Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umefanya vyema kutenda wema na kwenda zako, jitahidi tu usiumie roho.Nimetenda wema nimeenda zangu wakuu, lakini bado roho inaniuma aisee😥😥
Ndio hivyo alafu mtu kama huyu anakuja kukutafuta analalamika umemtenga, humsaidii kwa chochote.Duuh🤔🤔
Dah ila wanaume tunahuruma sana na hawa viumbe sema nao kwakujitoa ufahamu sifuri. Yan anashindwa kutoa tu taarifa kuwa kapata huduma na kuongeza maneno mawili matatu ya ukweli au uongoò???Huyo anatakiwa ajifunze kwa maumivu, next time akikosa msaada atajifunza kitu.
Mimi wiki iliyopita nadhani j4 ilinikumba ishu kama hii, nikamsaidia ili aende hospital nikakaa j5 nikampigia 2 times na sms juu kujua hali yake inaendeleaje lakini mpaka navyotype hapa hakuna response yeyote. Hiyo j5 alipost status ya bday party, simwambii kitu na wala simuombei shida ili anitafute tena ila nimenawa mikono tutabaki kuheshimiana tu.
Kwakweli, Bora wewe ulilijua mapemaNdio hivyo alafu mtu kama huyu anakuja kukutafuta analalamika umemtenga, humsaidii kwa chochote.
Mi ni mwepesi sana kutoa msaada na hela ambazo hata sina 😂 ila kitu ambacho sipendi ni mtu kunitumia kujinufaisha, nikishajua na kubaini hilo ndio basi. Nabaini kupitia mambo kama hayo ya mtu kuona umuhimu wakati akiwa na uhitaji na hapa ndio binadamu wengi utawajua kuwa ni wema wakiwa na shida ila kiuhalisia sio.
Nililijua mapema wapi na muamala nilishafanya? Ila ndio mwisho nshamdeleteKwakweli, Bora wewe ulilijua mapema
🤣🤣🤣🤣dah hatari sanasiku nyingine akija muonyeshe ukatili.
kuna single mom alinitapeli elfu 30, akanitapeli tena laki 1. siku moja bwana akapata ajali akavunjika pua. mamaye hana hata hela ya hospital. kapiga simu, akatuma mpaka video akiwa hosp kweli ukiangalia kavunjika.
anaomba msaada nimsaidie huku analia. hana hela ku clear bill. mm nilimwambia atafute hela alizonitapeli azitumie kulipa bill. alimpa mpaka mdogo wake simu anibembeleze mm nimeweka ngumu. nadhani walisema huyu mmeru ni mtoa roho
Kuna watu wana tabia za ajabu mno, wakishavuka shida moja wanasahau kuwa sio mwisho wa shida na kusaidiwa, na hata kama ni mwisho kushukuru ni jambo la muhimu sana.Dah ila wanaume tunahuruma sana na hawa viumbe sema nao kwakujitoa ufahamu sifuri. Yan anashindwa kutoa tu taarifa kuwa kapata huduma na kuongeza maneno mawili matatu ya ukweli au uongoò???
Dah ndo wana wa adamu tulivyo
Imenisikitisha sana,binadamu wengine ni wa ajabu sana,usishangae akaanza kuwaambia watu wewe ndio ulimloga mwanae.Habari za asubuhi wana JF,
Iko hivi, nina rafiki yangu ana mtoto (naweza nikasema ni single mom) ila isieleweke vibaya, nilisomaga nae O level huko ila nikama bahati tu tumejikuta tunaishi tena mtaa mmoja.
Ijumaa jioni wakati natoka tu ofisini alinipigia Simu akaniambia anashida kama naweza nipitie nyumbani kwao nikamuone, kwakua nilikua sina ratiba nyingine nikasema isiwe tabu kabla sijafika nyumbani nikapitia.
Nilimkuta yuko good ila mwanaye alikua anaumwa sana ile mtoto kazidiwa na akaniambia ameshindwa kwenda hospitali hana hela na almost kila aliyempigia simu wamemuahidi tu tangu asubuhi na hakuna aliyemtumia mpaka muda huo sa 1 jioni inaelekea saa 2.
