevile.. Sijui hata natakiwa kufanya nini, ila ngoja nimpigie kwanza simu nitarudi
Usipigie simu achana huyo ndo tabia huwezi badilisha kitu songa jitenge nae hana upendo na wewe .ila ana upendo akiwa na shida tu
 
Jamani wewe😃😃
siku nyingine akija muonyeshe ukatili.
kuna single mom alinitapeli elfu 30, akanitapeli tena laki 1. siku moja bwana akapata ajali akavunjika pua. mamaye hana hata hela ya hospital. kapiga simu, akatuma mpaka video akiwa hosp kweli ukiangalia kavunjika.
anaomba msaada nimsaidie huku analia. hana hela ku clear bill. mm nilimwambia atafute hela alizonitapeli azitumie kulipa bill. alimpa mpaka mdogo wake simu anibembeleze mm nimeweka ngumu. nadhani walisema huyu mmeru ni mtoa roho
 
Pole Lee, kiukweli kuumizwa na hilo ni haki yako maana linaumiza.

Umia halafu jipe muda utapona. Lakini wakati unaumia chukua huo muda kumpigia simu na kumuuliza imekuwajee. Maana inawezekana alitenga muda wa kuwashukuru akakumbuka tu miamala akasahau keshi

Au alikuweka wa mwishoo kiitifaki ili aje aweke status kuubwa ya ma rangirangi.

Au anasubiria ukawatembelee apige picha mkiwa wote afu ndo aseme. Huyu ndiye amekuwa zaidi ya ndugu maana yupo hapa pamoja nami.

Mpigie/mtembelee halafu mueleze hisia(mwanamke to mwanamke) zako naye ataeleza majibu yake
Nitafanya hivyo nikipata mda wa kwenda kwao.. Maana kwenye simu nahisi haitakua sawa
 
siku nyingine akija muonyeshe ukatili.
kuna single mom alinitapeli elfu 30, akanitapeli tena laki 1. siku moja bwana akapata ajali akavunjika pua. mamaye hana hata hela ya hospital. kapiga simu, akatuma mpaka video akiwa hosp kweli ukiangalia kavunjika.
anaomba msaada nimsaidie huku analia. hana hela ku clear bill. mm nilimwambia atafute hela alizonitapeli azitumie kulipa bill. alimpa mpaka mdogo wake simu anibembeleze mm nimeweka ngumu. nadhani walisema huyu mmeru ni mtoa roho
Mungu anakuona mkuu😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom