Sijui nieleweje hii sms.

Sijui nieleweje hii sms.

io ndo yaitwa asojua maana haambiwi maana,me naona mesej imejieleza ila umeitafcr peke ayo,apo ndo ulkua unapewa taarfa rasm kwamba anakusalit lakn labda kla akiwa ktk harakat hzo anapata vkwazo ndo anakuulza labda km kuna tego lolote umemtegeshea eb ltegue mwnyw aende na zake.TAFAKARI
 
kijana mi naona toka ile thread yako ya kwanza ulionyesha kutojiamini na mahusiano yako...sasa naona mamaa naye kaona bora atafute mwengine...anza kumchunguza kwa ukaribu...mulika mwizi
 
anakupenda sana kiasi kwamba huwa anajisikia vibaya anapo-do na mtu mwingine which is why huwa anamlazimisha jamaa acheue nje ili kukulindia heshima teh teh teh...
 
unatakiwa ujiulize ni kweli anashindwa kukucheat? au ana kufariji? kwa nini ajaribu kukucheat? hakupendi huyo! na kushauri na wewe huanze kujitoa mapema kabla hauja imba wimbo wa solemba!
 
Habari zenu wapendwa mwenzenu siku kama nne zilizopita nilipokea sms kutoka kwa mpenzi wangu ikisema "Yaani mpenzi ujue una nguvu sana moyoni mwangu hivi umeniwekea nini?" kwa shauku ya kutaka kujua nika Reply "Kwa nin unauliza hivyo" mpenzi wangu akakaa kimya kidogo na kunijibu "Ujue kila nikitaka kukusaliti najikuta automaticaly nashindwa I REal love you"Sikujibu kitu tena nikabaki natafakali usemi wake huo sasa naona unazidi kujipa nafasi kubwa kichwani mwangu mara nijipongeze mara niuzarau mara niogope kuwa kumbe huwa anafanyaga majaribio kama hayo.Jaman naombeni mnisaidie kuitafakari na kudadavua ujumbe huu tafadharini naombeni mtumie busara kunisaidia maana naona kama ka Sms kananichafulia radha kwenye mapenzi yangu.

Jaribujaribu yake ya kutaka kukusaliti iko siku atafanikiwa.
 
Nawe jaribu kumwambia vile vile kuwa: umejaribu mara kadhaa ku cheat, lakini moyo umekataa kwa ajili yake. Then angalia atakavyo react. Jibu utakalopewa na huyo demu wako, leta hapa jukwaani.
 
Nawe jaribu kumwambia vile vile kuwa: umejaribu mara kadhaa ku cheat, lakini moyo umekataa kwa ajili yake. Then angalia atakavyo react. Jibu utakalopewa na huyo demu wako, leta hapa jukwaani.
...............tena mwambie kitu kimefika kimiani, mara kikakataa !
 
Habari yako dada, i think kati ya wasichana wenye wapenzi waaminifu wewe ni mmoja wapo. Kama huyo mchumba wako kaamua kukwambia wazi kiasi hicho, ina maana na yeye ilikuwa inamuumiza sana akitafakari hayo majaribio aliyokuwa akitaka kuyafanya. So u re luck to have a man of that kind. Amini anakupenda kweli na sana. JIAMINI
 
mmmh, ngumu sana.

Ukirushiwa mishale 20, uwezekano wa baadhi kukupata ni kubwa.

Watch out!
Nimeipenda hii, ila ndugu Billie jifunze kupenda kupo na kuchukiwa kupo, kukubaliwa kupo na kukataliwa kupo, kumega kupo na kumegewa kupo ! Hapa ni kijitayarisha tuu na hayo majanga kisaikolojia. Zidisha 'control mechanics.'
Mwana.F.A anasema yeye akimegewa na yeye anamtafuta mnyonge na yeye anammegea, at least inamliwaza !
 
Habari yako dada, i think kati ya wasichana wenye wapenzi waaminifu wewe ni mmoja wapo. Kama huyo mchumba wako kaamua kukwambia wazi kiasi hicho, ina maana na yeye ilikuwa inamuumiza sana akitafakari hayo majaribio aliyokuwa akitaka kuyafanya. So u re luck to have a man of that kind. Amini anakupenda kweli na sana. JIAMINI

ndugu mimi ni wa kiume ila nashukuru kwa ushauri wako mzuri.
 
Uuuuuuuuhhhhhh
Habari zenu wapendwa mwenzenu siku kama nne zilizopita nilipokea sms kutoka kwa mpenzi wangu ikisema "Yaani mpenzi ujue una nguvu sana moyoni mwangu hivi umeniwekea nini?" kwa shauku ya kutaka kujua nika Reply "Kwa nin unauliza hivyo" mpenzi wangu akakaa kimya kidogo na kunijibu "Ujue kila nikitaka kukusaliti najikuta automaticaly nashindwa I REal love you"Sikujibu kitu tena nikabaki natafakali usemi wake huo sasa naona unazidi kujipa nafasi kubwa kichwani mwangu mara nijipongeze mara niuzarau mara niogope kuwa kumbe huwa anafanyaga majaribio kama hayo.Jaman naombeni mnisaidie kuitafakari na kudadavua ujumbe huu tafadharini naombeni mtumie busara kunisaidia maana naona kama ka Sms kananichafulia radha kwenye mapenzi yangu.

huwenda ashakusaliti,anajishaua tuuuu
 
You are finished!

Ila kama wewe ndo kakupanga wa ndoa, mtaoana tu.

Kumbuka, sharing is caring.

sometimes huwa nafikilia kama inawezekana ameshindwa kutumia lugha vizuri labda alimaanisha kuwa hawezi kabisa kufikilia kunisaliti kwa kuwa ananipenda sana imenibidi nijidanganye kwa style hii kwa kuwa sijawahi kufuma usaliti wowote
 
kaka huyo ni girlfriend wenu na sio wako peke yako ila usijali kaka kumegewa ni jambo la kawaida japokuwa wewe ameanza kuku-alert wengine huwa unamegewa bila ya kujua.
Hao ndio Mama zetu, shangazi zetu, dada zetu n.k na hizo ndio tabia zao inabidi uzizoee na uvumilie ukiona yamezidi tupa kulee!!
oops! Ningejua umri wako ningeweza ku-comment zaidi juu ya hiki ulichokisema. Lakini kwa kifupi, ku-cheat sio suala la kuwa mwanamke (mama, shangazi, dada kama ulivyosema), kila mtu anaweza kudanganya katika mapenzi. Hata wanaume wanadanganya sana. Tena nawezakusema wanaume ndio zaidi kuliko wanawake. Hapo umepotosha mada, wakiiiona wenyewe watakushambulia mpaka ukimbie jamvi.Toa ushauri wako bila kupotosha mada ndani ya mada.
 
Kwenye ile thread nyingine nilikushauri achana na huyo mwanamke.
Utakufa kwa presha bure.
 
Back
Top Bottom