Kiukweli sikua na hela and i was totally broke, yaani wiki ile iliyoisha mwenyewe nimeishi tu kwasababu nina wazazi maana nilikua nina mambo mengi yananihitaji hela kiasi kwamba sikua nimebakiwa na hata Mia mbovu. Lakini nikasema kwenye suala la kuokoa maisha ya mtoto isiwe kesi nikamwambia ngoja nirudi kwanza nyumbani, nikamsimulia mama tukaongea na dada yangu wakasema tu hapa kwa harakaharaka hatuna namna tumdanganye tu mzee kitu chochote jioni hii atupe hela, kweli mzee bila hiyana tukamshawishi akanipa 150k nikamfata kwao tukaenda hospitali usiku uleule.
Mtoto akapewa huduma ya kwanza na baadhi ya vipimo wakamlaza ili asubuhi aendelee na matibabu mengine (muda wote huo anawapigia ndugu zake wakiwemo na baba wa mtoto hata simu hawampokelei wengine), asubuhi yake niliomba tu ruhusa kazini nikawaambia nitachelewa ili nione mtoto atakua anaendeleaje.
Case ya mtoto ikawa kubwa wakasema tuende nae hospitali nyingine kubwa (Peramiho nadhani watu wa songea wanaijua), kuna vipimo alivyoambiwa wampime vilikua vinahitaji hela almost kama laki 2 tena nikamwambia mama akanitumia tukafanikisha. Kwasababu kazini nilikua wanapigapiga sana simu na nikaona wanaendelea vizuri na mama yake alikua ashafika nikamwambia naenda ofisini incase kimetokea chochote utatuambia nikampa na namba ya mama kama mimi nisipopokea ampigie, nikaondoka. The bad thing is nilikua busy busy sana hadi siku ikaisha sikuwatafuta tena.
Kinachoniumiza ni kwamba, jana mchana nilimpigia simu hakupokea nikaenda kwao sikukuta mtu, nikaenda hadi Peramiho tena kulivyo mbali nikaambiwa wameruhusiwa na hakunipa taarifa. Kuanzia jioni nimeingia WhatsApp naona ameweka status nyingi nyingi kufungua nikawa naona amescreenshot miamala yote ya watu waliokua wanamtuma hela na kuwapa credits Mungu awabariki sana kwa kuokoa maisha ya mwanae maana alikua kwenye hali mbaya sana na nini nini. Screenshot kama kumi hivi na kitu na amewataja na majina kabisa...
Cha ajabu hiyo miamala hakuna hata wa mtu mmoja uliofikia hata 30k, wote ni hizo hizo tu efu10 ef5 ef7, kawaandikia macaption mazito mazito. Nimebaki najiuliza mbona alikua ananiambia hawapokei simu, na hela inaonekana walimtumia siku ileile ambayo aliniambja na mimi niende kwake kumuona.
Mimi ambayo nilikua nae kuanzia siku ile hadi usiku nikaacha na kwenda kazini na tumeclear bills zote hata asante hajaniambia na wala taarifa kama wameruhusiwa hajanipa. Nimesubiri jana yote hadi leo saizi hajanipigia hata simu, Kina mama wananiuliza wanaendeaje nawaambia tu wanaendelea vizuri huku roho inauma.
Nimetenda wema nimeenda zangu wakuu, lakini bado roho inaniuma aisee😥😥
Kanuni ya utoaji haki inasema: Ni lazima mtu asikie upande wa pili, upande wa pili ni lazima usikilizwe.Ushauri mbaya huo, usimtafute tena huyo rafiki yako. Kwa ufupi ishi naye kinafiki na/au ua kabisa huo urafiki.
Pole sana. Japo wanasema kwamba tenda wema nenda zako lakini hili linaumiza sana.Habari za asubuhi wana JF,

Yeah ni kweli, but sometimes kushukuru kunamfanya aliyekusaidia ajiskie vizuriPole sana. Japo wanasema kwamba tenda wema nenda zako lakini hili linaumiza sana.
Huyo ni mtu wa ajabu sana na Hathamini. Kata kabisa mazoea naye, kuwa na rafiki kama huyo kwenye maisha ni bure, na hakuna kitu mtakachojenga.
Anyways, amefanya vibaya sana,.. I pray for you mabaya makubwa yampate na kumpa funzo kubwa juu ya huu upumbavu alioufanya. Stay calm