Sijui nieleweje hii sms.

Billie

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2011
Posts
13,588
Reaction score
22,752
Habari zenu wapendwa mwenzenu siku kama nne zilizopita nilipokea sms kutoka kwa mpenzi wangu ikisema "Yaani mpenzi ujue una nguvu sana moyoni mwangu hivi umeniwekea nini?" kwa shauku ya kutaka kujua nika Reply "Kwa nin unauliza hivyo" mpenzi wangu akakaa kimya kidogo na kunijibu "Ujue kila nikitaka kukusaliti najikuta automaticaly nashindwa I REal love you"Sikujibu kitu tena nikabaki natafakali usemi wake huo sasa naona unazidi kujipa nafasi kubwa kichwani mwangu mara nijipongeze mara niuzarau mara niogope kuwa kumbe huwa anafanyaga majaribio kama hayo.Jaman naombeni mnisaidie kuitafakari na kudadavua ujumbe huu tafadharini naombeni mtumie busara kunisaidia maana naona kama ka Sms kananichafulia radha kwenye mapenzi yangu.
 
mmmh, ngumu sana.

Ukirushiwa mishale 20, uwezekano wa baadhi kukupata ni kubwa.

Watch out!
 
Yaani ushaona wapi mtu akajisifu mwenyewe?
Shtuka ngoma inamegwa hiyo!
Na siku utayoyofumania inshu, ndio presha itakavyopanda!
 
Ana matamanio ya kukusaliti, muulize huwa anafuata nini huko? Wala huna la kujipongeza. Kuna kitu anatafuta, sasa akikufikiria ndo anaghairi, iko Siku hatakufikiria, au utamkera atafanikiwa kukusaliti.
 
Makubwa! Sasa alikwambia ili kukudhihirishia kua hua anafanya majaribio ya kucheat au?kweli hamnazo..
 

Usijipongeze bado! Kazi unayo kubwa mkuu! Take care.
 
Sahizo ndo ngoma imepigwa anakupumbaza na maneno matamu SHTUKA!
 
pole sana billie: iinaoneka huyo mpenzio siyo mwaminifu, huenda.alihisi umeshtukia mwenendo wake, ikamlazimu azuge ili apate kujua kama umemshtukia au lah! Take care!
 
Inategemeana amekuambia mkiwa kwenye hali gani,sometimes unakuta mnachat au kuongea kwa feelings mpaka mtu anaamua kueleza ukweli wake tena kwa nia nzuri,na yote ni kukuhakikishia kuwa anakupenda,yeye kuwa wazi kiasi hicho kwako shukuru sana maana kuna wengine wanafanya mambo yao kimya.
Anakupenda wala usiumize kichwa,ni ujumbe wa kawaida kuelezea hisia zake ili umwamini
 
Huyo anajua umezama. anazidi kukuzamisha tu. teh teh teh.
 
kaka wanammega huyo, mie angeniambia hivyo ni issue nzito, wala usijisifie ujinga huo, if she ever atempted to cheat on you, she has cheated on you,

 
Nisaidie nichukue hatua gani sasa.


unauliza hatua? kwani lazima uchukue hio hatua?

labda kama humpendi hapo ni sababu ya kushiba ya kumuacha.

Atakutangaziaje anataka ku cheat? hakuheshimu? au ndo manjonjo yamezidi?
 
mapenzi bwana, ndo maana mm nishaamua kuwa MWASITI kitambo tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…