Sijui ni uchawi huu?

Sijui ni uchawi huu?

Joined
Sep 10, 2019
Posts
17
Reaction score
15
Kwemah ndugu zangu?

Moja kwa moja kwenye mada, mimi ni mwanafunzi wa chuo Dodoma, muda kidogo kama miezi 4 iliyopita niliamia katika nyumba moja baada ya kushauriwa na mama mmoja mkazi wa eneo hilo aliyekuwa anasimamia hiyo nyumba ingawa siyo yake, nilikuwa pia namtumia katika kujenga hiyo nyumba yetu kama kuchota maji, mchanga, kujenga.

Nilihamia hapo sababu ni jirani na eneo ambalo nilikuwa nikisimamia ujenzi wa nyumba yetu, nikatafuta na mpangaji mwengine nikamuingiza bila kumshirikisha huyo mama na huyo mama akawa jirani yetu, hivyo tukawa wawili katika nyumba yote hiyo kubwa.

Baada ya kuingia katika ile nyumba nikawa mara nyingi ni mtu wa kulala sana, kushindwa kuamka mapema na kuchoka kupita kiasi, nikasema labda tiba ya hii hali niwe nafanya mazoezi ingawa kilingana na ratiba nikawa nashindwa kufanya labda itokee nimepiga push up kidogo au kuruka kamba.

Siku moja ambayo nilipanga mimi na rafiki yangu tufanye jogging, ikatokea kuna mjusi ambaye mara kwa mara nilikuwa nikimuona hapo ndani hivyo nikasema hiyo siku nimuue(ilikuwa mida ya saa 10). Alikuwa ukutani nikarusha teke nikamkanyaga ila sasa cha ajabu, niliua mjusi mmoja akawa pale chini lakini mikia ilikuwa miwili mizima kabisa, nikashangaa kweli.

Nikaomba kidogo nikapotezea baadae nikaenda mazoezi, hali ya kuchoka ikawa inaendelea baadae nikaanza kuwa najiuliza sasa ni mazoezi gani ambayo nitafanya yanitoe katika hii hali, je,kuruka kamba, kudanceau push up?

Baadae moyo ukawa unaniuma na kujiuliza maswali kama mazoezi nitafanya hadi lini na mbona mtu fulani hafanyi na yupo vizuri, inamaana siku zote maishani nitakuwa mtu wa mazoezi, watu ambao hawafanyi mazoezi wanaishi vipi maisha?!

Nikawa nakosa furaha kabisa, moyo unauma nikasema labda nitatizo la afya ya akili. Nimeenda hospitali nimetumia dawa miezi 2, wananielekeza lakini akili haitulii kabisa. Nafikiria jinsi ya kujitoa maisha.

Nimeenda kwenye maombi nikaanza kuota ndoto nyingi sana, kila siku hususan ile nyumba ninayoijenga inaharibika, mara nimuote yule mama jirani ni mchawi. Nasali sana natamani haya mawazo yatoke, nikitamani pia huyo mama limkute jambo ila bado.

Sasa nashindwa kuelewa je, ni maono, mawazo yangu, athari ya hizi dawa ama nini?!
 
ndugu ata mimi nimepaka na mama mmoja wa kimakonde yanayonitokea ni kama wewe kabisa,moyo inakua haitulii,nakosa raha, na akili kama inachanganyikwa nimeshaenda mpaka amana kwa afya ya akili lakini wapi!!
 
Hivi ukiota unafanya mapenzi na mtoto wa mwenye nyumba hii ina maana gani wakuu...huyu binti wa mwenye nyumba nilipitia mara moja ila kutokana na tabia zake mbaya nikapiga chini....
 
Hayo ni mapepo mahaba ambapo hufunga nyota yako isinawiri na kukufunga ktk kutoolewa/kutooa, kutopata mtoto, kutofanikiwa kiuchumi.
 
Ushauri huu unaweza kukusaidia niliwahi pitia hiyo hali unayopitia
Kuna mtu mmoja aliwahi sema ukiona umejaribu mambo yote kwa ushauri wa kisayansi lakini hali ni vile unahitaji nguvu zaidi ni hiyo ni NGUVU YA MUNGU

Jambo la kwanza amua kumkabidhi Yesu maisha yako uwe kiumbe kipya kwanza baada ya hapo Jifunze kuhusu Mungu huku ukiendelea na maombi ni suala la muda tu inakuwa imeisha suala omba pasipo kukata tamaa.

Hesabu 23:23 Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, Wala hapana uganga juu ya Israeli. Sasa habari za Yakobo na Israeli zitasemwa, Ni mambo gani aliyoyatenda Mungu!

Warumi 8:31 Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu?

Mungu awe nawe.
 
Kuwa karibu na Mungu na kufanya maombi mara kwa mara ukiombea hiyo hali iondoke,unatakiwa usimame vizuri kiroho na uishi katika usafi wa mwili na roho(jiepushe na maisha ya dhambi)...
 
Back
Top Bottom